Bosi wa zamani wa Benki ya Dunia Dominique Strauss-Kahn ameachiwa huru baada ya Mahakama ya Manhattan, New York, nchini Marekani kufuta kesi yake ya kubaka baada ya waendesha mashitaka kuomba kesi hiyo ifutwe kile kilichodaiwa ushahidi hafifu na uwongo wa mshtaki mfanyakazi wa hoteli Nafissatou Diallo. Waandamanaji kibao walifika mahakamani hapo kushinikiza afungwe kwa kitendo hicho, lakini ndio hivyo tena mahakama imemuachia na amekuwa huru kurudi nyumbani kwake Ufaransa ambako wachunguzi wa mambo wanasema anaweza kusimama kugombea Urais wa nchi hiyo katika uchaguzi ujao.
Mwanamke huyo wa Afrika Magharibi mwenye umri wa miaka 33 alidai Strauss-Kahn (62) alimshambulia kingono katika hoteli ya Sofitel kitongojini Manhattan mnamo Mei 14, mwaka huu. Bosi huyo wa zamani wa Benki Kuu alikamatwa ndani ya ndege ya Air France alipokuwa akijaribu kutoroka Marekani. Pichani anaonekana Strauss-Kahn na mkewe Anne-Sinclair pamoja na wakili wake wakitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru. Uchunguzi w DNA ulithibitisha kwamba Strauss Kahn alifanya ngono na mwanamke huyo lakini hiyo haikutosha kuthibitisha kwamba kitendo hicho kilikuwa kwa kulazimishwa au la.
hii inasikitisha sana manake huyu mzee ana tabia ya kupenda wanawake ni alimshika kweli yule mwanamke ila tu pesa ndio imefanya vitu vyake hapo.... atabaka tena mwingine huyu manake anajua ni atatolewa tu kwa pesa yake. how sad. na angekuwa mtu mweusi hapo ni angeenda tu jela lakini sababu ni mweupe anaachiwa HURU.... vitu vingine ni vya kijina manake kama yule mchezaji wa mpira MICHAEL VICK kaenda jela sababu ya kupiganisha mbwa huyu kabaka kweli na anachiliwa, kwa kweli inaudhi alichokosa tu ni kazi yake nzuri la sivyo ataendelea kuishi kifahari mstzzz
ReplyDeleteANGELIKUWA MZUNGU INGETHIBITIKA KABAKWA NA HASA BAADA YA HIVYO VIPIMO VYA DNA KUTHIBITIKA LAKINI NI MUAFRIKA IMESHAPAMBWA KUWA ALITAKA MWENYEWE EH MOLA TUEPUSHE WAAFRIKA NA MABALAA HAYA HASA TUISHIO UGHAIBUNI
ReplyDeleteKesi umeshinda , kimbembe nyumbani angalia mama alivyo na usongo mkifika home! pambaf
ReplyDeleteBosi wa zamani wa "Benki ya Dunia" na "Benki Kuu?" Au wa Fuko la Kimataifa la Fedha (IMF)?
ReplyDelete