"....Mjomba tushakwambia wese hakuna na kamba hiyo unaiona, mbona mbishi hivoooo..." anasema dada kuleee katika sheli ya Gapco mtaa wa Samora na Pamba jijini Dar jioni hii ambapo kuna baadhi ya sheli zimegoma kutoa huduma kwa kukaidi amri halali ya EWURA ya kushusha bei za wese. 

Jioni hii ilikuwa tafrani sehemu nyingi za jiji la Dar na kwengineko mikoani na wafanyabiashara wengine walisikika wakitamba kuwa wese hawatoi na hakuna wa kuwafanya lolote. Hata hivyo kuna sheli kibao zimetii amri na kuendelea kutoa hudma kwa bei iliyopangwa, huku wakilalamika lakini kwamba wanakula hasara kwani bei waliyonunulia ni ya juu zaidi. 

EWURA wamesema wanafanya uchunguzi na atayebainika kubania wese kwa makusudi hatua zitachukuliwa. Adhabu ya mfanyabiashara aliyekiuka agizo hili ni faini isiyozidi sh. milioni 3 ama kifungo cha miaka mitano jela ama vyote kwa mpigo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwani bongo kuna serikali au nchi inajiendesha yenyewe?achana na mafuta,kuna shule katika mitaa ya mbagala bado wanakaa kwenye mawe kama enzi za ujima au stone age.
    Kweli Siasa ni adui wa maendeleo.

    ReplyDelete
  2. Price controls ni disaster! Acha market ifanye kazi yake. Ni mambo ya supply na demand.

    Long Live Free Market Capitalism!

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu inaonekana hujui nini kinachoendelea kuhusu mafuta Duniani,mbona price control ndiyo inayotutesa siku nyingi,wazalishashi wa mafuta ,tuite nchi za kiarabu wanapanga wazalishe na wauze mafuta kiasi gani ili kucontrol bei na uchumi wao na huko ndo tatizo linakoanzia,wangeuza kadri walivyo nayo thamani yake ingekuwa sawa na maji ila wauzaji wa mafuta TZ walichokifanya jana na leo ni kielelezo cha aina ya serikali tuliyonayo na kwataswira hii haitatokea hata siku moja tukaendelea.Hakuna umeme hakuna mafuta ya taa kwa ajili ya kandili zetu matatizo tupu bongo

    ReplyDelete
  4. ths z gud..atleast bongo kuna some sort of protest tht actually works..in the long run serikali lzm wa sort out the problem cz kila mtu anaumia cz of ths...sasa ndio mtaona if the serikali z on ur side or not

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...