Habari Ankal,

Usiku wa kuamkia Jumamosi ya tarehe 20/08/2011,kuna jamaa mwenye gari namba T913 AQX ,aligonga gari yangu katika junction ya Service Road ya Sam Nujoma na Barabara itokeayo  Meeda Club.Baada ya mimi kushuka kwenye gari,jamaa akakimbia.Amenisababishia hasara.Sasa kupitia Globu ya Jamii,naomba pindi apatapo ujumbe huu,anitafute kupitia kwenye namba  0755575828 ili anilipe gharama nilizotumia kutengeneza gari yangu.Atambue kuwa huu mji ni mdogo kukimbia si suluhu.

Ahsante;

Mdau wa Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kazi ya kuthibitisha mahakamani kuwa ndiye aliyekugonga akakimbia ngumu.Wengine wakigonga hukimbilia polisi sehemu ingine kufungua kesi ingine ya kugongwa na huyo aliyemgonga akamkimbia anasema kuna mtu kanigonga akakimbia . Kwa hiyo uwe na uhakika na ushahidi hasa pia aweza pia kufungulia kesi ya uzushi kuwa umemzulia si yeye ikala kwako na jijini kuna mawakili ubwabwa kibao kesi kama hii yaweza kusumbua na kukupotezea muda na ukadaiwa fidia kibao ya kudhalilisha mtu kwenye public hasa aliyekugonga akakimbia kama ni mtani wangu mhaya.

    ReplyDelete
  2. Kwani bima huna wewe?

    ReplyDelete
  3. Acha mkwara wewe! Uzembe wako barabarani unataka uletee shida wenzako,fanya ufanyalo bwana nani alikutuma unywe pombe nyingi.

    ReplyDelete
  4. Ajisalimishe kwako wewe Kova?

    ReplyDelete
  5. Namna pekee ya kumpata huyo mtu ni kwenda TRA watakupatia details za hiyo number ya gari then utaweza kujua ni nani.

    ReplyDelete
  6. ushauri wa bure: kisheria haupaswi kutengeneza gari yako. hiyo ni kazi ya bima ambaya umekatia gari yako. huwa watu wengi tunafikiri kulipana barabarani ndo suluhu lakini ukienda kampuni uliyokatia bima ni kazi yao kutengeneza gari lako mdau, hiyo ndo sababu lazima ulipe bima. hii pia ni sawa na ukigonga gari la mtu, anatakiwa aende kwenye kampuni yake ya bima ambayo itatengeneza gari lake na kuidai bima yako. jaribu kuwauliza.
    mdau

    ReplyDelete
  7. Sasa wewe mdau unataka jamaa akulipe gharama kwani yeye BIMA? Kama unaendesha gari basi lazima uwe na BIMA ndio maana mambo kama haya yakotokea basi wanatengeneza gari lako. Pole sana ila huna ushahidi wowote hata ukimwona kesho huyo jamaa huwezi fanya lolote kwani hakuna ushahidi.

    ReplyDelete
  8. Wadu lakini, hii tabia ya watu kugonga alafu wakakimbia inakuwaje. sasa kama sababu ndo hizo kwamba akishakimbia anaweza kukuzushia balaa wewe mwenyewe inakuwaje. kumbuka siku hizi anayegonga akakaa ni wachache sana. Mie siku moja niligongwa na Profesor mzima wa UDSM akakimbia mchana kweupe, nikamkibiza mpaka ofisini kwake. Nikachujua polisi chuo tukampeleka Polisi ubungo Terminal. Lakini wale trafik wakaniambia siku nyingine ukigongwa usimkibize aliyekugonga maana aweza kukuua (tabia za watu ni ngumu) wakanishauri chukua no. ya gari alafu ripoti polisi. Polisi watalifanyia kazi hilo. Wengi hilo linatushinda ukichukulia ukubwa wa jiji na wingi wa magari hicho inakuwa kama kitendawili. Swala langu hii tabia ya watu kugonga alafu wakakimbia ni nini. ukuchukulia kuwa magari yanakatiwa bima. Kuna haja ya polisi trafiki kutoa mafunzo kwa hilo. au wengine wanaendesha magari ya kuiba kwa shemeji.

    ReplyDelete
  9. ni mimii unasemajeee sasaaa ndio nlikugongaa si nyumaa ahahhaaa

    ReplyDelete
  10. Huyu jamaa anachekesha sana. Akutafute wewe ni nani? Wewe ni kituo cha polisi? Sheria hata chembe haujui jamani. Pole sana! Ipeleke hiyo namba polisi, pata RB halafu shughuli ianze

    ReplyDelete
  11. Kama tutaendelea kupoteza muda kujadili jambo dogo kama hili, basi Tanzania yangu itaendelea kukaa gizani. Tumejawa na mitizamo hasi (negative) na yaliyo mepesi. Utashangaa! ndiyo maana mheshimiwa Sitta aliwatolea uvivu vijana wa kitanzania kwa kuwa na mawazo ya kiFIESTA FIESTA.
    Ndugu yangu, nenda karipoti polisi, na Bima yako wagharamie kutengeneza gari lako. Huyo aliyekimbia, akikamatwa na polisi atashitakiwa kwa kukiuka sheria ya barabarani kwa kusababisha ajali, kisha kukimbia na asiripoti polisi.
    Salaam

    ReplyDelete
  12. imekula kwako aiseee....mjini hapa

    ReplyDelete
  13. Mlioshauri akaripoti Polisi ni sawa, lakini inategemea na hao Polisi wenyewe. Mimi ni mwanamke, niligongwa na mtu kwa makusudi, maana nilijitahidi kumkwepa kwa kila hali yeye akawa anakuja tu, baada ya kunigonga akakimbia. Nilitoka hadi nje ya barabara thank God sikukumbana na mtu wala mti. Kwa msaada wa raia wema walioshuhudia hilo tukio nikapewa namba ya gari na nikatoa ripoti Polisi. Lakini majibu niliyopewa ndiyo yaliniacha hoi ... eti hakuna mtu anayetaka kuharibu gari lake kwa makusudi maana akikugonga na yeye atakuwa anaharibu gari lake. Kwahiyo, kitendo cha mgongaji kukimbia eti ni busara ndio iliyotumika na si vinginevyo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...