Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Jeshi la Polisi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuanza uchunguzi dhidi ya wanaotuhumiwa kulihujumu Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).
Amesema uchunguzi huo utaiwezesha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kufanya kazi yake. Waziri mkuu amesema uchunguzi uangalie utaratibu uliotumika katika uuzaji UDA.
Waziri Mkuu Pinda alitoa maelekeo hayo jana, alipotoa taarifa ya serikali ya kuiongezea fedha Wizara ya Uchukuzi kwa matumizi ya mwaka wa fedha 2011/2012.
Bila kueleza muda maalumu wa uchunguzi huo, Waziri Mkuu Pinda alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kusikiliza vilio vya wabunge kuhusu suala hilo, ambalo linagusa hisia na maslahi ya wananchi, hususan wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kutokana na hali iliyojitokeza bungeni kuhusu uuzwaji wa shirika hilo, serikali imeona ni vyema vyombo vyake vikachunguza jambo hilo. Pinda alisema baada ya uchunguzi kukamilika, serikali itachukua hatua kwa wote waliohusika katika uuzaji UDA kwa kufuata sheria na taratibu za nchi. “Tumeagiza CAG, TAKUKURU na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuanza uchunguzi wa jambo hili, utakapokamilika tutatoa taarifa na kuchukua uamuzi wa kisheria kwa wahusika,” alisema.
Waliwahusisha Meya wa Jiji wa Dar es Salaam, Dk. Didas Massaburi, mbunge wa Kaliua, Profesa Juma Kapuya (CCM), anayedaiwa kuwa na hisa 10,000 katika kampuni ya Simon Group iliyonunua UDA na aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya awamu ya tatu, Idd Simba, ambaye anadaiwa kuingiza fedha kwenye akaunti yake na nyingine ya asasi ya Pride.
Wabunge kutoka mkoa wa Dar es Salaam, wakizugumza na waandishi wa habari jana, walisema Dk. Massaburi, Mkurugenzi wa Jiji, Bakari Kingobi na watendaji wengine waliohusika na kadhia hiyo wasimamishwe kazi.
Kwa mujibu wa wabunge hao, hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya Simba, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, wajumbe wa bodi na watendaji wa shirika hilo waliohusika na kashfa hiyo. Mwenyekiti wa wabunge hao, Abass Mtemvu, alisema wanataka mkataba wa uuzaji UDA usitishwe. Alisema Dk. Massaburi na Kingobi walishiriki kikao batili kilichoitwa mkutano maalumu wa wanahisa wa UDA na kufanya uamuzi wa kukabidhi shirika la mali zake kwa Simon Group Limited.
Alisema kikao hicho kilichoitishwa na meya kilifanyika bila kuheshimu maelekezo ya barua ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya Februari 28, mwaka huu, yenye Kumb. Na. CAB. 185/295/01/27 iliyoagiza kusitisha mchakato wa kuuza hisa ambazo hazijagawiwa.
Nakala ya barua hiyo iliwasilishwa kwa Kingobi, meneja mkuu wa UDA, na wizara nyingine husika. Mtemvu alisema mkutano huo ulitanguliwa na kikao batili cha bodi ya wakurugenzi ya UDA, chini ya uenyekiti wa Simba, kilichofanyika Januari 28, mwaka huu, kilichoazimia kuuza hisa zisizogawiwa kwa Simon Group bila kuzingatia taratibu, kanuni na sheria.
Alisema Serikali itoe tamko kutokana na mgogoro wa kimaslahi ulioelezwa kuhusu kamati ndogo ya Bunge iliyoundwa na Kamati ya Miundombinu, kutokana na kutozingatiwa Kanuni za Bunge katika kutoa majukumu kwa kamati husika kuhusu kashfa ya UDA.
Miongoni mwa wajumbe ni Profesa Kapuya. Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni Mtemvu (Temeke – CCM), Mussa Zungu (Ilala - CCM), Iddi Azzan (Kinondoni - CCM), John Mnyika (Ubungo - CHADEMA), Halima Mdee (Kawe – CHADEMA), Dk. Faustine Ndungulile (Kigamboni –CCM), Eugene Mwaiposa (Ukonga – CCM), Dk. Makongoro Mahanga (Segerea –CCM). Wengine kupitia Viti Maalumu ni Zarina Madabida (CCM), Philipa Mturano (CHADEMA), Mariam Kisangi (CCM), Angellah Kairuki (CCM) na Dk. Fenella Mukangara (CCM).
Katika hatua nyingine, waziri mkuu alisema serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha wastaafu na wanaodai pensheni katika Shirika la TAZARA wanalipwa. Alisema hatua zimeanza kuchukuliwa ili kuhakikisha wastaafu hao kwa upande wa Tanzania, wanalipwa.
Waziri mkuu alitoa maagizo hayo siku moja baada ya wabunge kulalamikia kuuzwa UDA.
dawa iliyokuwa jikoni sasa imechemka inaweza gawiwa haya mmoja mmoja pata kidonge mpaka gamba litoke
ReplyDeleteAisee hii kali sasa, hivi UDA bado iko hai jamani ? Naomba mnifafanulie wadau wenzangu. Mimi nilidhani hili shirika lilikuwa limeshakufa zamaniii...Sasa sijuwi na Bayankata nayo ipo ?
ReplyDeleteYOTE TISA....KUMI HILO BASI BAYANKATA LEYLAND ALBION...
ReplyDeleteTunataka pia ukaguzi katika uuzaji wa Kiwira coal mine, NBC, Nyumba za serikali, TTCL/CELTEL, Mtibwa Sugar, mahoteli nk!
ReplyDeleteAnkal, umenikumbusha mbali sana, mabasi hayo yalikuwa na ruti ndefu sana mfano Shule ya Uhuru hadi Kongowe, likijaa mpaka mlangoni, tena mmebanana ile mbaya. Lakini bado nauli utataoa tu. Konda mbabe na hana muda wa kupoteza. Wakati huo nasoma Tambaza na kukaa Kurasini. Wadau wa Tambaza, 1979-1982 na wa njia ya Kilwa Road mnakumbuka mabasi haya?
ReplyDeleteYalikuwa mabasi imara sana na pia ilikuwepo huduma ya kulipa kabla kwa mwezi, kwenye basi unaingia na kadi yako tu.
Leo UDA haipo kabisa, imeuzwa kwa WAJANJA.
Takokuru hawafanyi kazi hadi waagizwe na Mizengwe??
ReplyDeleteHAO WABUNGE WATATU WA MWANZO NI AIBU TUPU KWENYE TAIFA WOTE NDIO WANASAMBAZA AIBU YA KUTEKETEZA VIJANA SASA BANIA COMMENT. MIE NINGEPENDA WACHUNGUZWE KAZI ZAO.
ReplyDeleteKaka hili bus umenikumbusha mbali sana enzi za Leyland Albion.
ReplyDeleteHayo mengine yalikuwa semi-automatic yana ki-gia kidogocha kupachika kwenye mapengo mapengo hivi.
Huyo wa Tambaza ni nani huyo nami nimesoma hapo Tambaza 1979 - 1982 Mwalimi wangu wa Darsa alikuwa Madam Msuya na wa Biology Mwalimu Busyanya.
Ni aibu sana mashirika kama UDA,NHC,Madini,Tanesco yanashindwaje kazi wakati palikuwa hakuna hata mshindani?Hawa wa NHC nyumba wamepewa toka serikalini baada ya kutaifishwa kutoka kwa wamiliki ,hivyo hawakuwa na gharama yoyote ya uanzishwaji wa shirika(Capital=zero) na kuna msururu wa wapangaji wanasubiria hizi nyumba lakini ufanisi =zero,na hawa UDA wapo funded na serikali palikuwa hakuna hata daladala ni wao tu,unashindwaje kuendeleza biashara isiyokuwa na mshindani????? this is a win win situation na hakuna gharama za kufanya matangazo ya biashara ktk haya mashirika.
ReplyDelete