Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini LHRC kimetoa wito kwa Serikali kusitisha kwanza uchimbaji wa madini aina ya Uranium katika wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma hadi itakapothibitisha kuwa na uwezo wa kuzuia madhara yanayotokana na athari zake kiafya kwa binadamu na kimazingira.
Akisoma tamko la kituo hicho Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho ya Sheria Bw HAROLD SUNGURA amesema licha ya serikali kuanza mchakato wa kuchimba madini hayo ndani ya Mto Mkuju na maeneo mengine ya Bahi na Manyoni hadi sasa haijawashirikisha wananchi ikiwemo kuwaelimisha kuhusu athari zake.
Kasema utafiti uliofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini LHRC katika migodi mbalimbali nchini ikiwemo Nzega, Geita na North Mara unaonesha kuwa uchimbaji wa madini umeleta maafa zaidi kwa Watanzania wengi kuliko faida.
Serikali imetakiwa kutazama kwa umakini uwekezaji wa mataifa makubwa hasa yaliyokuwa na mgogoro wa vita baridi katika sekta ya uchimbaji madini aina ya Uranium nchini zoezi linalotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Bw. Sungura amesema hatua hiyo italiepusha taifa kutotumiwa vibaya na mataifa hayo kama uwanja wa vita na mapatano kupitia madini hayo na mazingira yatokanayo na shughuli hiyo.
Madini ya Uranium yametajwa kusababisha madhara mbalimbali kwa afya ya binadamu kama vile saratani ya figo, ubongo, ini, damu, magonjwa ya moyo, kupunguza kinga mwilini, vifo vya watoto, kuharibika kwa mimba na kupunguza nguvu za kiume.
Chanzo: http://www.theeastafrica.blogspot.com/


I agree, 100%
ReplyDeleteNakumbuka maneno ya Adam malima N.Waziri wa nishati hivi juzi bungeni..,alisema kuna hivi vitaasisi vinawakwaza ktk kuleta maendeleo ya nishati mbadala ya makaa ya mawe kwa ajili ya kuzalisha umeme.sasa Tusipochimba nishati hizo alizotupa mungu tuzitumie kupata umeme na tuache kutegemea mvua na matumizi mengine ya nishati hiyo,tutakua hatufanyi sawa unapokataza jambo ni lazima utoe mbadala wake,tukubaliane tu kila inovation ina athari zake, kwa mfano technology ya computer zinapokwisha kazi yake zimechakaa namna ya ku dispose nayo ni tatizo lakini huwezi kusema tusitumie computer kwa dunia ya leo. Na ndiko tunakoelekea pia ktk matumizi ya uranium kuna wakati tutalazimika kutumia tu...,nchi kama japan bila urunium maviwanda yote yasingefanya kazi.kwa hiyo ni lazima tukubali mambo mengine ili tuendelee. Hizi NGO's mara nyingi zinatukwaza kupata maendeleo.
ReplyDeleteMwenye njaa iliyochanganyikana na ujinga hashauriki. Na siku zote chake ndicho kinamumaliza, badala ya kumuokowa. Yetu macho na masikio.
ReplyDeleteserikali iwe na uhakika kwamba wachimba madini ya uranium wana tumia taadhari za kutosha ili kujikinga na "rediation" za madini hayo, kwani madhara yake hayatasabisha asara kwa wakazi wa kiji hicho bali taifa kwani madhara hurithisha vizazi na vizazi.
ReplyDeleteHongera sana Bw. Sungura na Kituo chenu cha HAKI ZA BINADAMU.
ReplyDeletekwa kweli serikali yetu imeweka maisha yetu rehani. Ikiwa miji yetu ina mitaro iliyojaa vinyesi na mifuko ya rambo iliyogeuzwa kuwa mobile toilets, na bado tumeshindwa kuifanyia usafi - je vifusi vilivyosheheni mionzi vitakavyotoka kwenye machimbo ya madini hayo tutavitupa wapi? Zambi kwa sasa ina vifusi vyenye jumla ya tani milioni 4.5 hawajui pa kupeleka, chonde chonde jamani.
Isitoshe - uchimbaji huo utafanywa kwa miaka 12 kisha wawekezaji waondoke baada ya madini hayo kwisha - sisi tutabaki na vifusi na jamaa watakuwa wameshachukua chenchi yao. tutabaki na umasikini wetu PLUS magonjwa yasiyoisha kutokana na uchafuzi huo wa mazingira uliopindukia. Ikiwa dhahabu imesababisha maafa kule north Mara, hii urenium itatuponyesha kweli hasa kwa viongozi wa sampuli hii tunaowajua ambao wamezidi unyenyekevu kwa wawekezaji na wafanya biashara? Ikiwa kisingizio ni umeme - hizo ni porojo; kwani gesi ya songosongo na mnazi inatusaidiaje? mbona bado mgawo wa umeme unazidi? Watanzania tuamke.
Huyo kwenye picha sio HAROLD SUNGUSIA
ReplyDeleteHongereni Kituo cha Sheria;
ReplyDeleteendeleeni kuwabana hao jamaa mpaka kieleweke.
Lobby group hizi... ata zao la tumbaku walitaka liachwe.... hivi wanajua tumbaku integemewa na familia ngapi hapa Tanzania... tumeshatoka kwenye ujamaa tuache hizi fikra za kwamba kila ambacho atulkielewi ni kibaya zaidi ya vile tunavyo viona.... tafuteni kugombania haki za watu wenye shida sasa hivi na msiwe wafuasi wa wanasiasa....
ReplyDelete