Sendeu
Rage
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepeleka mashtaka mbele ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu. 
 
Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine iliiagiza Sekretarieti kupeleka mashtaka hayo kutokana na kauli za viongozi hao kabla ya mechi ya Yanga na Simba iliyochezwa Agosti 17 mwaka huu.
 
Rage alikaririwa na vyombo vya habari kuwa Simba haitapeleka timu uwanjani kama mchezaji wake Gervais Kago kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati hataruhusiwa kucheza, na kuwa ofisa mmoja wa TFF ndiye kikwazo kwa uhamisho wa mchezaji huyo.
 
Naye Sendeu kupitia vyombo vya habari alikaririwa kuwa Yanga haitaingiza timu uwanjani hadi itakapolipwa sh. milioni 16 inazoidai TFF ingawa deni hilo halikuwa na uhusiano na mechi hiyo ya Ngao ya Jamii.
 
Kauli hizo si tu zililenga kuvuruga mechi hiyo kwa kuwachanganya mashabiki, bali zilikuwa za kudhalilisha mchezo wa mpira wa miguu nchini.
 
Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi inayoongozwa na Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) mstaafu Alfred Tibaigana itakuwa na kikao Agosti 28 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine itajadili mashtaka dhidi ya viongozi hao.
 
Imetolewa na Boniface Wambura
Ofisa habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni kweli TFF ilitaka kuihujumu Simba kama Rage asingekuja juu. Kama walimruhusu Asamoh kuichezea Yanga wakati wa mchezo wa hisani mwaka jana bila kukamilisha usajili kwa nini hawakufanya hivyo kwa Simba hadi Rage atishie? na wanatangaza hayo zikiwa zimebaki siku tatu tu kabla ya mchezo ili kuivuruga Simba! hata kazi Rage aliyoifanya ya kuhakikisha Kago anapata ITC na kuruhusiwa katika ligi ilitakiwa kufanywa na TFF kwa hiyo maofisa wa kamati za TFF ndio wanatakiwa kushitakiwa.Lazima TFF wajue kwamba hawawezi kuaminiwa na Simba kwa kuwa itikadi yao wote inajulikana lazima kila maamuzi yao yatiliwe mashaka hadi yafafanuliwe.

    ReplyDelete
  2. nguo hizo hizo kila siku simba wewe ubunge wewe kweli africa njaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...