Wachuuzi wa biashara ndogo ndogo wa stand kuu ya mabasi mjini Lindi wakiuza bidhaa zao kwa abiria wa basi lililokuwa likitoka Mkoani Mtwara kwenda D,slaam,vijana wengi hapa nchini wamejikuta wakijiingiza katika biashara ya aina hiyo kufuatia ukosefu wa ajira
Akina mama wanaojihusisha na biashara ya kuuza samaki eneo la Nangurukuru wilaya ya kilwa wakisubiri wateja kama walivyokutwa na mpiga picha wetu hivi karibuni,kitoweo hicho hivi sasa kimekuwa kikinuliwa kwa wingi kufuatia kuendelea kwa mfungo wa ramadhani.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha kiranjeranje wengiwao wakiwa watoto wenye umri wa kwenda shule wakigombea maji kutoka kwenye moja ya vyanzo vilivyopo kijijini hapo.
Bw Emanuel Rwamelo akinywa maji kwa kutumia ndoo kutoka katika moja ya vyanzo vya maji katika kijiji cha kiranjeranje wilaya ya kilwa, kama alivyokutwa na mpiga picha wetu hivi karibuni.Picha na Muhidin Amri.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...