Rebecca Balira ... yesterday
Rebecca Balira

A SCIENTIFIC researcher used a 21-year-old she flew in from Africa as her unpaid slave, a court heard yesterday.


Rebecca Balira is alleged to have forced Methodia Mathias to cook, clean and wash for her while using her as a nanny to her three kids.


The Tanzanian had been promised a £96-a-month salary, but was never paid, London's Southwark Crown Court heard. Jurors were told she was punched when she displeased her boss.


Balira, 47, of Thamesmead, South London, is studying at the London School of Hygiene and Tropical Medicine. She denies trafficking a person for exploitation and holding another in servitude. Case continues. 

Source: http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/3727333/Scientist-kept-girl-of-21-as-a-slave.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kwa hapa UK hii ni kesi kubwa sana. Article haijaeleza mtuhumiwa ni kutoka nchi gani, lakini nadhani atakuwa ni mtanzania (my guess). Tukumbuke kila binadamu anastahili haki hata kama ni maskini.

    ReplyDelete
  2. Watu kama hawa ndio wanaongoza vyama vya upinzani. Sasa subiri wapewe madaraka, utaona UNAFIKI wao. Unamdhulumu mwenzio vijipesa vyake na kusingizia wewe mstaarabu unaishi UGHAIBUNI kwa waastaarabu. Wanamapinduzi wapo wengi!!

    ReplyDelete
  3. nimeisoma na mimi kwenye mazageti. aibu kwa mama mzima namna hii kukubali kuwa mtumwa!

    ReplyDelete
  4. noma, huyu mdada wa medical research mwanza,tanzania

    ReplyDelete
  5. Mbona watu wengi wanaghabu sana ,wanaishi nje ya Tanzania kama watumwa kwa ajili ya kutafuta ridhk,hivi kwa nini ?
    Umaskini mmbaya sana pia nadhani Watanzania inabidi tujifunze somo la upendo wa kweli la sivyo tunaweza kuchekesha dunia siku moja.

    ReplyDelete
  6. Lione kwanza hata kwenye picha linaonekana lina roho kutu sana!

    ReplyDelete
  7. Jamani tusimlaumu sana huyu mama. Wafanyakazi wa ndani nao ni vigeu geu. Unamchukua kutoka Tanzania akifika huku anarubuniwa na watu amgeuke mwajiri wake ili apate hifadhi na kubaki huku. Kwa hali halisi haiwezekani kwa mtu anayekuja huku kusoma kama huyu mama halafu aweze kumlipa mshahara wa kima cha chini cha Uingereza. Huyo mfanyakazi kama alikuwa anataka kubaki huku angemweleza mwajiri wake ukweli na sio kumwaribia kwa jinsi hii.

    ReplyDelete
  8. huyu mama anafikiri Huko ulaya ni bongo alikozoea kupiga maids na kmrudisha kijijini bila kumlipa au kumlaza jikoni au kumpa ukoko atakoma huko UK. lazima awajibishwe tatizo watu wamesoma lakini hawajui Human Rights. Lakini yawezekana maid naye kafundishwa maana maids wa kibongo nao ni noma! hawatabiriki. Tuache sheria ichukue mkondo wake

    ReplyDelete
  9. Jamani story kamili hamuijui. Huyu binti kamgeuka huyu mama, kapata jamma kijana wa Kenya wanasuka hii mipango. Alipelekwa kwa njia halali kwa maana ya kusaidiana kama ndugu. By the way ni binamu yake kabisa na wanatoka wote BUKOBA. Kufika kule katika kupeleka watoto nursery na shule akakutana na huyo kijana. Na hivi sasa ndo wanaishi nae huyo kijana. Sasa msiwe mnaongea vitu visivyo vya uhakika. Na hata kupigwa picha huyu mama, ni kwamba yote ni mipango. Mama kamaliza phd yake on time kabisa, karudi nimr mwanza lakini inabidi aende uingereza kwa ajili ya kesi. Rebecca alikua na nia ya kumsaidia ndugu hakutaka kumchukua mtu asiyemjua. Hili ndo lililomkuta. Passport alimtafutia officially la ilikuwa ya domestic worker-go and return ticket. Sasa kama alivyosema mtoa maoni mwingine, wasichana wa siku hizi ni hatari hata ndugu anakugeuka ndivyo alivyogeukwa Rebecca.

    ReplyDelete
  10. wengine humundani wanafikiri huyu mama ndio alofanywa mtumwa ,Hizi kesi zipo nyingi si Tanzania tu ukiangalia film ya I M SLAVE ni msudani naye anafanywa kama hivi,lakini hawa ndio wanaochukua sheria kwa sheria ya ulaya ukifanywa kama hivi basi unapewa sheria haijali umetoka au unafanya kazi kwa nani,
    nilikutana na Dada mmoja Amsterdam na yeye anatoka moshi alisafirishwa na mzungu kufika kule kamfungia ndani tulikutana nae market anashangaa kumbe huku kuna watu wanaongea kiswahili anafikiri ni mswahili peke yake dunia yote hii,basi amekimbia kwa mzungu wake sasa anakaa na mshkaji wangu tokea siku ile.Pia Ugiriki kuna muithiopia mmoja amechukuliwa kwao na kuwekwa ndani analipwa 50 euro kwa mwezi akizituma kwao wanamshukuru hadi watu walipomshtua ndio amemkimbia anafanya kazi kwengine kwa 800

    ReplyDelete
  11. Hawa ndo serikali yetu inawasomesha wapo kibao huku wanachafua nchi yetu na bado mshahara wake upo pale pale. Mfanyakazi wa serikali anaaga kuja kusoma anaendelea kulipwa kule aliko anapiga box bila kusoma anarudi bila cheti serikali inaendelea kumlinda. Mi nadhani imefika wakati kwa serikali kutumia mishahara inayolipa kutoka na kazi na si kulipa tu kwa kuamini mtumishi yuko majuu kumbe anajiendeleza tu. Na pia kama si serikali imempeleka mtumishi wake kusoma mbona inaendelea kumlipa? Haya sasa hawa ndo wasomi waliotumwa na serikali kusoma wakisha maliza wanakuwa madaktaari wataacha kukuchoma saline, wawe wabunge wataacha kuwaua albino ili wapate pesa?

    ReplyDelete
  12. Wacha sheria ipate ukweli. Binadamu hatuna shukrani wakati mwingine. Tunaweza kumrahumu Rebecca, kumbe binti kapakaza. Au tunaweza kumrahumu binti, kumbe Rebecca ndio mwenye makosa. So let us not judge the book without its cover.

    ReplyDelete
  13. Kesi ndiyo imeanza kusikilizwa nyie mmekuwa tayari na majibu yote. Subirini kesi iishe ndiyo mjue cha kusema, lakini hata hivyo midomo ni mali yenu na mnaweza kusema chochote mnchotaka na kwa vile hakuna anayewajua basi endeleeni kuropoka mjifurahishe mwisho wa siku mtaumbuka

    ReplyDelete
  14. Mambo kama haya yameanza kujitokeza huko Ulaya. Wafanyakazi wa ndani wanagiribiwa na watu wa nje kusudi wabaki huko. Ili iwezekane, anatungiwa
    kesi kama hii na watu. [hasa Wakenya wanawafanyia hivi Watz] ili waonekane wabaya na wawe na kashfa kama hizi. Wapeni tahadhari ndugu zenu.

    Huyu mama tusianze kumuhukumu maana kesi kama hizi zimeongezeka kule. Yawezekana huyu mfanyakazi wamekwisha kuingilia tayari na watu wa naman hii na yeye kwa kutaka kukaa huko ndiyo kaingizwa katika kesi kama hizi.

    Nadhani mama huyu hawezi kuwa na watoto watatu ughaibuni wanatunzwa na Mtz halafu akafanya mambo kama haya. Watoto watakuwa hatarini na kila mtu anajua hilo. Mungu amsaidie yabainike wazi.

    ReplyDelete
  15. Jamani tunapoangalia shilingi siku zote tunatakiwa kuangalia pande zote mbili. Huyu binti ni tamaa ya kupata maisha ya juu na wala hajateswa kama wengi tunavyoona hapo. kwanza ni ndugu ndugu kabisa na Rebecca Balira. Hii imekuja baada ya kwamba binti hataki kurudi kwao Africa baada ya Rebecca kumaliza PHD yake, kisha ona maisha ya UK ndo bora sasa anamkomesha cousin sister wake ambae amemtoa kuona dunia. Sasa haya ndo shukrani za mwanadamu. Tujifunze jamani, binadamu sie hatubebeki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...