Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt imezindua chupa mpya ya aina yake yenye ujazo wa mililita 330 katika kiwanda chake cha Dar es Salaam 

Kinywaji hicho, ambacho hakina kilevi kwa sasa kinauzwa kwenye kopo zenye ujazo wa mililita 330 lakini kuanzia leo kitapatikana kwenye chupa mpya itakayouzwa Tsh 1000 kwa chupa na Tsh 20,000 kwa kasha kwa bei ya reja reja.

“Chupa hii mpya itaziba pengo katika soko na kukifanya kinywaji hiki kupatikana kwa urahisi,” alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Bw. David Minja huku akisisitiza kuwa kinwaji hicho bado kitapatikana kwenye kopo pia.

Alisema Grand Malt ilizinduliwa Aprili mwaka jana lakini kwa sasa ni kinywaji namba moja kisichokuwa na kilevi Tanzania. “Tunawashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kukikubali kinywaji hiki na kukifanya kiwe namba moja. Tunawahakikishia kuwa kitakuwepo sokoni muda wote ili kuendelea kuwaburudisha watanzania,” alisema Bw. Minja.

“Tunapozindua kinywaji hiki leo, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa kinywaji kitakachouzwa kwenye chupa ni sawa na kile ambacho kinauzwa kwenye kopo, ambacho kina vitamini na mchanganyiko wa maziwa ya aina yake,” alisema Bwana Minja.

Meneja wa Grand Malt Consolata Adam alisema, “Grand Malt ilizinduliwa Tanzania mwaka jana na leo tunapozindua chupa hii mpya, tunawashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono.”

Alisema kinywaji hicho kimetokea kuwa bora kwa sababu ya ladha yake nzuri inayoifanya inyweke kirahisi kwa kuwa ina vitamini, laktosi yenye ladha nzuri, inayoitofautisha na malt zingine sokoni.

“Kinywaji hiki kinawafaa wafanyakazi wenye shughuli nyingi lakini pia kinafaa kwa matumizi ya nyumbani, wafanyakazi wa usiku, wanafunzi, vikao vya kibiashara na sherehe nyinginezo,” alisema Bi Consolata.

Alisema TBL itaendelea kukitangaza na kusambaza kinwaji hiki na kuhakikisha kinawafikia watanzania wengi zaidi popote walipo.
 Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Bw. David Minja akionesha chupa mpya ya Grand Malt
 Meneja wa Grand Malt Consolata Adam 
 Juu na chini ni uzinduzi rasmi wa chupa mpya ya kinywaji cha jamii cha Grand Malt


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...