Hivi ndivyo muonekano wa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar kwa kupande wa mjini na kigamboni unavyoonekana kutokea angani.
Maeneo ya Ilala,hiyo barabara yenye magari mengi ni Kawawa Rd inapokutana na Uhuru Rd.
Barabara ya Maendera inavyoonekana kutokea angani ikiwa imeshona ile mbaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. City center hakuna highways! Infrastracture bado poor need a lot of improvements.

    ReplyDelete
  2. Na usiku inaonekana kama vile Dubai? au inaonekana ni giza tuu?

    ReplyDelete
  3. Bongo jiji kubwa na zuri ila linatakiwa usafi sana na kukarabati majumba yake kwa kupigwa rangi vizuri, Sema sisi wa TZ hatuna usafi wa mitaa yetu pamoja na jiji letu lazima tufanye usafi wenyewe ili hata watalii wakija wataisifu nchi yetu si kila siku ni aibu wanasema kuwa TZ ni nchi chafu na ni kweli, tujaribu kuwa wasafi kwa nchi waBongo.

    ReplyDelete
  4. Ankal mji wetu kumbe mzuri kwa juu, lakini Kimbembe Ukiwa chini Foleni, kuchafu na watu hawazingatii mazingila kabisa wana jisaidia hovyo, wanatema mate hovyo msimu huu wa matunda wanatupa Mbegu na mabaki hovyo hovyo alafu wanailaumu silikali yetu tukufu tutafika kweli?

    ReplyDelete
  5. Ankali asante sana kwa taswila kwa kweli muonekano wa mji ni mzuri na unavutia

    kwa upande mwingine sijui kama muonekano wa mji unasaidia au unaweza kuita kuwa ni maendeleo ya taifa

    ikiwa mji umejengwa au utazidi kujengwa majengo marefu na bila kuzingatia vitu muhimu itakuwa haina faida yoyote ni sawa na kujenga nyumba juu ya maji itafika siku ya siku itaanguka au kuzama

    vitu muhimu ni kama vifuatavyo
    barabara za kuwafikisha kwa muda unaohitajika hao wahusika wanaohusika kufika hapo kwenye hayo majengo

    parking kuwepo na parking za magari zinazoweza kukidhi mahitaji ya watu wanaotaka kufika huko mjini kwa kupata huduma mbali mbali

    njia za maji taka na maji safi
    zamani kulipokuwa na nyumba ndogo za kawaida njia za maji taka na maji safi zilikuwa ni ndogo sana kutokana na majengo na wakazi wa sehemu hizo kuwa kidogo
    leo hii palipokuwa na nyumba ya kawaida ambayo inakaliwa labda na familia moja au mbili kwa sasa kumejengwa mjengo ambao ikiwa ni ofisi basi ni zaidi ya ofisi 50
    kama mjengo huo ni wa kuishi watu basi kila mjengo utakuwa unaishi zaidi ya familia 10
    sasa basi kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wa mijengo hiyo kunahitajika njia za kutosha za maji safi na maji taka

    kingine muhimu ni kuwa na njia za maji ya kuzimia moto kwaajili ya kujihami na matukio ya moto lazima kila baada ya nyumba kama 10 kuwepo na bomba la kuunganishia kupata maji ya kuzimia moto

    umeme ni muhimu kuwepo kwa taifa zima special kwenye maeneo ya mji kama huo

    kitu kingine hali ya ulinzi kwa maeneo kama hayo ni lazima yawe ya uhakika sina uhakika kana wana usalama wamefanikiwa kuweka camera za mitaa kwajili ya kupambana na matukio ya uharibifu kama wizi n.k

    mdau mwenye upeo wa mbali.

    ReplyDelete
  6. Ankal, tupatie picha za bongo za miaka ya mwanzoni mwa 90 ili tuakisi vizuri au japo kukumbushia enzi tu.

    ReplyDelete
  7. KUNA KITU KIMOJA KATI YA YOTE AMBAYO HUWA SIELEWI KWA NINI LABDA WADAU MTANISAIDIA.NI KUHUSU MITARO YA MAJI MACHAFU AMBAYO KWANINI WALIVYOICHIMBA WASIZIBE JUU NA KUACHIA SEHEMU PEKEE AMA SHIMO LA KUPITISHA MAJI HAYO AMBAYO YATASAIDIA KUPITISHA MAJI YA MVUA ZINAZO NYESHA KUPUNGUZA MAFURIKO YA BARABARANI.SIKU ZOTE NINAPOPITA KARIBU NA MITARO HIYO UTAKUTANA NA HARUFU MBAYA YA MAJI MACHAFU YALIYOCHANGANYIKA NA UCHAFU UNAOTUPWA NA WANANCHI IKISHA KUSABABISHA MBU WENGI KUZALIANA.HAPOHAPO UTAKUTA KUNACHANGISHWA PESA MAMILIONI KUSAIDIA KUTOKOMEZA MALARIA HUKU SERIKALI INAPALILIA MBU KUZALIANA HOVYO SASA HAPA HUWA SIELEWI KABISA INAMAANA SISI WATANZANIA HAKUNA KABISA MTU AKA-DESIGNE MASHIMO AMBAYO YATAENDANA NA JAMII NA KUPUNGUZA MARADHI?????????

    ReplyDelete
  8. WAKUBWA, HELL NO I TAKE IT BACK, 'WAHUSIKA' FUMUENI MAJENGO NA MIUNDO MBINU ILIYO KWENYE RESERVES ZA MIUNDO MBINU MAMA, WALIPENI WANANCHI WAPENI VIWANJA NJE YA MJI WAJENGE KWENYE MAENEO YALIYOPANGWA YENYE MIUNDO MBINU KAMILI (MAJI, MAJITAKA, UMEME ETC) HALAFU MU.EMBARK ON A GRAND DAR ES SALAAM MODERNISATION PROGRAM. ITACHUKUA PESA NYINGI LAKINI NI AFADHALI SASA HIVI KULIKO KUSUBIRI MPAKA 2050 WAKATI KUNA WAKAZI MIL SIJUI 20 HIVI HALAFU NDO MUANZE. WENZENU WATANI WA JADI WAMEANZA, CHEKI THIKA ROAD YAO NA MAFLYOVERS MENGINE, YOTE NI KATIKA KUREKEBISHA MAKOSA YA KIMIUNDO MBINU.

    AU KAMA VIPI ACHENI BONGO IENDELEE KI-FREESTYLE HALAFU MKAJENGE MJI MPYA BAGAMOYO (KUNA MTU ATATOKA USINGIZINI SASAHIVI KUDADADEKI MANAKE UKIPIGA CHAPUO LA KUJENGA MJI WA BWAGAMOYO HATA KAMA KAPUMZIKA MIGUU ITAMPELEKA OFISINI KUSAINI MAKARATASI, LOL!).

    WITH GOOD VISION (PLANNING, OUTSOURCING ETC), HARD WORK N.K. DAR ES SALAAM SHOULD BECOME THE BIGGEST CITY AND THE LARGEST COMMERCIAL METROPOLITAN OF THE BIGGEST ECONOMY IN EASTERN AFRICA IN 2035!

    ReplyDelete
  9. Ahsante Ankal kwa taswira hizi. Hili ndilo jiji la Dar Bwana lenye kila sifa, lakini sifa kuu ni UCHAFU!!!

    ReplyDelete
  10. Picha zinaonyesha jinsi mji ulivyojengwa kama magugu shambani. Hakuna cha mpangilio wala nini. Tulijijengea bora liende.

    ReplyDelete
  11. Jamani matatizo haya yote yametokana na viongozi wetu kutoona mbali. Na vile vile hakuna Mipango ya miji (town planning). Lazima tuangalie ongezeko la watu, mwaka hadi mwaka na tukadirie labda kila baada ya miaka kumi na tuweke mikakati ya kukabiliana na ongezeko hili, kama vile upanuzi wa barabara, upanuzi wa mifereji ya maji taka, uenezaji wa mabomba ya maji safi katika makazi mapya na mambo mengine mengi ambayo nikianza ya kuyajadili tutakesha hapa. Mimi nina uhakika kwamba viongozi wetu wengi katika manispaa nyingi hapa nchini hawana ujuzi au qualifications za town planning. Watu wamekaa mkao wa kula tu na wamewekwa pale kwa ajili ya kujuana. Huu ndio ukweli wa mambo. Mimi hii ndio kazi yangu, na inaniuma kuona nchi yetu inaangamia namna hii.

    ReplyDelete
  12. ndio mnaendelea kunufaika na muungano kisha mnasema hakuna serikali ya bara,zanzibar mumeiua hamtski hsys kuifanya mjii mkuu kwakuwa biashara zitahamia kule.Majengo ya Zanzibar tokea Karume.hongera CCM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...