maofisa wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) wakielezea shughuli zinazofanywa na mfuko wakiwa kwenye banda lao lililopo kwenye viwanja vya maonyesho ya nanenane yanayoendelea mkoani Kagera, aliyesimama ni Paul Kazi na mwingine ni Thadeo Rweyamba.
afisa mifugo wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi Patric Ishengoma akionyesha ngozi ya mbuzi ambayo inatumiwa na wajasiliamali kutengeneza viatu vya aina mbalimbali walioko kwenye banda la halmashauri hiyo lililopo katika viwanja vya maonyesha ya nanenane yanayoendelea mkoani Kagera kwenye viwanja vya Kyakailabwa.
Mama kalumuna ambaye ni afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi akionyesha aina za ndizi zinazozalishwa wilayani humo.
baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi wakionyesha mazao mbalimbali ya chakula na biashara yanayozalishwa wilayani misenyi kwenye banda lao lililoko kwenye viwanja vya maonyesho ya nanenane vilivyoko Kyakailabwa.
Hizo ndizi gani mbona hazieleweki?..tunahitaji kuona ile midizi halisi ya Kagera..zile NSHAKALA..NTOBE,NCHONCHO..haa haa haaa.Asante.
ReplyDeleteDavid V