Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akikagua gwaride la Majeshi ya Angola alipowasili uwanja wa ndege wa Nchio hiyo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa Nchi wanancha wa SADC.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC uliofungiliwa leo Nchini Angola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai wakati walipokutana kwenye Ikulu ya Angola.Viongozi hao wapo nchini humo kuhudhuria mkutano wa Viongozi wa Nchi wanachama wa SADC ulioanza leo mjini Angola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mfalme wa Mswati wa Swaziland wakati walipokutana kwenye Ikulu ya Angola.Viongozi hao wapo nchini humo kuhudhuria mkutano wa Viongozi wa Nchi wanachama wa SADC ulioanza leo mjini Angola.


Ankal
ReplyDeletePicha ya kwanza hapo juu, si sahihi kusema kuwa Makamu wa Rais anakagua gwaride, hapo hakuna gwaride kwani hakuna vikosi zaidi hao askari unaowaona hapo, walichofanya hapo ni kutengeneza SALAAM maalum kwa kiongozi mgeni kutambua uwepo wake, inaitwa Guard of Honour. Ni salamu ya kijeshi na huko kuweka silaha mbele juu ni kupiga saluti.