Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (wa pili) akiwa miongoni mwa maspika wa mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya wa Madola (CPA) Kanda ya Afrika wikiingia kwenye ukumbi wa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 13 wa Maspika na Wenyeviti wa Bunge mjini Lilongwe, Malawi leo. Mkutano huo umefunguliwa na Rais wa Malawi leo Mhe. Bingu wa Mutharika na utaisha tarehe 14 Agosti 2011.
Spika Makinda (wa pili kushoto) akifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyojikita kwenye kuimarisha umoja na mshikamano ili kuliondoa bara la Afrika katika umaskini uliokithiri. Kulia ni Spika wa Sierra Leone na kushoto no Spika wa Zambia.
Ujumbe wa Maafisa kutoka Bunge la Tanzania
Rais Bingu wa Mutharika akipokea heshima kabla hajauhutubia mkutano huo uliohudhuriwa na nchi zote kumi na tisa za Afrika za Jumuiya ya Madola (ambazo ni Tanzania, Afrika Kusini, Malawi, Kenya, Botswana, Cameroon, Rwanda, Uganda, Zambia, Namibia na Zimbabwe. Nyingine ni Seychelles, Swaziland, Gambia, Ghana, Lesotho, Mauritius, Sierra Leone, Nigeria na Msumbiji).
Katibu Msaidizi wa CPA Kanda ya Afrika (wa pili shoto) Bw. Demetrius Mgalami kutoka Tanzania. |
Spika Makinda (wa kwanza kulia waliokaa) kwenye picha ya pamoja ya Maspika na Wenyeviti wa Bunge. Katikati mwenye fimbo ni Ngwazi Profesa Bingu wa Mutharika, Rais wa Jamhuri ya Malawi.
Picha zote na mdau Prosper Minja wa Bunge
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...