Basi la Abiria likilazimika kuli-overtake lori lililokuwa limeegeswa barabarani bila ya kuwa na alama yoyote ya kiusalama,jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine huweza kusababisha ajali ya kizembe na kupelekea watu wengi kupoteza maisha.
Pamoja na kwamba eneo hili linamaandishi ya kumtaka dereva kuendesha gari pole pole lakini kwa dereva wa basi hili ilikuwa ni kama ndio kaambiwa aongeze spidi.
Taswira ya kwanza ajali nyingi utokea kwa mtindo huo bila kuweka alama yoyote ile ni matatizo. Taswira ya pili Dereva wa basi hana kosa kwa sababu hiyo SLOW DOWN ni ya upande mwingine ukiangalia mstari ni dashed line kwa hiyo hakatazwi kuovertake hapo sema yeye inabidi aangalie upande wa pili kwanza lakini hajawekewa solid line kumkataza kuovertake huo ndio ufahamu wangu mdogo nilionao.
ReplyDelete"SLOW DOWN" maana yake nini?
ReplyDeleteHalafu usituzingue wewe, anayekwenda alama haimwambii slow down isipokuwa anayekuja upande wa kulia. Hata hivyo alama kuwa waweza kuovertake zinaruhusu ilimradi unaangalia usalama, halafu panaonekana hapo ni pori pengine ni kivuko kwa wanyama pori au mifugo. Ila yule aliyeegesha mlori wake bila alama kweli huyo ndo hatari zaidi. Au madereva mnasemaje?
ReplyDeleteAnkal, picha kama hizi ni ushahidi muhimu tu wa uvunjaji kanuni za usalama barabarani. Kama Jeshi la polisi na serikali kwa ujumla wake wako serious na wana uchungu juu ya maisha ya wengi wanaopotea na kuumia bila sababu barabarani, mimi nitakuwa mmojawapo kupiga picha na kuzipeleka zikachukuliwe hatua na wahusika, hiyo itaweza kusaidia kwa kiasi baada ya watu kujua linaloweza kuwasibu.Tatizo tu sijui ndio chanzo kingine cha mapato kitakuwa kwa wahemiwa maafande wetu!! Mungu atusaidie
ReplyDeletesingle yellow line ni no parking au no kusubiri abiria labda kuwe na ishara nyengine lakini unaruhusiwa kusimama kupakia na kupakua abiria hasa hapo hakuna time ya kuonesha, lorry hana kosa ila ni kosa kama kakaa zaidi ya dk 5 bila kupakia au kupakua
ReplyDeleteLong white line kisha short black line au blank you can overtake hakuna restriction,ila kama ingelikua white line ni short kisha black line au gap ni kubwa ni overtake at your own risk.
sasa mifugo pia kuna alama zake na hiyo ni motorway hakuna mwenye kosa hapo labda lorry kama amepark na sio kwa sababu nilotaja
(mdau wa usalama dunia nzima)
Naungana na wadau hapo juu kuwa dereva wa hilo basi lililo picha ya chini hana makosa kwa kuwa wanaoshauriwa kupunguza mwendo ni wale wanaokwenda upande wa pili. Pia naona barabara mbele ni nyeupe inayomuwezesha kuli-overtake hilo lori ambalo inaelekea lipo katika mwende mdogo. Pia nimetembelea blog ya othmanmichuzi.blogspot.com/ naona imetulia. Cha kujiuliza hapa ni hivi kuna blog ngapi zenye neno 'michuzi'? Inaelekea 'Michuzi' sasa ni 'brand'.
ReplyDeleteHapo wakulaumiwa ni askari wa usalama Barbarani ,mi nadhani waziri wa mambo ya ndani akishindwa basi Rais atowe amri ya kuwa na Polisi wa usalama barbarani katika kila Basi linalosafiri kwenda mkoani ikiwa kama ni moja ya wajibu wao kila siku,wataukuwa wanabadilisha basi na kurudi na yale yanayorudi pale yanapokutana iwe morogoro,Mombo n.k
ReplyDeleteAu serikali inunuwe camera za barbarani na kuweka kituo katika kila mkowa.
Au Abiria wawe wanachukuwa picha za namba za mabasi yanayoendesha bila mpangilio na kuwasilisha wizara ya mambo ya ndani kwa Waziri mwenyewe na Dereva achukuliwe hatuwa za haraka.
Tunalalamikia serikali bure wakati imejenga Barabara na zinaaribiwa kwa uzembe ,maendeleo yakuja vipi kama tutaishia kukarabati barabra kila siku na kupoteza wataalamu?
NILIPOTEZA MKE WANGU MPENZI KWA MTINDO HUU. LORI LILIHARIBIKA NA KUBAKI HAPO HAP BARABARANI, MVUA INANYESHA, SAA MBILI USIKU. KABLA HATUJALIFIKIA GARI INGINE IKAWA INAKUJA, HALAFU IKAWA NA FULL (HUWA NAFIKIRIA, NADHANI KULIONA VYEMA HILO GARI BOVU)ALIPOPITA TU, TUKALIGONGA KWA NYUMA MIMI NIKIWA NAENDESHA, YEYE AKAIWA AMEMPAKATA MTOTO WA MWAKA MMOJA, NA DADA NYUMA, SISI WOTE WATUATU TULITOKA KAMA TULIVYO, YEYE ALIUMIZWA NA KITU KICHWANI AMBACHO HATA SIKUJUI HADI LEO. KIOO CHA MBELE KILIVUNJIKA ILA SIO KWA KUTAWANYIKA (FIBERS) TUNAMSHUKURU MUNGU MAISHA YANAENDELEA.
ReplyDeleteWADAU, TUEPUKE KUENDESHA USIKU KADRI TUWEZAVYO. TUWE MAKINI MUDA WOTE KWAMBA KUNA TRACTOR, ROLI LIMESIMAMA NJIANI BILA ALAMA YEYOTE
Kwa jinsi hiyo picha ya chini ilivyopigwa inaelekea gari alilokuwemo mpiga picha (ambaye nina hakika alikuwa amekaa mbele kiti cha abiria) pia lilikuwa lina-overtake, na ni unafiki mkubwa kumshutumu dereva wa basi. Ankal kuwa makini na posts kama hizi. Humu ndani kuna wadadisi wenye upeo mkubwa sana.
ReplyDeleteMdau,
Arusha
me ni kijana nasoma construction engineering hapa mashariki ya kati,nilichoweza kugundua mm ni kwamba barabara zetu ukilinganisha na za huku mbelembele ni nyembamba sana,barabara zenye 2 lanes kama hiyo hapo juu zinajengwa ndani ya mji na mitaa isio na congestion sana,ila ikishakuwa barabara inaunganisha mji m1 na mwingine ni kama utaratib au sheria kuwe na atleast 2 lanes each side of the road with cars goes in opposite direction wd a barrier katikati yao,pia kila upande kuwe na atleast 0.5m space kwa ajili ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli,ajali nyingi za nyumban huko ni wakat wa kuovertake upande mwingine gar linakuja then kabooom,kwa mtindo huo ni ndoto ajali kupungua,solution ni kuongeza upana wa barabara,katikati kuweka kizuizi,kila upande gari ziende na uelekeo wake,wasimamiz wa sheria za barabarani wafanye kazi zao ipasavyo atleast tunaweza kupunguza ukubwa wa tatizo! Wako ktk ujenz wa Taifa:)
ReplyDeleteDah! Mdau Tue Aug 02, 04:42:00 PM2011 maelezo yako yanatia simanzi. Pole sana. Nakubaliana na wewe kuwa kuendesha usiku katika barabara kuu za Tanzania hi hatari sana. Kuna siku nilisafiri usiku kutoka Dar kwenda Arusha na kuhesabu malori 16 yaliyoharibika barabarani kati ya Chalinze na Segera. Huu ni wastani wa lori moja kila kilomita 10. Kwa wale ambao hulazimika kusafiri usiku, nashauri wahakikishe kuwa taa zao za mbele zinafanya kazi vyema kwani ajali nyingi za usiku zinaweza kuepukwa endapo taa zitakuwa zinafanya kazi vizuri. Magari mengi ya siku za karibuni yana taa za mbele za plastiki badala ya kioo (sealed beam). Kwa mazingira yetu ya Tanzania, taa hizi huota ukungu kwa ndani na hii hufanya mwanga wake ufifie. Nawashauri wale wenye magari yenye taa zenye ukungu ndani kutosafiri safari za mbali usiku na magari hayo kabla ya kurekebisha taa zao.
ReplyDelete