Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr. Asha Rose Migiro  akizungumzia umuhimu wa Taifa kusimamia haki ya mtoto ya kuishi kwa amani na furaha bila kufanyiwa Ukatili wa aina yoyote katika Kilele cha uzinduzi wa ripoti ya Utafiti na Mpango wa Kitaifa wa kushughulikia  “Ukatili kwa Watoto” na mpango wa Udhibiti wa Taifa.
 Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Umoja Mataifa Dr. Asha Rose Migiro,  wa pili kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba, wa kwanza kushoto Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Shukuru Kawambwa, wa Pili Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI (Elimu) Mh. Majaliwa Majaaliwa na wa Kwanza Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Mponda kwa pamoja wakikaribisha maandamano yaliyokuwa yakiingia katika viwanja vya Karimjee
 baadhi ya Mabalozi na watu mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi wa ripoti ya Utafiti na Mpango wa Kitaifa wa kushughulikia “Ukatili kwa Watoto” na mpango wa Udhibiti wa Taifa
Watoto wa Shule mbalimbali za msingi wakiwa kwenye maandamano  katika sherehe za uzinduzi wa ripoti ya Utafiti na Mpango wa Kitaifa wa kushughulikia “Ukatili kwa Watoto” na mpango wa Udhibiti wa Taifa
Baadhi ya Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Jeshi la Polisi wakishiriki maandamano ya kuzindua ripoti ya Utafiti na Mpango wa Kitaifa wa kushughulikia Ukatili kwa Watoto na Mpango wa udhibiti wa taifa. Uzinduzi uliofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa UN Bi. Asha Rose  Migiro katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Picha kwa hisani ya Mo Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mapambano ya ukatili kwa watoto yaanzie kwenye swala zima la fimbo mashuleni

    ReplyDelete
  2. Mbona maandamano naona ni watoto na kina mama tu. Je,kina baba wapi? au ndiyo wakatili? Mnasemaje wadau?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...