Daraja la Kisiwani Kojani Pemba ambalo wananchi wa kisiwa hicho wameahidi kumuadabisha Mbunge wao kutokana na kushindwa kuchangia ujenzi wa daraja hilo(Picha na Idara ya habari Maelezo Zanzibar)
NA FAKI MJAKA-MAELEZO ZANZIBAR
WANANCHI wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba,wamedhamiria
Kumtia adabu Mbunge wa Jimbo hilo,Rashid Ali Omar(CUF) kwa kile walichodai kuwafanyia kitendo cha udhalilishaji.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya wenzake,mmoja wa viongozi wa kamati ya Maendeleo ya Jimbo hilo,Shaame Omar Rohostoki,wamekula kiapo kufanya hivyo kutokana na kuwafanyai kitendo hicho.
“Wallahi laadhim Mbunge wetu ambae tumemchagua ametufanyia kitendo sio kizuri cha kutudhalilisha,hivyo na sisi hatukubali tuko tayari kwa lolote ili na sisi tumtie adabu,”alisema Rohostoki
Akielezea chanzo cha tukio hilo Rohostoki ambae ni mmoja wa wanaojinadi kufanya tukio alisema walimfuata mbunge huyo ili awasaidie kuendeleza ujenzi wa daraja ambalo wanajenga ambapo mbunge huyo alidai kuwa hawezi kutoa msaada bila ya kujionea ujenzi wenyewe.
Rohostoki alisema baada ya Mbunge huyo kufika kujionea ujenzi aliwapongeza kwa juhudi walizozifanya na kuwataka wamfuate nyumbani kwake Kiungoni ili akawapatie msaada wa Makalbi ambayo yangehitimisha ujenzi huo.
Aidha Rohostoki alisema akiwa ameongozana na kamati ya watu wawili wa maendeleo ya Jimbo hilo, walifika nyumbani kwa Mbunge huyo kwa lengo la kwenda kupatiwa msaada huo.
Alisema mara baada ya kufika kwa ujumbe huo nyumbani kwa Mbunge huyo walimkuta akizungumza na simu huku akilalamika kuwa Makalbi hayapo sehemu husika wala hakuna njia ya kuyapata kwani yameisha.
“Tuliongoza mimi na wenzangu wawili amabo ni wajumbe wa kamati ya maendeleo ya Jimbo letu,na mara baada ya kufika tukamkuta Mbunge anazungumza na simu akilalamika baada ya kuambiwa makalbi yamekwisha,”alisem Rohostoki..
Mara baada ya kupata majibu hayo Mbunge huyo alimpa simu Rohostoki ili kuthibitisha kwamba makalbi hayo yamekwisha,jambo ambalo alilosema kuwa sio kweli.
Aidha Rohostoki alisema wakiwa wanaondoka nyumbani kwa Mbunge huyo walipita sehemu ambayo yanauzwa makalbu hayo na kuyakuta yanauzwa kama kawaida na muuzaji hakufanya mazungumzo na Mbunge huyo.
Hivyo kitendo hicho Rohostoki na wana kamati wenzake wamekiita kuwa ni cha udhalilishaji kwao,hivyo wamedhamiria kulipiza kisasi kwa Mbunge huyo,atakapofika katika eneo lao.
“Kitendo alichotufanyia Mbunge huyo ni cha udhalilishaji,kwa hiyo ikiwa sisi ndio tuliomchagua na ameweza kutufanyia kitendo sio cha kiungwana,tunaahidi tutamuonesha,”alieleza.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,kwa njia ya simu Mbunge huyo ambae bado yuko Bungeni Dodoma katika kikao cha Bajeti,amekiri kuwepo kwa tukio hilo.
Amesema kuwa kilichopelekea kutoke kwa hitilafu hiyo ni kutokana na daraja hilo ambalo ndio chanzo cha mgogoro huo halikuwepo katika mradi wa maendeleo ya Jimbo.
Amesema mbali na hayo pia walimlazimisha kufanya jambo ambalo katika kipindi hicho hakuwa na uwezo nalo kulifanya.
Hivyo Mbunge huyo amesema kuwa yeye hakuona kuwa ni jambo kubwa na lakutisha,hivyo aliweka taarifa katika ngazi za Jimbo,lakini amesema kutokana na hali hiyo kuwa kila siku inaendelea kuwa mbaya na kufikia mpaka katika vyombo vya habari ataweka taarifa katika vyombo husika kwa ajili ya usalama wake.
Hivyo Mbunge huyo amesema kuwa yeye hakuona kuwa ni jambo kubwa na lakutisha,hivyo aliweka taarifa katika ngazi za Jimbo,lakini amesema kutokana na hali hiyo kuwa kila siku inaendelea kuwa mbaya na kufikia mpaka katika vyombo vya habari ataweka taarifa katika vyombo husika kwa ajili ya usalama wake.
“Hapo mwanzo ndugu mwandishi niliona ni jambo la kawaida ambapo niliweza kupeleka taarifa katika ngazi za Jimbo,lakini kutokana na haya yamezidi kuwa makubwa itanilazimu kuweka taarifa zaidi kwa vyombo husika vya sheria kwa ajili ya usalama wangu,”alisema Mbunge huyo.


Sasa mhe. Mbunge hadi ukawapeleka wajumbe wa kamati nyumbani kwako..ulidhani hao ni watoto wadogo? Kwa nini hukuwaeleza wazi kuwa mpango wa kujenga daraja haukuwa kwenye bajeti kwa wakati ule? Au hujui taratibu za bajeti? Ulifikiri utatoa fedha mfukoni? Danganya toto...kalagabaho!!
ReplyDeleteyakhe, mtoeni busha tu aangaike nalo, tuone kama na Dodoma ataenda tena.
ReplyDeleteHivi nyinyi Wabunge munadhani mutaendelea kudanganya wananchi mpaka lini?
ReplyDeleteSiku hivi watu wamesoma, wanawasiliana na wenzao kwa mitandao hivyo kuwadanganya watu wazima musifanye kwani mambo hayo yamepitwa na wakati.
Mapesa yote hayo munayopata ya maendeleo ya jimbo munadhani ni ya kwenu?