Mkurugenzi wa Taasisi ya Allure International,Jacqueline Kamukala (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandalizi ya hafla ya itakayofanyika katika Hoteli ya Moven Pick Agosti 6,jijini Dar es Salaam.kulia ni Afisa Mahusiano wa Taasisi hiyo,Rio Paul na kushoto ni Mratibu wa Hafla hiyo,Martin Kadinda.
Taasisi ya Allure International kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeandaa hafla ya hisani itakayofanyika katika Hoteli ya Moven Pick Agosti 6, mwaka huu kwa ajili ya kunua vifaa vya macho kwa hospitali zetu za rufaa Tanzania ili kukomesha matatizo ya macho katika jamii nchini.
Taasisi hii ya Allure International imeamua kuanza na mikoa miwili ya Tanzania ambayo ni Mwanza-Bugando na Mbeya.
Hafla hiyo inakusudia kusaidia kuboresha hospitali zetu za rufaa vile kusaidia watu wasio na uwezo kupata huduma za macho sawa na wengine nchini Tanzania.Harambee hii itasaidia kupatikana kwa vifaa vya tiba mahususi kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa wa macho Nchini.
Vifaa hivyo vitakapopatikana vitapelekwa katika Hospitali za Rufaa za Bugando, Mwanza na Mbeya kutokana na ukweli kwamba huko mikoani ndipo kwenye matatizo mengi ya macho na watanzania wengi wamekuwa wakipuuzia swala hili wakati wengine wakipata shida ,mateso hata kupoteza maisha yao.
Kampuni hii kwa kushirikiana na Wizara ya Afya tumeamua kuandaa hafla hiyo ili kusaidia upatikanaji wa vifaa hivyo.
Katika kusherehesha hafla hiyo, kutakuwa na mambo mbalimbali hususani burudani ambapo Bendi ya B Bendi, Simba Tradition Dancers, Fashion show kutoka kwa wanamitindo wa Tanzania, na hotuba kwa mgeni rasmi.
Harambee hii imedhaminiwa na; Serengeti Breweries Tanzania, Nssf, Clouds Fm Sozmy International, City Star Boutique bila kusahau Golden Fork Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...