Mkuu wa mkoa wa Kagera,Mh. Mohamed Babu
Na Audax Mutiganzi,Bukoba

MKUU wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu ameziagiza halmashauri za wilaya mkoani humo kuhakikisha zinatenga fedha kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya makusanyo ya mapato ya ndani hususani yanayotokana na ushuru wa zao la kahawa zitakazowawezesha wakulima wa kahawa mkoani humo kuongeze uzalishaji.

Babu alitoa agizo hilo hivi karibuni katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya taasisi ya utafiti wa kahawa nchini (TACRI) ambayo katika kanda ya Kagera ilifanyika katika kituo cha utafiti wa mazao kilichopo maruku nje kidogo ya mji wa Bukoba.

Alisema fedha hizo zikitengwa zitafanikisha mkakati wa serikali ya mkoa wa Kagera wa kuboresha kahawa inayozalishwa mkoani humo pia wa kuongeza uzalishaji wa kahawa toka tani 13,000 za sasa hadi tani 44,600 ifikapo mwaka 2016.

Mkuu huyo wa mkoa alisema huyo wa mkoa alisema fedha hiyo zitawasaidia wakulima wa zao kahawa kujinunulia pembejeo, mbolea ya samadi na ya viwandani, kupanua mashamba, kuboresha mashamba yaliyopo na pia zitawajengeauweezo kupata miche bora yenye uwezo wa kupambana na magonjwa yanayoshambulia mikahawa.

Aliendelea uzalishaji wa kahawa unapoongezeka na pia kahawa inayozalishwa ikawa ubora umaskini wa kipato wa mtu mmoja mmoja unapungua sana, alisema kwa sasa katika mkoa wa Kagera wastani wa kipato kwa mtu mmoja mmoja ni wastani wa shilingi 420,000.

Babu alisema kipato hicho ni kmidogo sana na kinatokana na uwajibikaji wa wananchi mkoani Kagera, Alisema baadhi ya wakulima mkoani Kagera bado wanaendekeza kilimo cha kizamani ndio maana kilimo chao hakina tija.

Alisema sasa ni wakati wa wananchi wa mkoa wa Kagera kubadilika na kutafuta namna ya kuongeza uzalishaji , mkuu huyo wa mkoa alisema wananchi wataongeza uzalishaji wa mazao ikiwa watafuata maelekezo ya kilimo wanayopata toka kwa mafisa kilimo.

Aliipongeza taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) kanda ya Kagera kwa kazi nzuri ya inayoifanya ya kutafiti miche bora ya kahawa inayoweza kuhimili magonjwa, pia aliishukuru jumuia ya ulaya kwa jitihada inazozifanya za kuiwezesha taasisi hiyo iweze kufanya kazi yake vizuri ya utafiti wa miche bora ya kahawa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya TACRI nchini Vedasto Ngaiza awali katika hotuba yake alisema uzalishaji wa kahawa mkoani Kagera unachangiwa na elewa mdogo walionao baadhi ya wakulima.

Ngaiza alisema kuna baadhi ya wakulima wa kahawa wanaopiga matumizi ya mbolea ya chumvichumvi, alisema baadhi ya wakulima wanadai kuwa mbolea hiyo ina madhara, alisema mbolea ya chumvichumvi haina madhara yoyote.

Alisema mbolea hiyo wakulima wakiitumia wataongeza uzalishaji wa kahawa, aliendelea kusema kuwa wakiongeza uzalishaji wa kahawa watakuwa wanaongeza kipato chao hivyo wataweza kuondokana na umasikini.

Naye Meneja wa TACRI kanda ya Bukoba Malyatabu Ngh'oma katika taarifa yake alimweleza mkuu wa mkoa kuwa zaidi ya miche bora ya kahawa milioni 8.2 imezalishwa na TACRI tangu mwaka 2001 hadi mwaka 2011, alisema iliyosambazwa kwa wakulima ni zaidi ya milioni 6.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...