Na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka Zanzibar kinatarajia kuanzisha Stashaada ya Uhazili ya Uhasibu (POST GRADUATE) mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Chuo Hicho,Kamal Kombo Bakari wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Chuo hicho huko Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
Amesema kuwa mbali ya Masomo yalioanzishwa ya Basic Sataficate na Diploma ya kawaida lakini Chuo hicho mwaka huu kinatarajia kuanzisha Stashahada hiyo ya Uhazili ya Uhasibu (POST GRADUATE).
Amesema wameamua kufanya hivyo ili kulingana zaidi na Vyuo vinavyotoa Elimu ya Juu hapa Nchini kwa makusudi ya kuongeza Program za Masomo ya Kati na Stashaada za juu zaidi.
Bw. Kamal amesema Masomo yanayotolewa na Chuo hicho cha Uhasibu Chwaka yanaendeshwa na Walimu wenye Utaalamu wa kutosha pamoja na kufuata vigezo na Mitaala inayokubalika Kitaifa.
Mkuu wa Chuo hicho cha Chwaka ametowa wito kwa Wanafunzi wenye sifa za kujiuga na Chuo hicho kuitumia fursa hiyo kwa kujipatia elimu ya juu inayokwenda na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia kwa kuanza kwenda kuchukuwa fomu mwezi huu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...