![]() |
MAMA YETU FATMA NINDI |
Mama, hatuamini kama ni mwaka mmoja umepita sasa toka ulipotuacha tarehe 12-08-2010.Siku ya leo inaleta kumbukumbu zisizoelezeka na zisizostahimilika.Ni vigumu sana kukubali kuwa haupo nasi ila hatunabudi kumshukuru Mungu kwa mapenzi yake.
Sisi tulikupenda sana lakini Mungu alikupenda zaidi.
Umetuacha mapema tukiwa bado tunakuhitaji kwani wewe ulikuwa ndiyo nguzo na muhimili wa maisha yetu.
Unakumbukwa sana na mama yako, mama mkwe wako,watoto wako Anna, Patrick, James na Charles, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na majirani zako.
Mama ulikuwa na upendo na ucheshi usiokuwa na kifani.
Umetangulia mama na tutakukumbuka daima.
TUNAMWOMBA MWENYEZI MUNGU AILAZE
ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI,
AMINA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...