Mh.Balozi Mwanaidi Maajar alipoingia kwenye park kwa kujaribu kuwaelewesha Watanzania waishio DMV kuhusu DICOTA na umuhimu wa kujivunia sherehe za Uhuru kwani miaka 50 si kitu kidogo
Mh.Balozi akisalimiana na wadau waliokuwepo kwenye nyama ya DICOTA SUMMER EVENT
Mama Munanka nae akisalimiana na Asha Nyang'anyi
Mh.Balozi akitayarisha mawili matatu ya kuongea kwenye mkutano huu wa DICOTA ambae baadae aliruhusu maswali
Mama Munanka akisaliamiana na Muganda huku Mh.akiongea jambo
Mh Balozi akiongea na Watanzania wannaoishi DMVna umuhimu wa kujiandisha mapema kwenye mkutano wa DICOTA utakaoenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya UHURU.
Watanzania waliofika leo,wakimsiliza Mh.Balozi


Ni vizuri kuona watanzania wakishirikiana namna hii. Lakini jambo moja ni kwamba kama tungeweza kutoa muda angalao wa kuomboleza waliofiwa. Hii shughuli ingefanyika next Sunday. Tumekuwa na misiba mitatu kwa mpigo na Jumamosi tumemuga kidee kwa huzuni kubwa, na jioni ile ile tukaenda kwenye Msiba wa Thomasi kule Riverdale, yote hayo ni matukio ya huzuni na hawa watu tulikuwa tuna wajua sana na ni marafiki zetu.
ReplyDeleteNext day, jumapili tuko kwenye Nyama choma na Mziki mkubwa tu unapigwa. Na ukiangalia utaona kwamba watu wanatengemewa kuja ni wale wale waliokuwa kwenye misiba hii. Maoni yangu ni kwamba tungetoa muda angalao watu watulize akili kidogo....Asanteni sana.
Nakubaliana nawe hapo juu, misiba ni yetu wote. Pamoja na majonzi yote tuliyokuwa nayo Jumamosi tulikuwa hatuna budi kuendelea na hii event sababu kubwa ni kuwa matayarisho yake yalikwisha fanywa muda mrefu (venue ilikwisha lipiwa na manunuzi ya perishable items yalikwisha fanywa). Ndiyo sababu kubwa iliyotufanya kutoahirisha hii shughuli. Pili muda tulionao mpaka DICOTA conference ni takribani mwezi mmoja na tuna deadlines za kuzimeet for malipo na confirmation, hivyo tulitaka habari hii iwafikie watanzania wote wa hapa mjini DC, na vitongoji vyake ili watu wajiweke sawa financially kujiandaa kuregister for the conference. Wote tupo pamoja katika misiba hii na nilikuwepo kwenye shughuli zote za misiba na niliwaona wengi tuu waliojumuika nasi kwenye misiba yote walikuwepo hapa kwenye DICOTA summer get together EVENT, nadhani cha msingi hatukuingilia program yeyote ya sala au harambee, hapo nadhani ingekuwa issue. Nawaomba watanzania wenzangu tuendelee kushirikiana katika masuala yote ya huzuni na furaha. Nawashukuru nyote mliofika na nadhani madukuduku yote yalijubiwa vizuri na Mheshimiwa balozi. Mwanakamati Local Committee
ReplyDeleteNimekuelewa
ReplyDeleteAsante.