Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Mecki Sadik  akiagana na wazee na madiwani wa jiji la Dar es salaam leo jioni baada ya futari aliyowaandalia katika viwanja vya Karimjee hall 
 Mh. Mecky Sadick akiagana na wageni wake
 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar na wageni wake
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Mecky Sadik (kushoto) akiwa na Shehe Mkuu wa Mkoa huo Sheikh Alhad Mussa Salum pamoja na Kamanda kanda maalumu ya Kipolisi ya Dar Afande Suleiman Kova (kulia)
Mzee Tamba (kati) akisalimiana na mwanaharakati na mmoja wa wazee wa Dar es salaam Binti Kamba baada ya hafla hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Jamani naomba kuuliza Kaimu mkuu ni cheo ganio hicho mbona sijawahi kukisikia!au ni Kaimu Meya au kaimu wa Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar au ni Kaimu cheo kipya!MImi ninavyoelewa Kaimu ni kama Makam sasa ni makam wa Rais au wa Mufti!Nielewesheni,,Hicho cheo sikukiacha TZ,,,Ahlam UK

    ReplyDelete
  2. viongozi wakumbukeni na wasiokuwa na uwezo kwani kila siku mnafuturisha watu wenye uwezo wao lakini watu wengi na mayatima hawana uhakika na futari wakipata wanashukuru kikweli

    ReplyDelete
  3. Mchangiaji wa kwanza Kukaimu ni kushikilia madaraka kwa niaba ya mtu umakamu ni kuwa chini ya mtu fulani na akiondoka automatically unakaimu madaraka hayo. Sasa kwenye vyeo vya ukuu wa mikoa hatuna makamu mkuu wa mkoa so huyu Sadick Mecky ni mkuu wa mkoa wa Lindi na kaimu mkuu wa mkoa wa Dar shavu tu

    ReplyDelete
  4. Naona kiongozi anaweza kufuturisha wengine kama wataongelea mambo ya uongozi na maendeleo ya taifa baada ya hiyo futari,ili nao hao waliofuturishwa(madiwani) waende kuwasaidia wananchi katika kata na vitongoji vyao wasiokuwa na uwezo wa kununua futari na pia kuwasaidia wanacnhi wao kujikwamua na hayo maisha duni yanayowazunguka.
    Blaablaa/ siasa ndio inayoongoza sasa kwa vingozi wa dini na hata viongozi wa serikali.
    Tunataka viongozi wa kweli na sio wale mnaouza maliasili za taifa kwa manufaa yenu binafsi.

    ReplyDelete
  5. tafuteni futari zenu na nyinyi. Mnapofanya jubilee mbona hatusemi.

    ReplyDelete
  6. Asalaam,
    tunaambiwa ni vizuri tule tukiwa na njaa ni kauli ya Mtume wetu Muhammad (SAW)hii ina tafsiri kubwa sana inalenga hata wenye kufuturisha hayo mapochopocho ebu sogeeni pembezoni huko nako mkafuturishe nao wapate ladha ya hizo juice na hayo mapochopocho. Kuna watu wanafuturu mwezi mzima kwa shida. jaribuni kuangalia na wengine acheni ubinafsi wenu fuateni matendo ya Kiongozi wetu Muhammad (SAW)
    Wabillah tawfiq

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...