Na Tiganya Vincent- MAELEZO,Dodoma.

Jumla ya wanachama 7,000 wameandikishwa kujiunga na Mfuko wa Akiba wa Wafanyakazi wa Serikali mara baada ya uzinduzi mpango wa hiari mwaka 2010.

Hatua hiyo imetokana na Serikali kupitia Wizara ya Kazi na Ajira kupitisha Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya 2003 ambayo inaitaka mifuko ya hifadhi ya Jamii kupanua wigo wa wanachama wake ili kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wengi.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Ofisa Uendeshaji wa Mfuko wa Akiba wa Wafanyakazi Serikali kwenye banda la Wizara ya Fedha Charles Komba wakati wa maonyesho ya wakulima ya nane nane ambayo yanafanyika kitaifa mjini Dodoma.

Alisema kuwa lengo la mfuko huo pia ni kuwafikia wazalishaji binafsi ambao hawachangi katika mifuko ya pesheni kutokana na ajira zao na wale wanaochangia mifuko mingine lakini wanahitaji kujiwekea akiba zaidi.

Komba aliongeza kuwa nia ya mpango huo ni kuwasaidia wananchi kujihakikishia kipato zaidi na kujikinga na majanga mbalimbali pindi uwezo wa wanachama kufanyakazi unapopungua.

Alisema kuwa chini ya mpango huu umekusudia kuwasaidia watanzania wote wenye uwezo wa kufanyakazi na wenye kipato kwa kuwapa huduma ya hifadhi kwa ajili ya manufaa ya uzeeni.

Komba alitaja baadhi ya walengwa kuwa ni pamoja na wafanyabiashara ndogondogo ili kuwajengea uwezo wa kujikinga na matatizo yanayotokana na umri mkubwa, kupoteza kipato , kuumia kazini au kufariki.

Alieeleza kuwa mtanzania yoyote anaweza kujiunga na mpango wa hiari wa mfuko wa GEPF ili mradi awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi 60 na awe na kazi inayompatia kipato halali.

Komba alisema kuwa mwanachama atakayejiunga baada ya kutimiza miaka 55 au zaidi atapaswa kuamua kipindi ambacho anakusudia kujiwekea akiba.

Alisema kuwa mwanachama afungwi kila mwezi bali ni kila anapopata fedha kulingana na kipato chake na kuongeza kuwa fomu za kujiunga na unachama ni bure.

Mpango wa Hiari ulizinduliwa mwaka 2010 na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Ali Mohamedi Sheni.



Serikali kupitia Wizara ya Kazi na Ajira iliandaa Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003 pamoja na Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi za Jamii ya mwaka 2008 iliimiza kupanua kwa wigo wa wanachma wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii iliyopo ili kuwafika watu wote wenye uwezo wa kuzalisha kipato.



Hadi hivi sasa Tanzania inayo mifuko ya Hifadhi ya Jamii ifuatayo Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF); Mfuko wa hifadhi za jamii (PSPF), Mfuko wa hifadhi za jamii (PPF) Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mfuko wa Akiba wa Watumishi wa Serikali (GEPF) Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF)na Mfuko wa Hifahi ya Jamii Zanzibar-ZSSF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...