Baadhi ya wageni   waliohudhuria kwenye mabanda ya maonyesho ya wanawake wajasiriamali yaliyofanyika Aug,4,2011 kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ni maalumu kwaajili ya Mke wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mama Dkt.  Denise Bucumi Nkurunziza alioyaandaliwa na Mwenyeji wake Mke wa Rais Na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete ili kuangalia shughuli za wajasiriamali wanawake nchini. Mama Nkurunziza yupo nchini katika ziara ya siku sita
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akimpatia zawadi ya kinyago maalumu Mke wa Rais wa Burundi Mama Dkt. Denise Bucumi Nkurunziza Aug 4,2011 ,jijini Dar es Salaam
 Mke wa Rais wa Burundi Mama Dkt. Denise Bucumi Nkurunziza (kushoto) akimpatia zawadi ya kikapu cha asili cha kuhifadhia   chakula Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete jijini Dar es Salaaam Aug. 4,2011 , Hafla hiyo imefanyika na kuambatana na  Futari kwaajili ya wanawake wajasiriamali walioandaliwa na Mke wa RaisMama Salma Kikwete
 Mjasiriamali Elina Mgonja kutoka Kibaha mkoani Pwani (alievaa vazi la utamaduni akimpa maelezo  kuhusu utengenezaji wa kitenge cha aina ya Batiki Mke wa Rais wa Burundi Dkt. Denise Bucumi Nkurunzinza alipotembelea mabanda ya maonyesho ya wajasiriamali wanawake 
 Mjasiriamali kutoka kikundi cha Haika jijini Dar es salaam Elihaika Mrema (kushoto) akitoa maelezo ya ushonaji nguo kwa mke wa Rais wa Burundi Dkt.  Denise Bucumi Nkurunziza na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
Mjasiriamali kutoka Rocky,s Product Zahrock Ahmed (kushoto) akionyesha bidhaa zake mbalimbali anazozitengeneza kwaajili ya viungo mbalimbali vya chakula (spices) wakati Mke wa Rais wa Burundi Mama Dkt. Denise Bucumi Nkurunziza alivyotembelea katika mabanda ya maonyesho ya wanawake wajasiriamali katika viwanja vya Taasisi ya WAMA. Picha zote na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...