Hapa Dr Lawi Kupaza akijiandaa kuingia kwenye Operation ambayo kwa mujibu wa maelezo yake ilikuwa ni operation ngumu sana na imempa changamoto kubwa sana katika kazi yake ya Udaktari.
Hapa akiwa na mmoja wa wagonjwa wake ambao alishawahi kumfanyia operation na anaendelea vizuri, kama mnavyomuona hapo akiwa na furaha kubwa kupiga picha na Daktari wake.

Dr Lawi kupaza ni miongoni mwa madaktari wachache ambao ni hazina katika taifa letu la Tanzania, ni Daktari ambae anatambua maadili (ETHICS) za udaktari na kutambua kua Udaktari ni wito ambao mwenyezi Mungu amekupa ili uweze kuwasaidia wengine ambao hawana uwezo katika matatizo mbali mbali yanayo husu afya zao, 

sisi binafsi kama Blog ya Mtanzania Halisi (KAPINGAZ) tunampongeza sana kwa jitihada zake za kuisaidia hii jamii ya kitanzania ambayo kwa sasa imegubikwa na matatizo mengi sana hasa ya kiafya, 

ukiangalia upande wa madawa ni shida na pia upande wa Wataalam wa afya hasa hawa wa udaktari ni wachache au wengi wao wakihitimu katika vyuo vyetu huenda kufanya kazi katika Hospitali za Nje ya Nchi yetu. 

Tunamtakia maisha marefu na yenye fanaka katika kuiendeleza fani yake ya udaktari na aweze kuwasaidia watanzania wengi zaidi. 

kwa awasiliano zaidi mpigie kwa namba yake hii +255 715 645216

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongera mdau...mungu akuzidishie.

    ReplyDelete
  2. Ughaibuni watakupa viza uje uwatibu na mshahara wako utaonezeka mara kumi kwa huo unaopata huko.

    ReplyDelete
  3. SASA ULIZIA VIZURI MAISHA YAKE... UTAKUTA YA KISHIDA SHIDA TU... MADAKTARI WENZIE USA, UK, N.K USISEME.... MUNGU AKUPE NGUVU WAKATI TUNASUBIRI CHAMA KINGINE KIINGIE MADARAKANI...

    ReplyDelete
  4. Mh daktari wa hospitali gani?

    ReplyDelete
  5. huyu sio mwanafunzi wa udaktari bado? kawa daktari lini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...