Mke wa Rais wa Burundi Mama Denise Bucumi (kushoto) akiongea na waandishi wa habari katika Ofisi za Taasisi ya WAMA jijini Dar es Salaam leo baada ya kufanya mazugumzo na Mwenyeji wake mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia), Mke huyo wa Rais wa Burundi atakuwa na ziara ya siku sita nchini Mke wa Rais Wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake nchini WAMA Mama Salma Kikwete(kulia) akifafanua jambo wakati alipoongea na waandishi wa habari August 3,2011 katika ofisi ya Taasisi yake jijini baada ya kumkaribisha mke wa Rais wa Burundi Mama Denise Bucumi Nkurunziza (kushoto) aliepo nchini kwa ziara ya siku sitaMke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akimkabidhi vipeperushi vya Taasisi yake Mke wa Rais wa Burundi Mama Denise Bucumi (kushoto) alipotembelea katika Ofisi za Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo alifanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya wanawake na watoto pamoja na masuala mengine ya kijamiiMke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akimkabidhi vipeperushi vya Taasisi yake Mke wa Rais wa Burundi Mama Denise Bucumi (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja katika Ofisi za WAMA jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Mdau Mwanakombo Jumaa wa MAELEZO
Home
Unlabelled
mke wa rais wa burundi aanza ziara ya siku sita nchini leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...