Ndugu michuzi naomba unifikishie ujumbe huu ili mmmiliki wa kampuni ya Dar Express aione na kuifanyia kazi.
Mimi ni msafiri wa mara kwa mara kwa kutumia basi la Dar Express kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi na kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam. Kwa ujumla ndugu Michuzi huduma za usafiri za Dar Express zilikuwa nzuri mwanzoni lakini kwa sasa haziridhishi kabisa na abiria wengi wamekuwa wakilalamika. Malalamiko yangu na ya abiria wengi yamejikita katika mambo yafuatayo:
1) Kwenye Mizani:
Pamoja na kwamba abiria wanalipa nauli kubwa (shilingi 55,000 Tsh au 3,500 Ksh) kwa safari abiria wamekuwa wakishushwa kwenye basi mara basi linapokaribia kwenye Mzani uliopo njia panda. Kwa kawaida abiria wa viti vya nyuma huwa wanashushwa pale katika stendi ya Himo na kupakiwa kwenye gari ndogo (taxi) ili kuvushwa kwenye mzani.
Abiria hao hupakiwa tena kwenye basi baada ya basi kuwa limepimwa uzito kwenye mzani wa Himo. Kwa pale Namanga utaratibu ni kwamba baada ya abiria kugonga paspoti zao wanatakiwa kurudi kwenye basi ili liweze kupimwa uzito. Cha kushangaza ni kwamba kondakta wa basi huwapakia baadhi ya abiria kwenye gari ndogo aina ya NOAH na kuwasafirisha zaidi ya kilomita tano halafu wanashuka na kusubiri basi.
Pia wakati basi linakaribia Mzani wa Himo/njia panda kutoka Nairobi abiria pia wanashushwa kwenye kituo cha mafuta karibu na mzani na kupakiwa kwenye taxi na kuvushwa kwenye mzani mpaka stendi ya Himo.
Hali hii kwa ujumla inaleta usumbufu kwa abiria na pia ni kinyume na taratibu na sheria za nchi kwani hii ni janja ya kukwepa ushuru na pia kuharibu barabara zetu. Katika hili nawaomba pia abiria wanaotumia usafiri wa barabara kukataa kushuka kwenye mabasi mara wanapoombwa kufanya hivyo.
Ndugu Michuzi katika hili naomba pia kama una namba ya simu ya Magufuli (Waziri wa ujenzi) uiweke hapa ili siku nyingine nimpigie moja kwa moja na kumjulisha.
2. Basi kutokupita stendi ya Moshi na Arusha:
Kwa kawaida gari linapaswa kupita stendi ya Moshi na Arusha na kwa uelewa wangu huu ni utaratibu kwa mabasi yote. Lakini cha kushangaza ni kwamba basi linalokwenda Nairobi na kutoka Nairobi kwenda Dar es salaam mara nyingi hawapiti stendi za moshi na Arusha na wala abiria hawataarifiwi kabla.
Mara nyingi kunakuwa na abiria wenye vifurushi vidogo vya mkononi ikiwa ni pamoja na fedha kwa ajili ya kuwapa ndugu na marafiki zao ambao wanakuwa wanasubiri basi hilo kwenye stendi za Moshi na Arusha. Kwa kuwa basi halipiti stendi na abiria hawafahamishwi hii inaleta usumbufu mkubwa kwa abiria.
3) Huduma ya chakula:
Ukitaka kusafiri kwa magari ya Dar Express na kama ukitaka kula lazima ule kwenye hoteli yao Korogwe. Hili sina shida nalo sana lakini tatizo langu ni abiria wanaotoka Nairobi na kufika Korogwe kuanzia saa tisa na kuendelea ikiwa ni pamoja na watoto wadogo.
Ukizingatia kwamba basi halikupita stendi ya Arusha wala Moshi na safari kutoka Nairobi inaanza saan 12.30 Asubuhi ni vigumu kwa abiria kusafiri kwa zaidi ya masaa kumi bila kupata huduma ya chakula. Ni vyema abiria wanaotoka Nairobi wakapata nafasi ya kula chakula Arusha au Moshi badala ya kuwapeleka mpaka Korogwe.
Huduma ya maji na soda inayotolewa kwenye basi kuanzia saa saba mchana haitoshi.
Ukataji wa tiketi:
Kama unasafiri na basi la Dar Express kwenda au kutoka Nairobi lazima ukate tiketi yako siku moja kabla ya safari. Ukitaka kupata tiketi kabla ya hapo huwezi kupata.
Kwa abiria wanaoanzia Moshi kwenda Nairobi ukienda kununua tiketi hata kama ni siku moja kabla ya safari huwezi kupata kwa kisingizio kwamba tiketi za kuanzia moshi zinauzwa siku ya safari.
Hii inakuwa ni usumbufu kwa abiria wanaoanzia safari moshi kwani mara nyingi basi linajaza abiria kutoka Dar Es Salaam hii ina maana kwamba ukisubiri mpaka siku ya safari huwezi kupata nafasi. Ili kuwa na uhakika wa safari abiria analazimika kununua tiketi ya kuanzia Dar es salaam kwa shilingi 55,000Tsh ili kuwa na uhakika wa kusafiri wakati nauli ya kutoka Moshi kwenda Nairobi ni chini ya 30,000 Tshs.
Kwa sababu kampuni imewatangazia abiria kwamba kuna usafiri wa Moshi Nairobi basi ni vyema wakawa na utaratibu wa kutenga viti kwa ajili ya abiria wanaoanzia safari moshi vinginevyo waweke wazi kwamba hakuna nafasi kwa abiria wanaoanzia safari moshi. Mimi ni miongoni mwa abiria niliolazimika kulipa 50,000 Tsh kutoka moshi kwenda Nairobi.
Ni vyema viongozi wa kampuni wakaangalia tena upya utaratibu uliopo na huduma kwa abiria kwa lengo la kuboresha huduma kwa abiria vinginevyo abiria watapoteza imani na kuhamia kwenye kampuni zingine.
Ni mimi mtumiaji wa Basi la Dar Express (Dar - Nairobi - Dar)
Tafadhali usiweke email wala jina langu kwa sasa.
Asante
Happygod
Michuzi hivi malalamiko nyeti kama haya huwa yanaishia hapa hapa kwenye blogu au Michuzi Blog ina system ya kuyafikisha kwenye sehemu husika kwa hatua zaidi? Ningependa sana kujua hili. Najua ni vigumu ku deal na malalamiko yote lakini kwa hili wanachofanya Dar Express ni ukiukwaji mkubwa wa sheria. Inawezekana mmiliki wa Dar Express hajui kinachoendelea barabarani. Badala ya malalamiko kama hayo kuishia tuu hapa, ingekuwa vizuri kama tungepata feedback toka kwa wahusika kupitia Michuzi Blog juu ya hatua zilizochukuliwa. Au kama kuna watu wako karibu na mhusika, wanaweza kuwakilisha hayo malalamiko na kumpa update Michuzi ili aweke kwenye blog. Vingine kama malalamiko yataishia kwenye mtandao tuu, hakuna kitakachofanyika.
ReplyDeleteKula five mdau hapo juu.
ReplyDeleteDar express zamani walikuwa wanatoa huduma mzuri kwa sababu kulikua kuna kitu kinaitwa SCANDINAVIA EXPRESS. Dar expr walikua wanaiga service za kule sasa modal imekufa, na wao ubunifu hakuna. wanashida ganni wakati hakuna competition?. Muchuzi fikisha comments hizi kwa wahusika wa basi, may be watajirekebisha.
ReplyDeleteKwa kweli huduma za hilo basi kwa sasa ni mbaya sana wiki iliyopita nilisafiri na basi hilo kwenda Arusha. Lakini tukiwa njiani dereva akawa anayapita magari kwa fujo sana ikafikia anapita magari yapatayo matano bila kujali magari yanayokuja mbele yetu. Ili kujaribu kutatua tatizo hili abiria wakalalamika na pia condakta akaitwa na kuombwa kumsihi dereva awe makini. Cha kushangaza dereva akakasirika na kuanza kutembea polepole yaani alitembea mwendo kama wa mtu atembeavyo kwa miguu. Basi tulipofika Chalinze tukamtaarifu trafik ambaye alimchukua na kumpeleka kituoni walipofika kituoni ikabainika kuwa ananuka pombe n a pia hana leseni. Kufuatia hali hiyo abiria walimkataa dereva na kumpigia simu mmiliki wa mabasi hayo lakini tukashangaa akawa anakataa kutusaidia akidai kuwa dereva wake ni mzoefu na kuwa anamuamini ila tuu sisi abiria tuna gubu. Baada ya mabishano makali ilipofika saa 10 jioni mmiliki ndio akakubali kuleta dereva mwinine ambapo tulifika Arusha saa sita usiku na hata dereva aliyeletwa mara hii ya pili pia alikuwa na maneno mengi ya kejeli kwa biria.
ReplyDeletePia mwezi uliopita nilisafiri na basi hilO hilo tena na dereva wa kwanza niliyemtaja hapo juu alifanya vituko hivyo hivyo abiria walipomkanya kuwa apunguze mwendo alianza kutembea polepole tukachelewa kufika dar dereva huyo hataki kabisa kukanywa na anaendesha gari vibaya sana sana
Najiuliza hivi nduGu Mremi analijua hili au ni nini kinaendelea kwake.
Si hayo tu , hata lugha ya wahudumu si nzuri. Hata abiria akitaka kuchimba dawa inakuwa matusi matupu...inaonekana kama wana haraka sana...spidi hiyo usiseme. siku gari likipata ajali hakuna atakayeomba maji..... Dar express wapande tu wavuta bangi ndio wanawezana nayo. binadamu mwenye akili nzuri ni shida tupu
ReplyDeleteHATA YULE DADA ANAYEKATA TICKET PALE OFISI YA NAIROBI NI MJEURU KUPITA KIASI,NA HATA UKIMTISHA UTARIPORT OFISINI DAR KWA WAHUSIKA ANAJIBU YEYE HAOGOPI CHOCHOTE HATA WENYE BASI ANAMJUA YEYE NANI!!! SIKU ALIPONIJIBU HIVYO ILIBIDI NINYAMAZE KIMYA NIKAWA NAJIULIZA AU NI NYUMBA NDOGO YA MWENYE BASI? KWANI HICHO KIBURI SIO CHA KAWAIDA.
ReplyDeleteWATANZANIA TUUNGANE SAUTI IWE MOJA TUSINGOJEE, TUNAOMBA MMILIKI WA MABASI YA DAR EXPRESS HATUJIBU OFFICIAL, JAPOKUWA MIE BINAFSI NA DAR EXPRESS BASI TUBAKOELEKEA NI YALE YA CHINJA CHINJA
ReplyDeleteNafikri kwenye tiketi kuna namba ya mmiliki kama sijakosea.
ReplyDeleteWatu bana!!! biashara ya usafirishaji ni ya ushindani kuna aina nyingi sana ya usafiri unaweza kutumia kutoka Dar-Nairobi sasa unapolalamika huduma ya Dar express peke yake wakati aujalazimishwa kupanda!badilisha usafiri wakikosa wateja watajirekebisha!!
ReplyDeleteMichuzi please tusaidie kulifikisha kwa wahusika huu ni uhujumu uchumi,barabara zinatengenezwa kwa gharama kubwa sana sasa hawa wahuni wanafanya upuuzi wao huu kwa tamaa zao to the expense ya walipa kodi,wanajaza mizigo mingi sana na kutuharibia barabara.Tatizo lingine ni kwa abiria,kwanini ukubali kushushwa kwenye basi na kupakiwa kwenye tax ili kuwasaidia hawa watu kukwepa kodi na kuvunja sheria? kwa nini ukubali usumbufu wote huo wa kupanda na kushuka? hivi ukiumia au hiyo tax ikapata ajali na ukaumia au kufa utadai kwa bima gani? bima ya mwenye basi au tax.Abiria acheni kuburuzwa kamavile mmepewa lift.
ReplyDeleteHuduma za Dar express kwa kweli zimekuwa mbaya sana siku hizi,wahudumu wao hata kugawa maji siku hizi hawagawi wanachofanya ni kuweka box la maji katikati kenye njia ndani ya basi halafu kila abiria anainuka mwenyewe kwenda kujichukulia maji,hebu fikiria usumbufu wa abiria kuinuka kujichukulia maji wakati basi liko kwenye mwendo na mara nyingine una mtoto, sijui kama uongozi wao wanalijua hili.Kitu kingine ni kwamba abiria wakisha kula pale kwenye hotel yao korogwe mkiingia kwenye basi wahudumu wanaweka box moja au mawili ya kuwekea uchafu au mabaki ya chakula pale kwenye kinjia ndani ya basi,uchafu huo hauondolewi mpaka mwisho wa safari na wakati mwingine uchafu unasambaa ndani ya basi inabakia kuwa kero tu kwa abiria. Dar express mtabakia na jina tu lakini sifa nzuri mliyokuwa nayo haipo tena vinginevyo mjirekebisha.Msipojirekebisha tutawapeleka kwenye vyombo vyote vya habari.
Hata yule dada wa ofisi ya arusha mara nyingi huwa anajibu anavyofikiria yeye mwenyewe kama vile hajui wajibu wake .
ReplyDeleteInabidi michuzi utusaidie kufikisha huu ujumbe kwa mhusika au tupatiwe namba ya mhusika.
Kwa kweli huduma za Dar-Express zimekua mbovu,kuanzia mwendo kasi,magari mabovu na huduma ndani ya gari n.k na wanajivuna kwasababu ukiangalia kusafiri na Akamba au Kampala couch ni kufika usiku na the buses are not comfortable.
ReplyDeletePia Kilimanjaro Express walikua wanatoa huduma ya usafiri Dar-Nairobi-Dar na huduma pia zilikua nzuri lakini walikua wanalalamika wateja hamna..Kwa kweli kama hawatajirekebisha ni bora kutafuta usafiri mwingine mbadala kuliko kuatarisha maisha maisha ya watu.
Mdau wa 8:56 nakupa big up, hivi kwa nini nyinyi abiria munyanyaswe na muuza tiketi, dereva, konda, mwenye basi, na bado munaendelea kupanda hilo basi tu? Kwani muna ubia au munapunguziwa nauli?
ReplyDeleteAchaneni nae aoze na mabasi yake kama ameshindwa kuhudumikia abiria ipasavyo na tutaona kama ataendelea na maringo yake.
WATANZANIA TUAMKE TUACHE UJINGA WA KULALAMIKA OVYO WAKATI TUNAWEZA KUWANYOOSHA HAWA WAFANYA BIASHARA.
Mbona Mhusika anaweka direct numba ya kupiga kama kuna Matatizo!! Let just be fair to the owner and call him to tell the problem!!
ReplyDeleteKuna mdau amesema hapo juu kwamba mwenye kampuni aliwahi kupigiwa simu wakati dereva wake akiendesha gari akiwa ana harufu ya pombe na kushikiliwa na polisi pale chalinze lakini mwenye kampuni akadai si kweli na anamwamini sana huyo dereva wake baada ya mambo kuwa magumu then akatuma dereva mwingine.. sasa huoni hapa mwenye kampuni anawatetea madereva wake?? Mimi nafikiri ni vyema mwenye kampuni akafanya utafiti wa malalamiko ya abiria wake ambao ndiyo wateja wake then baada ya hapo akikuta kuna ufisadi atafakari achukue hatua hata kama nikufanya maamuzi magumu afanye.
ReplyDeleteNI KWELI HUDUMA ZA DAR EXPRESS NI MBOVU SANA.CHA MUHIMU NI KUSUSIA HUDUMA ZAO. MABASI YAKO MENGI. TUWASUSIE JAMANI.
ReplyDeleteNamba za simu zilizopo katika tiketi ukizipiga wanapokea wafanyakazi waliopo katika vituo husika ambao nao hujibu vibaya sidhani kama mmiliki ameweka namba yake hapo katika tiketi.
ReplyDeleteHata hivyo ningependa kushauri huwa mmiliki wa basi akifanya/akikiuka kanuni za usafirishaji anaweza kuripotiwa SUMATRA. SUMATRA wanapokea malalamiko kupitia fomu maalum ambayo inapatikana katika mtandao wake zipo za kiswahili na kingereza. SUMATRA wanaweza kumuamuru mmiliki kulipa fidia au kutoa adhabu yoyote kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo ni muhimu sana kwa mmiliki kufanyia kazi malalamiko ya wateja maana sio kila jambo SUMATRA ina mamlaka ya kulisikiliza mfano kutotoa soda au kukataa mteja kuruhusiwa kuchimba dawa n.k.
MH Hii ni Hatari sana nakumbuka Mwaka jana nilishauriwa sana nisiipande hili basi kwa sababu kama hizi...MR MREMI acha kucheka na hawa ndugu tatizo Ni nini???mbona DAR EXPRESS ilikuwa inaongoza kwa kusifika...Kwa AJALI ni mda mrefu sijasikia
ReplyDeleteKUNA TATIZO ,,,,
Chukua HATUA MAPEMA
Na hiii Hija na hizi Comment zinajenga na Umtafute Ndugu MICHUZI Umpongeze kwa kuwa na hii Blog....................
Kuhusu pombe ni kweli. Madereva wakifika pale kwenye hotel yao Korogwe breck ya kwanza ni pale kaunta ya baa na kupata moja baridi kuna wengine wanapataga redbull na wengine kinywaji cha kwenye chupa kama wanabisha nitawapiga picha siku moja na kuiweka hapa jamvini. Pia gari lilokuwa linaenda Nairobi tarehe 16/8/11 kodakta wa basi kama sikosei jina lake ni makundi alikuwa anawakejeli kina mama waliokuwa wanaomba kuchimba dawa.
ReplyDeleteSahihisho ndugu Michuzi: Ni konda wa gari lililokuwa linaenda Nairobi Tarehe 14/8/11 na wala siyo la tarehe 16/8/11. Samahani kwa usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na post yangu ya awali kuhusu kejeli ya konda kwa kina mama walioomba kuchimba dawa....
ReplyDelete