Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) baada ya kukimkabidhi mbuzi mzee wa Kanisa la KKKT Usharika wa Sinza Bw. Manase Mwana Ndanshau wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la KKKT Usharika wa Mwenge jijini Dar es Salaam leo. Mbuzi huyo alinunuliwa kwa sh. milioni moja. Jumla ya shilingi milioni 64 taslimu zilipatikana hapo hapo  katika haramabee hiyo.
 Kwaya ikitumbuiza
 Waumini wakileta mbuzi ili wapigwe mnada kuchangia kanisa hilo
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh Edward Lowassa Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi hiyo George Fupe  wakiongoza kuimba wakati wa mnada wa kuchangia ujenzi wa kanisa hilo
Mh Lowassa akimpa mkono mmoja wa wachangiaji wa ujenzi wa kanisa hilo

Picha na Habari na  Francis Dande
wa Globu ya Jamii
KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mwenge, Dar es Salaam, limepata zaidi ya sh. milioni 119 katika harambee  iliyoendeshwa leo na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kwa ajili ya kuchangisha fedha za kumalizia ujenzi wa kanisa hilo.


Hadi mwisho wa harambee hiyo iliyofanyika kwa watu kuchangia papo hapo na kunadiwa vitu mbalimbali, zilipatikana sh. 119,562,300 zikiwemo fedha taslimu sh. milioni 30.7 ambazo Lowassa alichangisha papo hapo na kumkabidhi Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi hiyo George Fupe.


Mapema katika risala, Mchungaji  Luhuvilo Sigala alisema, ili kumalizia ujenzi wa kanisa hilo zilikuwa zinahitajika sh. milioni 94 na kwamba hadi sasa kanisa hilo limeshajengwa kwa asilimia zaidi ya 80.


Baadhi ya vitu vilivyonadiwa na Lowassa ambaye alifuatana na Mkewe, Regina Lowassa, ni mbuzi watano waliotolewa na waumini, mchele, sukari na mikungu ya ndizi.


Akizungumza katika misa kabla ya harambee hiyo, Fupe aliwataka waumini wa Kikristo na hususani wa KKKT kuhakikisha wanawalea watoto wao katika mazingira ya kupenda dini ili kuweza kupatikana waumini wa baadae.


Mchungaji Fupe alisema kujenga makanisa bora bila  kuwalea watoto katika malezi hayo hakutakuwa na faida yoyote kwa sababu baada ya miaka ijayo  yatabakia makanisa mengi yasiyo na waumini.


"Kuna nchi nilitembelea hivi karibuni nikashangaa kuona makanisa makubwa makubwa, nilipohudhuria misa na kuombwa kuiendesha nilishangaa kukuta kanisa kubwa lakini ndani mna waumini wachache mno" alisema Fupe na kuongeza.


"Nikauliza mbona kanisa ni kubwa mno tena la ghorofa lakini waumini wachache? nikaambiwa siku hizi waumini hawaji kanisani na sababu kubwa ni kwamba vijana wamenyimwa utamaduni wa kuabudu walipokuwa watoto", alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera Mhe. Lowasa, juhudi zako zinafaa kupigiwa mfano. Ongeza juhudi tupo nyuma yako.

    ReplyDelete
  2. Dah hongera bwana Manaseh Mwana Ndanshau kweli mzee unakipaji cha mnada uliwakimbiza watu wa mwenge mpaka basi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...