Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen (pichani) ametangaza kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ugenini inayochezwa kwenye tarehe zinazotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA dates. Mechi itachezwa Agosti 10 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa; Shabani Dihile (JKT Ruvu) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Amir Maftah (Simba), Chacha Marwa (Yanga) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Juma Seif ‘Kijiko’ (Yanga), Jabir Aziz (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Soud Mohamed (Toto Africans) na Godfrey Taita (Yanga). Washambuliaji ni Salum Machaku (Simba), Julius Mrope (Yanga), Mrisho Ngassa (Azam), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), John Bocco (Azam) na Thomas Ulimwengu (U23).
Timu itaingia kambini kesho (Agosti 5 mwaka huu) jijini Dar es Salaam na itaanza mazoezi siku hiyo hiyo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Msafara wa timu hiyo wa jumla ya watu 30 utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.
Boniface Wambura 
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yanga Stars kama kawaida...hapo hakuna kipa hata mmoja anayemfikia kaseja. This is why taifa stars haitakaa iwe ya maana labda tuache majungu mpaka kwa kocha mzungu. TFF imeoza katika ufisadi wa kisoka. Kamwe hatutapiga hatua kama makocha wataachwa bila kupewa misingi ya soka na kuacha usimba na yanga!

    ReplyDelete
  2. Nampongeza kocha kwa kuchagua kikosi kizuri,naamini kitafiti kulingana na mfumo wake, karibu sana mtaalamu Kijiko,natumai idara ya ufungaji itamalizwa na Ulimwengu, cheers!

    ReplyDelete
  3. Wambura tangu umekuwa Ofisa wa Habari wa TFF unapoteza uwezo wako wako uandishi wa habari tofauti na ulivyokuwa kwenye news papers.Tunaelewa uko "Bize".

    Sasa hii habari hujasema timu inaingia kambini kucheza na nani(unachukulia kila mtu anafahamu)"....msafara wa timu...utaongozwa..."(Msafara wa kuelekea wapi..na lini.?.).

    David V

    ReplyDelete
  4. Ina maana Mrisho Ngassa hakufanikiwa kusaini Seattle Sounders?

    ReplyDelete
  5. Kaseja limebaki jina tuu lakini hakuna kitu pale kwa sasa. Ngassa amefanikliwa Seattle Sounders lakini kwa vile msimu wa Major League Soccer unaelekea ukingoni yeye atawajoin mwanzoni wa kambi msimu ujao March nafikiri.

    ReplyDelete
  6. hivi ina maana tegete hafai kucheza taifa star tena au,,i mean how can ths john boko bette than him,,first it was maximo na kaseja and now poulsen na tegete,,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...