AFISA MDHAMINI WIZARA YA BIASHARA VIWANDA NA MASOKO BW. HEMED SULEIMAN ALI AMEWATAKA WAKULIMA WA ZAO LA KARAFUU KUUZA ZAO HILO KATIKA SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA ZSTC NA KUACHA TABIA YA KUWAUZIA WATU MITAANI.


AMESEMA CHOMBO AMBACHO KIMERUHUSIWA KUNUNUA KARAFUU NI ZSTC PEKEE PAMOJA NA KUWA KUMEJITOKEZA BAADHI YA WANANCHI KUPITA MITAANI KUNUNUA KINYUME CHA SHERIA JAMBO AMBALO LINAWAKOSESHA MAPATO WAKULIMA.


AKIZUNGUMZA NA WAKULIMA WA ZAO HILO WA WILAYA YA MKOANI KWENYE UKUMBI WA UMOJA NI NGUVU AMEFAHAMISHA KUWA SERIKALI INAFANYA KILA JUHUDI KUONGEZA BEI YAKARAFUU PAMOJA NA KUWASOGEZEA VITUO VYA UNUNUZI KARIBU NA WANANCHI ILI KUWAONDOSHEA USUMBUFU.


NAYE MKUU WA WILAYA YA MKOANI BW. JAKU HAMIS MBWANA AMEWASISITIZA WAKULIMA HAO KUENDELEA KUITUNZA NA KUITHAMINI MIKARAFUU KWA FAIDA YAO NA TAIFA KWA UJUMLA.


AMESEMA SERIKALI ITAHAKIKISHA KUWA INACHUKUA HATUA ZA KUWAFIKIA WAKULIMA WA ZAO HILO ILI KUONA MWENENDO MZIMA WA UCHUMAJI NA UUZAJI UNAVYOENDELEA.


NAO WAWAKULIMA HAO WAMEIOMBA SERIKALI KUREJESHA HUDUMA ZA ULIPAJI KWA ANAYEANGUKA WAKATI WA UCHUMAJI WA ZAO HILO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...