Hussein Zulfiqar (kushoto) mwanafunzi bora wa March 2011. Wengine ni wale waliopata alama zaidi ya 70 – Erick Mtewelle, Jeniffer Ukwuoma, Adam Abdallah na Diwani Mwamengo. Mwenye T-shirt nyeupe ni Moiz Salemwalla Mkurugenzi wa IIT.
CHUO cha Kimataifa cha Technologia ya Habari cha Institute for Information Technology - IIT, kimetoa zawadi ya tuzo ya kimataifa kwa mwanafunzi bora Hussein Zulfikar baada ya kufanya vizuri katika mtihani wake mwaka huu na kushinda wenzake zaidi ya 1,000 kutoka visiwa vya Carribean na barani Afrika.
Mkurugenzi wa Mipango wa IIT, Bw. Moiz Salemwalla alikabidhi tuzo kwa kufaulu vizuri Stashahada ya Kimataifa ya Mawasiliano na Komputa alisema mwanafunzi huyo aliwashinda wenzake baada ya kufualu vizuri kufikia kupita wote kutoka vyuo 37 vilivyoko katika nchi 13 tofauti.
Bw. Salemwalla alisema mwanachuo huyo ameungana na wenzake wanne waliofanya vizuri katika mafunzo ya mawasiliano na komputa yanayotolewa na chuo hicho kufikia mwezi Machi mwaka huu.
Alisema chuo hicho ambacho kimeidhinishwa na Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE)na kutoa mafunzo ya Mawasiliano na Komputa kilitoa tuzo kwa wanafunzi Jenifer Ukwuoma, Erick Mtewele, Diwani Mwamengo na Adam Abdallah.
Ofisa Mkuu wa chuo hicho, Bw. Mohammed Yusufali alisema chuo hicho ambacho hutoa wahitimu zaidi ya 200 kwa mwaka hutoa mafunzo hayo kushirikiana na Uingereza pia kimetoa ofa ya punguzo ya ada kwa wanachuo hao.
Alisema chuo hicho hutoa cheti cha kimataifa cha komputa, hutoa stashahada ya kimataifa,shahada na Uzamili na stashahada ya Biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...