Mkaguziwa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Bw Juma Kwame akieleza mambo muhimu kuhusu CHF,kwa waandishi wa Habari ili kutoa ufahamu kuhusiana na mfuko huo unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Kanda ya Kusini,Beatus Chijumba akitoa taarifa ya utekelezaji ya Mfuko huo kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa Waandishi wa Habari.
 waandishi wakipewa vikasha vya taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Mfuko wa bima ya Afya.

Na Abdulaziz Video

Watoa huduma za Afya zikiwemo zahanati na Hospital za wilaya zimetakiwa kuhakikisha wana jamii wengi wanajiunga na Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) ili kuweza kukusanya fedha nyingi zitakazosaidia kuboresha huduma za Afya vijijini.

Hatua hiyo imekiwa ikiwa na Lengo la kuhakikisha kuwa huduma za bima ya afya (NHIF/CHF) zinawafikia wananchi walio wengi na kuongeza asilimia ya wanachama kutoka 7.7% (2010) hadi 30% ifikapo 2015 (Ilani ya uchaguzi wa CCM 2010, sura ya 6, kifungu cha 36(f) Hayo yalielezwa na Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya,Kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara,Bw Beatus Chijumba alipokuwa akitoa maelezo mafupi kwa waandishi habari waliokuwa ktk semina ya siku moja ya mashirikiano baina ya anahabari na mfuko huo.

Hatua hiyo imefikiwa Kwa kuzingatia changamoto zilizojitokeza kwa kipindi tangu kuanzishwa kwake,Ambapo Mfuko huo una malengo ya kuongeza uwigo wa wanachama,kuboresha zaidi mafao kwa wanachama,kuhakikisha kuwa watoa huduma wanatoa huduma zilizo bora zaidi hasa kwa wale wanachama wanaoishi vijijini.

Aidha Bw Chijumba ameitaja wilaya ya LIWALE kuwa ni wilaya pekee kati ya wilaya zote za mkoa wa Lindi ambayo imenufaika na Ruzuku ya Tele kwa Tele inayotolewa na serikali kupitia uchangiaji wa mfuko wa Afya ya Jami(CHF).

Ambapo wilaya hiyo ilafanikiwa kuchangisha jumla ya Milioni 16 na kufanikiwa kuongezwa na serikali zingine Milioni 16 na kuwa na Milioni 32 zilizoweza kusaidia Uboreshaji wa Huduma ikiwemo
upatikanaji wa Dawa na vifaa tiba Semina hiyo ya siku moja imefanyika katikaukumbi wa jengo la Posta,Manispaa ya Mtwara na kuhudhuriwa na waandishi wa Vyombo mbalimbali toka Mkoa wa Lindi na Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...