hi Ankal,

Pole na suam! na nina imani zimebaki siku mbili hatimaye uimalize na kusherekea!!

Ankal naomba unitolee tangazo langu kwenye libeneke lako kama ifuatavyo:

Mimi ni mwanaume wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 46 naitwa Devis, nina Uraia wa moja ya nchi za Ulaya( Nchi naweka kapuni!),mkristo lakini siendi kanisani kila jumapili ila nashiriki kwenye misa muda ukiruhusu!, naishi hapa Ughaibuni(Europe) zaidi ya miaka 15 natafuta mwanamke wa kitanzania mwenye umri usio chini ya miaka 27 ambaye pia anaishi kati ya moja ya nchi za Ulaya na awe na elimu sio chini ya kidato cha nne, awe anaweza kuongea Kiingereza kwa raha zake!, Kiswahili kama Kawa! na mojawapo ya lugha nyingine ya kigeni kama French. spanish na nk.

Pia napenda kuwa muwazi zaidi sitaki mwanamke mwenye udaku mwingi, awe anajua na kufahamu anachotaka katika maisha yake na anaelewa walau maisha ni nini, yaani anataka nini? ili iwe nini! na kwa sababu gani!? Sina muda wa kuanza kufundishana maisha ila wa kusaidiana maisha kwa hali na mali . 

Mimi sio tajili ila mwanamke atakayejitokeza awe radhi kukudhi mahitaji ya kimaisha pamoja nami hapa Ughaibuni na Tanzania. Awe radhi walau kuzaa na mimi watoto walau wawili au zaidi na kuishi na mimi huku nilipo bila matatizo. Awe Muwazi kwa kila kitu, kikazi(Kielimu), kifamilia na kijumuia(Society and freindship), anayejipenda kimawazi, kimwili na kujiamini kibinafsi, hupendelea mazungumzo ya kiuchumi, kijumuia, kimaendeleo na kisiasa katika ulimwengu.

Kwa yeyote mwanamke mwenye nia ya kufahamina na mimi , tafadhali nitumie majibu yako kwenye email yangu kaufmann31@yahoo.de na picha zako. Bila picha yako sitajibu email yako ila nakutakia bahati njema maishani.Maelezo zaidi baadaye na majukumu mema.

Asanteni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. maisha nini? anataka nini? ini iwe nini? hizo ndio ishu zako, Je, na wewe umechelewa kuona kwanini? umeshindwa kupata mtu tanzania kwa nini? na kwa sababu gani? mwanamke..., mwanamke...., mwanamke....hiyo hulka yako ndio imekufanya usioe muda wote na kutokuwa na familia hadi sasa!! Na utakaempata hatadumu. Labda uchukue mwenye watoto akuletee muwalee pamoja. Be good to women. Stop chauvinism. Women are not commodities

    ReplyDelete
  2. Mzee umeweka wazi vitu unavyotaka wewe sio vibaya.Ila na wewe weka picha yako hapa ili wadada wakuone ukiwa na gazeti la mwezi uliopita au week iliyopita.Nasema hivi kwa sababu wadau wanaweka picha za miaka 25 iliyopita halafu ukija kutana nae inakuwa noma si unaelewa tena.Pia nakushauri tumia familia yako walioko nyumbani wakutafutie mwenzio hii ni njia rahisi kuliko mtandao.

    ReplyDelete
  3. Wazo zuri mdau wa nchi ya kapuni(ughaibuni). Mimi ningelikushauri ufike kwenye minuso mbali ambayo hufanywa na waTZ ili ujichagulie atakayekufaa. Lakini pia kutakuwa na Miss Vodacom hivi karibuni angalia yupi mzuri wao ili uoe maana wewe kwa vile una uraia wa nchi ya ughaibuni wazee hawatapinga na viza pia atapewa mara moja. Mdau nafasi ndio hiyo!

    ReplyDelete
  4. Hutaki kusema nchi unayoishi halafu email yako inakuuza yahoo.de

    ReplyDelete
  5. Baba umechelewa. Unataka mwanamke unayemzidi miaka takribani 20?? big no if a I have to coose. 2. hao watoto mtakaozaa wauite babu au? kumbuka atakapokuwa na umri wa kuanza shule wewe utrakuwa close to 60. Nakushauri forget about geting married man!!

    ReplyDelete
  6. Umechemka ... Nchi usiyoitaja yahoo.de alafu Kaufmann ni maarufu huko Deutschland kwa usafiri na supermarket.
    Bro hebu uwe unafanyiwa counceling kabla ya kuchemka kwenye mtandao. Ankal kampuni yake bado ndogo na thats why hana mtu wakuchuja contents zako. Unapokuwa serious weka picha yako.
    Ushauri wangu ndio huu.

    ReplyDelete
  7. hujatumia kauli nzuri ya utafutaji, ni km vile unacommand! i guess siyo mwanaume mwema wewe, wewe umeandika bila kuweka picha ila wenzio ndo wakuwekee picha eti la sivyo hutajibu..utadhani umeambiwa huku bongo kuna wanawake wenye shida sana na wanaume hivyo ukisema lolote utapata tu! japo ni mtu mzima but hujatulia hata chembe, jua lishakuchwa ndo unatafuta mke! wakati unavaa suruali ulikuwa wapi na sasa wavaa msuli ndo watafuta..loo! jifunze lugha nzuri.

    ReplyDelete
  8. looo, ati mwanamke chini y miaka 27 huyo si atakuwa sawa na binti yako? acha hizo kwani ulikuwa wapi miaka yote hiyo mbaba wewe? yaelekea ulikuwa unachagua saana na lazima utapata koroma tuu piga ua kiza hiki cha dot com binti umri chini ya miaka 27 lazima itakula kwako tu!

    ReplyDelete
  9. Duh pole sana, 46yrs hujaoaaaaaaaaaaa na kauli hizo hatushangai bro maana hakuna mwanamke atakaeweza kuvumilia uj..ga.... ooops!
    Haya kazi kwenu kinadada wenye shida ya wachumba wa ughaibuni jina kapuni siku zote ulikuwa unapiga wapi saaa hizi ndio unatafuta shuka eti na watoto lol kumpa mwenzio mzigo wakuwa mjane bureeeeeeee kisa ughaibuni jina kapuni...!
    Kila la heri ughaibuni jina kapuni

    ReplyDelete
  10. Pumbafu Mkuwa we haya ndio uliyokwenda jifunza UGHAIBUNI yaani hata kama maisha ya wasichana wa kitanzania ni magumu lakini kwa lugha hii hupati hata changu doa . tafuta wadhungu waliokufunza lugha hiyo ya kihuni, isiyo na adabu kwani uliambiwa mwanamke ni BIDHAA.
    Muwe mnarudi nyumbani kujifunza mengine mliyosahau kama matumizi ya KAULI katika jamii.
    MTANZANIA HALISI

    ReplyDelete
  11. Jamani kasikia. ushauri, sisi watanzania/wabongo/wafrika, tuna utaratibu wa kupata wenzi wetu.jamani hata kama umekaa ulaya miaka 90 yaani una shindwa kurudi kwenu ukatafute mwenyewe au kwa msaada wa ndugu,dada,mashangazi, hukosi mke wa kuoa,badala ya ya kumwaga mbwembwe humu,hebu tuwe waafrika linapo tokea swala hili la kuoa nyumbani rudi.Kaka S.

    ReplyDelete
  12. Ukiendelea na hizo kauli zako hutakaa upate mke, hilo sahau. bora uende kuwa padre tu. mwanaume una kauli mbaya sana sana, mke atayevumilia hayo masimango yako. mwanamke anakiwa kumbelelezwa, kusikilizwa, kuelimishwa taratibu kwa mapenzi. tena kwa babu kama wewe unatakiwa umlee mkeo kama mwanao. Ila nawashauri wadada wote wanatafuta wachumba wasijitokeze kwako, una tabia mbaya sana. watapata wanaume wengine siyo wewe.

    ReplyDelete
  13. wewe ingawa uko ulaya reasoning yako ni very poor. utatafutaji mke kwa kuangalia mipaka ya nchi kwamba lazima awe anaishi katika nchi fulani? kwa hiyo kama mtu yuko new zealand humtaki?

    ReplyDelete
  14. Naomba niulize, wewe unafanya kazi gani. Unaongea lugha ngapi? Je unaongea kingereza fluent? Na umesoma mpaka kiwango gani?

    ReplyDelete
  15. we ni fala, nadhani umeogopa kuweka picha yako na kuitaja nchi maana ulijilipua, ulikuwa unasubiri upate makaratasi ndo ufikirie kuoa, umeikana nchi yako na kujiita mkimbizi toka nchi zenye vita ili upate uraia, huna hekima wala busara mpumbavu wewe, unazani ukisema uko ughaibuni ndo utatetemekewa,unaongea kaa wanya ndo maana hupati mwanamke, watanzania kibao wamejaa ughaibuni tena wenye sura na tabia nzuri ila nahisi una kasoro kubwa mno, baba mtu mzima ndo unafikiria kutafuta mke tena kwenye mtandao! we kenge kweli lol, kafe mbele dunya wewe.

    ReplyDelete
  16. umekaa huko hadi unajiita KAUFMANN (maana yake "merchant")! rudi nyumbani umalizie kipande kilichobaki cha uhai wako na ndugu zako. usitafute kuharibu maisha ya binti zetu

    ReplyDelete
  17. Mheshimiwa mbebabox kuna genetics center nyingi tuu hapa Deutchland, peleka hizo request zako wakuumbie msichana unayemtaka kisha mlipie mamaako flight aje wampande hizo genetics akuzalie huyo mwanamke unayemtaka kisha umuwowe

    ReplyDelete
  18. Nyoo nani akubali kuolewa na mbabu kama wewe???? hata nguvu ukute zimeshakuishia!! kafie mbele huko!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...