Mgeni rasmi,Muwakilishi Mkurugenzi wa UNAID-Tanzania,Dr.Jean-Luc akisoma hotuba yake mapema leo kwenye viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar,wakati wa maadhimisho ya tamasha la vijana la Kimataifa Duniani,ambapo kauli mbiu yake ni "Majadiliano na Maelewano miongoni mwetu".
 Ofisa habari wa Umoja wa Mataifa-Tanzania (UNIC),Bi Stella Vuzo akipeana mkono na Mgeni rasmi,Muwakilishi Mkurugenzi wa UNAID-Tanzania,Dr.Jean-Luc mara baada ya kusoma hotuba yake kwa vijana waliofika kwenye tamasha la vijana la Kimataifa Duniani.
Ofisa Habari kutoka Umoja wa Mataifa-Tanzania (UNIC),Bi.Stella Vuzo akizungumza mbele ya mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tamasha la maadhimisho ya siku ya Vijana ya Kimataifa Duniani,lililofanyika leo kwenye viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar,aidha Bi.Stella pia aliwashukuru watu wote waliohudhuria tamasha hilo la Vijana.
 Muwasilisha Mada kwenye tamasha hilo la maadhimisho ya siku ya Vijana ya Kimataifa Duniani,ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji kutoka taasisi ya TYC ( Tanzania Youth Coalition),Bwa. Humphrey Pole Pole,akizungumza mbele ya mgeni rasmi pamoja na wegeni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tamasha hilo la Vijana,ambapo mambo kadha kadha yalizungumzwa kwa ajili ya Vijana.
Mwakilishi kutoka shirika lisilo la Kiserikali,HAKI ELIMU,Bwa.Elisante Gedion akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi,hotuba hiyo ambayo ililenga katika mazingira ya vijana na suala la ajira kwa upana wake na pia namna ya kujikwamua katika lindi la umaskini kama vijana kwa namna moja ama nyingine ,aidha Bwa.Gedion katika hotuba yake pia alisisitiza kuwa vijana wanapaswa washirikishwe kwenye ujasiliamali ili waweze kupambana na lindi la umaskini badala ya kujiingiza kwenye vitendo viovu.
Ofisa habari wa Umoja wa Mataifa-Tanzania (UNIC),Bi Stella Vuzo (mwenye kofia) akiwa pamoja na Mgeni rasmi,Muwakilishi Mkurugenzi wa UNAID-Tanzania,Dr.Jean-Luc wakipewa melezo mafupi kwenye moja ya maonyesho ya vitabu mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar wakati tamasha la vijana la Kimataifa Duniani likiendelea.
 Baadhi ya vijana mbalimbali walioshiriki kikamilifu katika kuandaa tamasha hilo la maadhimisho ya siku ya Vijana ya Kimataifa Duniani kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar.
 Baadhi ya Wanafunzi wakisikiliza na kufutilia kwa makini mambo kadha wa kadha yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo mapema leo,wakati wa maadhimisho ya siku ya Vijana ya Kimataifa Duniani
 Baadhi ya Vijana kutoka sehemu mbalimbali pia walifika kusikiliza mada zilizotolewa na wahusika kwenye maadhimisho hayo adhimu kwa Vijana Duniani kote.
baadhi ya Wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari waliokutana mapema leo kwenye viwanja vya Biafra katika kuadhimisha siku ya Vijana ya Kimataifa Duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...