Gari hii iliyo katika maonesho ya NaneNane banda la TPDC inajieleza yenyewe kama maneno yalivyoandikwa. Picha na mdau  Samwel Mtuwa
SEHEMU YA INJINI , UNAWEZA KUBADILISHA GARI YAKO NA KUTUMIA GESI ASILI .... SOOOOOOOOOO CHEAP............

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hilo gari limekuwa katika maonyesho kwa miaka mingi sana..Sabasaba, nanenane nk. Cha kujiuliza hapa ni kwamba TPDC ni Engineering firm? Je wanabadilisha magari (ya watu binafsi, taasisi nk) kutoka petrol kuwa ya Diesel? Wameanza lini? Tokea wanaanza mpaka leo wamekwisha badilisha magari mangapi? Inagharimu kiasi gani kubadilisha gari? Mtu ukibadilisha gari yako, vituo vya kujazia gesi (Refill) vipo?

    Pale UDSM (Faculty of engineering miaka hiyo, kama 7-8 hivi iliyopita, nao walikuwa wanaonyesha pick-up iliyobadilishwa kutumia BIO-DIESEL. Wenye kujua kuhusu hilo, tujuzeni waliishia wapi? Waliendelea au nao waliishia kwenye maonyesho?

    ReplyDelete
  2. Tutajie bei. tupe na vituo tutakapojaza ikiniishia gesi hiyo singida?

    ReplyDelete
  3. TPDC kwa kushirikiana na wataalam pale DIT wanafanya kazi hiyo ya ubadilishaji, hivi sasa kuna zaidi ya magari 40 jijini Dar es Salaam wanatumia gesi asili katika magari yao. Ni rahisi sana, milioni moja inatosha kubadilisha mfumo huo.

    Kuhusu vituo(filling stations ipo pale Ubungo kuelekea chuo kikuu na mpango wa kujenga vingine waja, usichelewe wahi sasa. Mdau JM, Lumumba Street.

    ReplyDelete
  4. Acheni hayo nyie hapo juu; Aliyeweka picha hiyo ni mdau tu kama nyinyi. Namba ya simu, email vyote vipo peupe peee. Kama unahitaji huduma piga simu au andika barua pepe utapata maelezo kwa wahusika. Ninapata hasira sana kwa watu wasiosifu maendeleo bali wao ni kutaka kukosoa tu na ndio maana hamuendelei!

    ReplyDelete
  5. Lugha, lugha, jameni tafuteni ushauri wa BAKITA kabla ya kuweka tangazo rasmi kama hilo - sidhani kama wanatoza ada kubwa!

    GARI HII INA....vs GARI HILI LINA....

    ReplyDelete
  6. Kachasu (Pure alcohol) inayotengenezwa Singida inaweza kuendesha gari. Pombe hiyo inauwa watu wengi Singida na watu wana hiyo technologia siku nyingi. Kachasu inatengenezwa toka mtama na uwele. Ikisha anza kuuzwa kama petrol walevi watapungua na maisha ya watu yatakuwa saved.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...