JB BELMONT HOTEL (ZAMANI PARADISE CITY HOTEL) ILIYOPO MAENEO YA POSTA MPYA IMEJITOSA KUDHAMINI PAMBANO LA UBINGWA WA MABARA WA UBO BANTAM WEIGHT KATI YA MBWANA MATUMLA VS FRANCIS MIYEYUSHO LITAKALOFANYIKA TAREHE 30 OCTOBER DIAMOND JUBILEE HALL.
AKIZUNGUMZIA HILO MKURUGENZI WA KAMPUNI YA DARWORLD LINKS LTD AMBAO NI WAANDAAJI WA PAMBANO HILO MODDY BAWAZIR (PICHANI JUU AKIWA NA MABONDIA MBWANA (SHOTO) NA MIYEYUSHO) ALISEMA "KWA KWELI NIMEFURAHISHWA SANA NA UDHAMINI HUU NA HII INALETA MOYO WA KUANDAA PAMBANO LILILO BORA KABISA".
BAWAZIR ALIWATAKA WADHAMINI ZAIDI KUJITOKEZA KUDHAMINI MPAMBANO HUU WA KIMATAIFA AMBAPO PIA KUTAKUWA NA MAPAMBANO YA UTANGULIZI 7 IKIWEMO NGUMI ZA KINA DADA KATI YA AGNES TOKA MALAWI NA FURAHA TOKA TANZANIA.
"NAOMBA MAKAMPUNI NA TAASISI MBALIMBALI KAMA VODACOM,TIGO,AIRTEL,ZANTEL, SERENGETI BREWERIES,TBL,KONYAGI,PEPSI, COLA NA MENGINEYO YAJITOKEZE KUUNGANA NA JB BELMONT HOTEL,MICHUZI BLOG,SHAFFIHDAUDA BLOG NA GAZETI LA JAMBO LEO KUDHAMINI PAMBANO HILI ILI KUUINUA ZAIDI MCHEZO HUU WA NGUMI ULIOKUSANYA WAPENZI WENGI SIKU ZA KARIBUNI" ALISEMA BAWAZIR.
KWA MAWASILIANO NA KAMPUNI YA DARWORLD LINKS LTD SIMU NO.0715 666686.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...