Ankal,
Hapa Sauzi wananchi wanaweza kujionea kwa uwazi kupitia mtandao jinsi viongozi wao wa kiserikali na kisiasa wanavyotumbua !

Mtandao maalum uliosheheni taarifa za mali, na zawadi ambazo viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge na raisi unaweka wazi pia zawadi kama vile simu, mifugo na vito ambavyo viongozi wamekuwa wakipokea kutoka kwa watu mbali mbali, mashirika na makampuni.

Pia mtandao huo ambao ni www.ipocafrica.org (Kama unavyojionea pichani)unaonyesha hata wabunge ambao wamewahi kuwa wakurugenzi wa makampuni na wale ambao wanamiliki hisa katika makampuni mbalimbali.

Natamani bongo nasi tungekuwa na mtandao kama huu, tujionee ‘vijisenti’ vya wanasiasa wetu !

John.
Eastern Cape, Sauzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni Kweli mdau uo mtandao ni muafaka kwa Tanzania, ila sitashangaa ukiuleta Bongo, kuna wanasiasa watasema tena "hizo ni hila na njama za pepo wachafu-shetani".

    NB:Iyo statement iliyotelwa na mbunge wa vitu maalum(CCM) Mchungaji Getrude Rwakatale, alipobanwa na tume ya maadili ya viongozi kwa kutuludisha form akadai ni hila za shetani tu ndio maana form zake haionekani.

    ReplyDelete
  2. Wa kwetu fedha zao hazipatikani kihalali hivyo, hivyo haitasadia kitu maana hazipo kwa majina yao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...