Habari za kazi Uncle michuzi,
mimi shida yangu kubwa naomba wadau wanisaidie zimepita siku kama tatu nilisoma kwenye Blogu yako kwamba huko zanzibar kuna kituo cha kusaidia vijana walioshindikana yani wavuta bangi na pombe bila mpangilio sasa kuna wadau waliotoa anuani ya hicho kituo please naomba unisaidie kwani nina mdogo wangu wa kiume ameshindikana ni msomi ana DEGREE lakini amekuwa mzigo wa familia Uncle naomba wewe na wadau mnisaidie.

ASANTENI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. pole ndugu yangu,ila wala usipate shida kwenda hadi zanzibar kwani huduma kama hiyo inapatikana hosp ya mhimbili kule kwenue jengo la watu wenye ugonjwa wa akili, kuna kituo au huduma za TAPP/MAT kuna doz ambazo hupatiwa na ataacha kabisa,utawakuta vijana wengi sana wamepata huduma hizo na sasa wako sawa na wanafurahia maisha na wengine wameanza kutafuta ajira na kujishughulisha.

    ReplyDelete
  2. fika pale muhimbili kuna kituo cha kutoa huduma hizo kule kwenye jengo la wagonjwa wa akili,wapo vijana wengi walokuwa wanatumia madawa na sasa wameacha,atapata dawa hizo na ushauri,pole sana

    ReplyDelete
  3. fika pale muhimbili jengo la wagonjwa wa akili kuna huduma hizo na wapo vijana wengi wameacha kabisa

    ReplyDelete
  4. Kituo cha kuachishwa madawa ya kulevya na pombe. Sio kituo cha watu walioshinda! Uliza Wizara ya Afya, Zanzibar au Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais. Kila la heri. Kuna waliweza kuacha kabisa, pia kuna waliokwenda hapo mara tatu ndio wakaacha. Kuacha hayo mambo ni wewe binafsi mtumiaji uamue. Mimi niliweza kuacha fegi kwa kudhamiria kuwa sasa fegi siitaki tena katika maisha yangu. Hapo nyuma niliweza kuacha siku chache na kurudia lakini nilipodhamiria niliweza na sasa niko safi miaka kumi!

    ReplyDelete
  5. pole sana tafafhali e mail me khamissaid@gmail.com, nitakulink na wahusika
    Mdau. zenj

    ReplyDelete
  6. Pole sana ndugu yangu. Nenda Tanga Lutindi Hospital, wana huduma nzuri sana kwa wiki wanacharge sh.25,000/=. Lakini huduma zao ni nzuri sana na wameshasaidia watu wengi sana.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana mdau kwa jitihada zako za kutaka kumnusuru mdogo wako.

    Natumaini atathamini msaada munaompatia kama familia na kuacha kabisa.

    ReplyDelete
  8. Achana na muhimbili...pale wawekwa kama wafungwa, mazingira sio ideal...no couselling...wagonjwa wapigana waachiwa waumizana, Tanga Lutindi is the best! kituo kilianzishwa na wamisionari wa ujerumani...for more details, kaulizie pale muhimbili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...