Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo akitoa taarifa kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Kitundu Jairo  kufuatia tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wabunge tarehe 18 julai 2011 mjini Dodoma. kulia kwake ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Ludovick Utoh na aliyesiamama na wanahabari mwenye koti jeusi ni Mkurugenzi wa Habari Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu

Na Francis DandeKwa mujibu wa katika taarifa yake yenye kurasa nne Katibu Mkuu Kiongozi amesema kutokana na mamlaka aliyonayo kwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma, tarehe 21a bjulai, 2011, kwa kuzingatia uzito wa tuhuma alianzisha uchunguzi wa awali na kumpa likizo ya malipo Bwana Jairo ili kupisha uchunguzi.

Uchunguzi huo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Lodovick Utoah  umeonyesha kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni julai 18 hazikuwa kuthibitishwa, kutokana na na matokeo hayo ya uchunguzi wa awali, “mimi kama mamlaka ya nidhamu ya katibu mkuu Nishati na Madini, Bw David Jairo, sitaweza kuendelea na hatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma (notice) na hati ya mashitaka kwa sababu bw. Jairo hajapatikana na kosa la kinidhamu (disciplinary offence) kwa mujibu wa taarifa maalum. 

 Amesema kufuatia matokeo hayo ya taarifa hii ya awali na kwa mamlaka niliyonayo kwa mujibu wa sheria namba 8 ya utumishi wa Umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003, NINAAMURU BWANA DAVID KITUNDU JAIRO AREJEE KAZINI KUANZIA SIKU YA JUMATANO TAREHE 24 AGOSTI  2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Well, Ndugu Watanzania wenzetu naona tumegundua ni kwa jinsi gani serikali ya awamu ya nne ilivyomakini kutudhihirishia umahiri wake juu ya maamuzi.

    NAmpongeza katibu kiongozi kwa hatua hii
    nampongeza Waziri mkuu kwa umahiri alioufanya kule bungeni
    Kwa mtindo huu tutafika tuu.

    ReplyDelete
  2. tatizo la watanzania huwa tunahukumu kwa tuhuma ...ndugu zangu tuhuma sio hatia.... waosha vinywa mmeumbuka hahahahaha....

    ReplyDelete
  3. Hata mimi naipongeza sirikali yetu kwa kweli, imefanya uamuzi ambao wananchi wengi waliutarajia. Hongera sana Mheshimiwa Jiro, umeula. Nataka niwakumbushe tu Wananchi wenzangu kuwa kile kilichoonekana bungeni mpaka uamuzi wa kumsimamisha kazi kwa muda, (na hata waziri mkuu na spika kuhamaki na kumsubiri mheshimiwa rais kutua SA ili spika wamueleze) si ushahidi tosha wa kumfukuza kazi na kumchukulia hatua za kumuadhibu kisheria. Mlio m-accuse mnahitaji ushahidi zaidi ya huo ili achukuliwe hatua za nidhamu.Kwa mtindo huu tutaendelea tu, na tutafika. Tujiandae na tuhamasishe wananchi kukichagua tena chama tawala uchaguzi ujao.

    ReplyDelete
  4. Yangu macho

    ReplyDelete
  5. Hili nalo tunamwachia Mungu. Yes si nyie mna akili sana halafu sisi ni zero, upstair kweupeee. Haya bana.

    ReplyDelete
  6. ipo siku itafika

    ReplyDelete
  7. Anony wa kwanza hapo juu nakuunga mkono,nimekukubali kwa FASIHI SIMULIZI.Na mimi Nampongeza Katibu kiongozi,Waziri mkuu, rais na CCM kwa ujumla.

    David V

    ReplyDelete
  8. Tunakupongeza na wewe uliyetoa maoni hapa juu, tutafika tu usiwe na wasiwasi. Fanya kazi kwa bidii. Huwezi kutoa tuhuma bungeni kama huna uthibitisho wa kutosha. Yalikuwa ni majungu tu.

    ReplyDelete
  9. Asante Beatrice Shelukindo kwa kuthubutu. Hata kama hana hatia, ila ujumbe kwa viongozi wengine umefika.

    ReplyDelete
  10. Kuhamisha fedha kutoka akaunti moja ya serikali kwenda akaunti nyingine ya serikali inakuwaje rushwa? utasemaje umefanya uchunguzi na kugundua kuwa wizara ina taasisi zaidi ya ishirini? Beatrice Shelukindo kwa hili alikosea na inapaswa amwombe Jairo msamaha kwa kuwa amemfedhehesha sana mbele ya jamii ya watanzania. Watanzania jamani majungu si njia ya kuleta maendeleo nchini. Haiwezekani mtu akaadhibiwa kwa chuki binafsi. Its not right and should never be allowed to happen. God Bless Tanzania.

    ReplyDelete
  11. TATIZO LETU WA TANZANIA TUKISHA SIKIA HABARI KTK VYOMBO VYA HABARI TUNAJENGA HISIA ZA KUAMINI MOJA KWA MOJA NA NDIO MAANA NCHI NYINGI DUNIANI ZINA VIBANA VYOMBO VYA HABARI KUEPUKA MATATIZO KAMA HAYO NA MENGINE LAKINI HAPO BONGO HUO UHURU WA HABARI JAPO NI KWA NIA NJEMA LAKINI UNAIPELEKA NCHI ALI JOJO UMEINGIZA VITINA NA CHUKI ZISIZO ELEZEKA KILA TUFUNGUAPO MITANDAO SISI WENGI WETU TULIO MBALI TUNAONA KABISA HALI HIYO YA MAJUNGU KUCHUKIANA NA HASA HAYO MAGAZETI YA KAMPUNI BINAFSI NA BAADHI YA BLOG MBALI MBALI TUKUMBUKE KUWA NCHI NYINGI DUNANI ZINAKUMBWA NA MACHAFUKO CHANZO NI HIVYO VYOMBO VYA HABARI VINAKUWA KTK KUWALAZIMISHA WANANCHI KUAMINI YASIYO YA KWERI HAYA WABONGO KAZI KWETU - MDAU UGHAIBUNI

    ReplyDelete
  12. Lakini msemaji hapo juu hauko sawa. Taarifa ya Jairo haikuwa jungu hata kidogo. jambo limezungumzwa bungeni na Mheshimiwa Waziri Mkuu akalitolea tamko la hasira kabisa. Sasa Katibu Mkuu anaposema hakukuwa na kosa lolote dhidi ya Jairo inakanganya kigodo. Unashindwa kuelewa hii inakaaje sasa. Na kama wenye uelewa wanachanganyikiwa, je wenye uelewa mdogo? Hebu serikali tujiangalie upya ili kujua wapi kuna tatizo. Mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa. Ukiangalia maamuzi mengine yangezuia watu kusema kama yangetolewa kwa uangalifu na kuzingatia muonekano wa uadilifu. lakini ni bahati mbaya haiwi hivyo.

    ReplyDelete
  13. Bw. Michuzi tusaidie kupata hiyo video ya Luhanjo. Ahsante

    ReplyDelete
  14. Bravo Luhanjo kwa maamuzi kwa kutoa maamuzi magumu. Hata ile kesi ya UDA iwekeni kapuni yale ni majungu tu hakuna ushaidi wa kutosha. Hata vile vibanda vya kufugia simba vilivyoko soko la machinga complex vilivyogharimu tuvijisent 1.2 Billioni yale ni majungu tu.

    ReplyDelete
  15. Mimi sijawaelewa bado. Tuhuma zilikuwa kuchangisha fedha kwenye idara mbalimbali ili "bajeti ipite". Barua iliwasilishwa sote tukaiona. Swali langu ni kwamba bajeti inapitishwa kwa fedha au na wabunge pale bungeni?

    Pesa zinazochangishwa (milioni 50 kila idara) zinatumikaje kupitisha bajeti? Kama umeandaa bajeti yako vizuri pesa za kuipitisha ni za nini tena? Kwa mtu yeyote mwenye akili haya ni mazingira ya rushwa.

    Lakini sishangai. Sijui ni lini mafisadi Tanzania watapatikana.

    ReplyDelete
  16. Michuzi, tunataka utuambie who are you rooting for, naona umeruhusu maoni yanaoyo mfagilia Jairo, na yetu yanayo ikandia serikali ukayaminya

    ReplyDelete
  17. jee kwa tukio hili, tunalitathmini hilo Bunge letu? Kwa maoni yangu wabunge hawana uwezo wa kuchunguza na wanakurupuka kwenye maamuzi yao. Hii ni kuitia hasara kwa kwa maoni yangu Katibu aende vyombo vya sheria akadai kusafishwa jina lake na kurudishiwa haki zake kipindi cha kukaa bure kwake, Jee hasara hiyo iwapo atalipwa nani atagharamia wabunge au Serikali??????????

    ReplyDelete
  18. kila idara imeombwa kuchangia milioni 50! Na kwa taarifa sahihi inasema idara 8 zilichangia, that means tayari akaunti ya TGS ilikuwa na Tsh 400 milioni. Swali la kujiuliza, bajeti inasomwa bungeni ka muda wa siku 2 ama 3, sasa ni matumizi gani yanayoweza kutumia milioni 400 ili "kupitisha" bajeti?

    Wizara nzima pamoja na watendaji wake wote wakisema waende Dodoma kwa siku 3 hawawezi kumaliza hiyo fedha kwa viwango halisi vya serikali kwa posho na hela ya kujikimu!

    Sasa hela yote hiyo kwa kila idara kutoa Tsh 50 milioni ilikuwa ya nini?

    ReplyDelete
  19. hehehe kweli naona ajira zimeongezeka. Kuna watu wameajiriwa kutoa koment za kusafisha.

    We uliepo ughaibuni, hujui kinachotupata sisi. Hujui shida ya maji, wala umeme na unafanya kazi kwa bidiii sana kuweza kuishi huko. Watanzania wengi wamejiajiri sasa, ila nishati ya umeme inaua makampuni. Huna unachoweza kutetea hapa tanzania. Endelea kupumzika tu. Tukiamua kuuana is for our own good.

    Big up magazeti.hehehe kweli naona ajira zimeongezeka. Kuna watu wameajiriwa kutoa koment za kusafisha.

    We uliepo ughaibuni, hujui kinachotupata sisi. Hujui shida ya maji, wala umeme na unafanya kazi kwa bidiii sana kuweza kuishi huko. Watanzania wengi wamejiajiri sasa, ila nishati ya umeme inaua makampuni. Huna unachoweza kutetea hapa tanzania. Endelea kupumzika tu. Tukiamua kuuana is for our own good.

    Big up magazeti.

    ReplyDelete
  20. kama ni kweli hana hatia tunaomba shelukindo ashitakiwe, pinda na spika wamuombe msamaha, vinginevyo ni ccm ccm ahhh! chama cha mapinduzi ccm namba wani!!!

    ReplyDelete
  21. aaaah, haya i expected this anyway. hawakudhibitisha vipi wakati barua yenye sahihi yake ipo?
    ishu ni kuwa aliomba hizo mil 50 za nini?

    ReplyDelete
  22. haingii akilini, 500mil zilipangwa kwenye bajeti ipi? na kama ni kawaida hizo posho nyingine za nini? rushwa imeshahalalishwa kuwa sehemu ya maisha. takrima walihalilisha ndio iwe ajabu kwa michango

    ReplyDelete
  23. kaka michu!.........inachekesha sana kuona serikali ipo kwenye dhamana ya watu flan!! sasa hii ni nini!? maana hata hiyo saini ya huyo jairo ni feki kwenye hiyo barua na kama feki mie nataka aikane tu then tuendelee kusikilza upuuzi wa hao wanajiodai wana dhamaana ya wananchi! huku ni kulindana tu! na si ajabu ya haya, maana yapo makubwa mno mpaka leo hadithi tu tunapewa, sembuse iwe huyo jairo kutaka vimilon 50 kila idara,kuna wangapi wamekula mpaka leo wapo happy life na family zao,wapi lowasa,karamagi,sumaye na hela zetu za AIDS zilizopotea kwake,wapi mramba,msabaha,na wengineo tunawajua maana sio siri suala la uadilifu ktk tanzania siku hizi,na hao ziro brain hapo juu wanaochangia upuuzi na ndio wanaotuharibia nchi kwa njaa zao za shiling.mbili. angalia leo tz maji issue,umeme issue,chakula je!? na mafuta, then wanatuambia nini? hata kusikiliza inakera, wizi mtupu.

    kaka issa sie tupo huku kama watumwa kwa sababu ya hao jamaa hakika, maana hakuna hata huruma kidogo.
    mie naona hata mh.rais anapata wakati mgumu sana kwa watendaji wabov, maana kila atayemuweka ni mtihani tu!
    mdau jp.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...