Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete yuko mjini Windhoek, Namibia kwa ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo. Rais Kikwete ameondoka nchini asubuhi ya leo, Alhamisi, Agosti 11, 2011, na atarejea baadaye leo.
Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yuko Namibia kuhudhuria mkutano wa wakuu wa vyama vya siasa vilivyopigania uhuru miongoni mwa nchi za kusini mwa Afrika.
Katika mkutano huo wa leo, chama tawala cha Nambia cha SWAPO kinavikaribisha vyama vya CCM, ANC cha Afrika Kusini, Frelimo cha Mozambique, MPLA cha Angola na ZANU-PF cha Zimbabwe.
Mkutano huo wa siku moja unalenga kuangalia historia ya uhusiano baina ya vyama hivyo, na jinsi historia hiyo inavyoweza kutumika kuongeza ushirikiano baina ya vyama hivyo katika mazingira ya sasa.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo muhimu miongoni mwa vyama ambavyo viliongoza mapambano ya kisiasa, na kwenye nchi nyingi pia mapambano ya kijeshi na vita ya ukombozi, ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Wilsom Mukama.

CCM: Jamani wazima wadau, dah Frelimo umenenepa kichizi, unakula nini? ANC namjua kwa kutia msosi, anakukaribisha nini manake majirani nyie.
ReplyDeleteFrelimo: Ah wapi, njaa tu bana. Vipi huko home kwako kwema? Mbona umekuwa hivyo, unafanya dayati nini?
CCM: Mambo magumu bana tena yanabadilika kila kukicha.
MPLA: Tatizo nduguzanguni hamtaki mabadiliko. Sometimes lazima usakrifais vitu flani ili uwe katika hali murua...
ANC: Na hilo ndio jambo la msingi, azawaiz mtalazimishwa kubadilika... Si mnaona ZANU PF alivyofulia?
ZANU PF: Oya achana na mimi bana, acha kufatilia mambo yangu kabisa wewe...
ANC: Oya mwana, just joking bana, mshkaji mkali kama hujala mchana?
ZANU PF: SIyo hivyo bana, we unaleta utani kwenye masuala muhimu. Mi mwenzio nimepitia kipindi kigumu sana mtu wangu. Nimebana kichizi mpaka ikawa noma ikabidi niachie tu, ila maisha bado hayajakaa sawa kuna dogo nuksi sana homu, tumemuadopti kutoka mtaani. SWAPO vipi mwana mbona kimya sana, leta walau laga tubamize tupunguze machungu basi...
SWAPO: Mi nimeshaacha kunywa wadau. Nakunywa rozela na juisi ya ubuyu tu.
CCM: Ah kudadadeki nyie tatizo bado wachanga. Mi wote nimewafuta pupu nyie, tangu mkiwa wadogo mnajikojolea hovyo, kwa hiyo hakuna anayejua michakato inavyokwenda kama mimi. Mi mkongwe kwenye sanaa bana, tangu enzi za traki moja, sio nyie kompyuta na mavokoda tu...
ANC: CC acha umachinoo mwana, mambo yamebadilika siku hizi.
ZANU PF: Huyu mchizi namuheshimu lakini naona anazidi ubishi. Mtu wangu yatakukuta yaliyomkuta KANU, si umeona mchizi wako hata hapa hajatokezea. Nasikia kafulia kichizi sikuizi.
CCM: Mchizi alichezea kazi badala ya mshahara, LMFAO! Mi nlimwambia yule...
SWAPO: Oya usijione uko juu sana mwana, itakula kwako.
CCM: Nyie bwana wadogo naona mmeshajiona watu wazima coz nowadays mnavuta sigara na kutafuta mademu, naona mnanizingua tu hapa...
ANC: Ahcha hasira mwanangu, haya maisha lazima tulindane.
Frelimo: Ilo ndo la msingi wadau, sasa inakuwaje? Si tupige msosi kwanza?
ZANU PF: Afu kudadadeki kama umenisoma, sijala homu wiki nzima hapa mpaka utumbo umekuwa kama stroo ya juisi za Azamu, unashangaa nini CCM? Zinakuja homu kibao ila kudadadeki kijoti wanauza dola laki nne za Zim...
Wote: Ahaaaaa, haaaaahaa...
ZANU PF: Oya acheni mambo ya kishamba, sasa mnacheka nini? Si maisha tu? We CCM mwenye we usipoangalia mwaka huu kudadadeki utanunua wese lita moja elfu tano zenu, thats if wese lenyewe lipo. Nasikia mmefulia, LMFAO!
SWAPO: Jama tukagonge menu kwanza halafu tuje tupige stori. Sasa we Frelimo unatangulia unajua jikoni wapi?
Frelimo: Mi nafata harufu mwana, niko fasta!