Ankal,
Polisi hapa Sauzi wapo na kazi nzito ya kulinda raia na mali zao, na zaidi ya hapo kujilinda wenyewe kwani wanashambuliwa na kuuawa sana. Embu fikiria kwa mwaka huu tuu, tayari polisi 50 wamekwisha fariki dunia, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, tena wengi wao wanauawa kwa SHABA !- Bunduki.

Hivyo serikali imeagiza ni AMRI kwa polisi kuvaa vizuia risasi – Bullet -Proof vests kwa askari wote wanapokuwa wapo kikazi zaidi, hata kama wapo ofisini wakiandika taarifa mbalimbali. Gazeti la Beeld linaeleza kuwa makamanda wa ngazi zote watashughulikiwa endapo itapatikana kuwa askari walio chini yao hawafuati maagizo hayo.

Hii inakumbusha jinsi ambavyo hali ya uhalifu bado ipo juu hapa SAUZI. Si ajabu hapa kukuta askari wengi wana ‘chamoto ‘ wakati wowote wakitembea. Mapambano ya askari na majambazi mitaani hasa Joberg na Pretoria si mambo ya kushangaza sana hapa.

Pichani ni mfano wa bullet proof vest wanazotakiwa kuvaa askari muda wote.
Labda ndio maana bongo inasemekana ni nchi ya amani sana…eti eehh, mambo haya hayapo !

Mdau, John
Sauzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inafika hatua binadamu anakua haoni tafauti ya kuishi na kufa. Binadamu kama huyo anaweza kufanya jambo lolote. Ndio maisha ya watu wengi wa ughaibuni na raha zote walizonazo. Mtu kuuwa hauni taabu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...