DAR EXPRESS YATOA HUDUMA CHAFU, SUMATRA LIANGALIENI NA HILI

Habari za kazi wadau wa Globu ya Jamii
Kwanza natoa pongeza zangu sana kwa kazi kubwa unayofanya ya kutuhabarisha, kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza.
Siku ya jumapili asubuhi tarehe 20/08/2011, nilikuwa nawasafirsha ndugu zangu wawili kuelekea mkoa wa Arusha kupitia basi laDar Express lilikiwa na registration no. T 367 ARH, departure time ya basi ilikuwa ni saa 12:00 asubuhi ambalo linaondokea pale shekilango au urafiki kama wengi tulivyozoea kupaita, nilikata tiketi 2 ambayo thamani yake ni shs 25,000/= kwa kila moja, wakati tunapandisha mizigo kwenye buti ya gari alitokea kijana mmoja ni KONDA  wa basi na kusema kwamba unatakiwa kulipia mizigo, kwa taratibu kabisa nilimuuliza kwa nini? akasema mizigo hiyo ni mingi, nikamwambia kuwa huwezi kupima mizigo kwa macho, mizigo inapimwa na mizani na uniambie ni uzito wa kg ngapi abiria anapokata basi ndio anapewa free na baada ya kuoneka abiria amezidisha mizigo basi ndipo mtapiga mahesbu kutokana na kg ambazo zimezidi halafu alipie, lakini yule kijana alikuja juu sana nakusema haiwezeani inabidi ulipie ndio kuna kaka mmoja akanishauri nimuone supervisor wao kwa jina ni Mzee Mosha, kama sijakosea nilimfuata supervisor na kumuomba twende naye aone ile mizigo na kwa makubaliano ya kupima ndio naweza kulipia, yule supervisor alikwenda kuona na kusema kuwa hakuna neno rudisha mizigo kwenye basi then safari ianze, lakini kondacta wa lile basi ambaye sikuweza kupata jina lake alitoa kauli cahafu sana na kumwambia yule supervisor kuwa wewe ni supervisor mpaka kwenye buti na kutoa maneno ya kashfa sana, ndipo supervisor akaamuru gari liondoke baada ya mizigo ya abiria wangu kurudishwa kwenye gari. Baada ya basi uondoka niliwasikia dada mmoja na kaka mmoja nao pia wakilalamika kuwa nao pia wamepata matatizo kama yangu baada yakuambiwa alipie godoro dogo la mwanafunzi, kwa bahati nzuri wao walikuwa wanafahamiana na mtoto mwenye kampuni ya mabasi wakamipigia simu na kufika pale ndio akaweza kupakia.
Nakumbuka haya mabasi yalisababisha ajali kipindi fulani hivi na watu waikuwa wanayaogopa na watu kuwaita chinja chinja, lakini walijitahidi na huduma nzuri mpaka wananchi wakasahau yale machungu ya ndugu zao ufariki katika ajalli, sasa je Yule mtanzamnia mabaye hamjui mtoto wa basi atasaidiwa na nani???? Ombi langu kwa SUMATRA ni lazima tiketi za abiria ziandikwe free kilogram ambazo abiria anazipata kutokana na tiketi na kila basi wawe na mizani kwa ajili ya kupima uzito ili mzigo utakapozidi ndio alipie. Na hii itamsaidia abiria kuwa makini na mizigo yake kwani anajua kilo zake ni kiasi gani.
Mmiliki wa basi la Dar Express
Kwa sasa hivi customer service ambayo wateja tulikuwa tumezoea hakuna, ili naomba ilifanyie kazi, kwa kuna uonekano wa KONDA kutaka kijipatia pesa zaidi. Fanya uchunguzi nah ii zaidi ya mara mbili nimepanda basi ambali konda ni huyo huyo niliyemuona juzi ana kauli chafu sana ni kijana mbaye hafai kabisa kutoa huduma kama hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Afadhali kuna mtu kajitolea kuongea same this happened to me in Moshi January nilipokuwa naelekea Dar konda anadai nilipie mzigo.Mizigo nimepanda nayo ndege same luggages hamna extra cost leo nilipie zaidi eti DAR EXPRESS.Sasa mimi mbaya zaidi mhudumu yule dada (i wish i got her name) kanikalia kooni anataka nimpe kidogo.Mpaka tumefika Dar ananiambia usiponipa napeleka mizigo ofisini kwetu, mizigo ishafika nikamwambia wapeleka ofisini ikafanye nini?

    Well hiyo hela alikuwa anaomba nilikuwa nayo na nisingeshindwa kutoa ila ilikuwa ni ulaghai plus walikuwa na jazba.Mi naona somebody need to address hili basi hata ukitumiwa hela through them wanakuzungusha sana kama hawataki kukupa vile.Nilimtumia hela mama yangu ilibidi aende na polisi ndo akapewa hela

    ReplyDelete
  2. Hayeni wazee wa DAR-EXPRESS....Investment yenu siyo ya kitoto...pesa ya kutisha mmeiwekeza...then mnaajiri VICHAA bila even a basic training ya CUSTOMER CARE.........wake up you guys!

    ReplyDelete
  3. yaani nyie ni bora sana magari yenu huko mi nikienda moshi na arusha naona raha kwa habari ya mizigo jamani magari yetu sisi huku wasafiri wa lindi na mtwara ni kero tupu maana hata begi lako la nguo km auwezi kuongea basi imekula kwako hata laptop tu wanatoza kwakweli kwa sasa tufanye km ndege tu kwamba mwisho ni kilo fulani na ziandikwe kwenye tiketi na pia gharama ya kuzidi iwekwe hili mtu ukitaka kusafiri either upime mwenyewe au basi liwe na mzani wake itakua bora sana na mimi nasema kuwa SUMATRA na CHAMA CHA ABIRIA sijui wenyewe wanajiitaje mi sijui naomba hiki kitu ianze mara moja maana otherwise munaleta usumbufu mkubwa sana kwa abiria

    ReplyDelete
  4. hata mm yalinitokea juzi nilivyo kuwa natoka moshi lakini sikulipa nilikataaa katakataa na nikaambiwa nipandee ivyoo ivyooo

    ReplyDelete
  5. Sekta nzima ya usafiri wa mabasi imeoza kuanzia ilipoanza, haijawahi kuwa sawa. Tatizo KUU la Tanzania ni UONGOZI na USIMAMIZI, haya mawili ndio chanzo cha kila shida utakayokumbana nayo au hata kuifikiria tu. Huko vijijini ndio usiseme, wanateswa balaa. Siku moja nilikuwa natoka Magu kuelekea Mwanza mjini, nilipanda 'haisi.' Kuna kina mama wawili walipanda 'haisi' ikiwa imeshajaa 'levo siti' hivyo ikawalazimu kusimama. Tukiwa njiani kukawa na jamaa kama 6 hivi wakasimamisha gari. Bahati mbaya nafasi iliwatosha wanne tu, jamaa wakasema 'haisi' iendoke tu maana hawawezi kusafiri kwa mafungu mafungu. Konda kuona atakosa hela nyingi akawaamuru wale kina mama wawili wateremke ili awachukue wale jamaa wote. Cha ajabu, pengine kwa vile walikaripiwa, wale kina mama wakaanza kushuka kweli! Sikuamini, ndipo mimi na abiria wenzangu tukagoma wasishushwe vinginevyo konda na dereva wake wangeumia vibaya. Tulimaanisha kweli kweli. Baada ya mzozo wa kama dakika 3 hivi ikashindikana kuwashusha na tukaendelea na safari. Watu wengi sana wanakumbwa na matatizo safarini. Nchi zilizoendelea napo yapo yapo, ila si mengi wala si makubwa kama Tanzania. Huku wanajitahidi sana katika UONGOZI na USIMAMIZI (ikiwa ni pamoja na kuweka kila kitu wazi wazi), suala si kuwa na viongozi peke yake.

    Poleni sana wasafiri wote nyumbani Tanzania.

    ReplyDelete
  6. Mdau- SUMATRAAugust 27, 2011

    Poleni sana wadau, kilo za abiria kusafiri nazo bila kulipia ni kilo 20, na ili kuhakiki kama zimezidi ni lazima zipimwe kwa mzani na sio macho. Mmiliki wa Dar exp. ni mstaarabu sana na tayari nimewasilina nae.

    SUMATRA kwa upande wetu tunalifuatilia kwa umakini suala hili

    Mdau kutoka SUMATRA

    ReplyDelete
  7. Ni kweli kabisa mdau usemayo hawa wahudumu wa haya mabasi wana kauli mbaya sana mtu unapo kubali kulipa 25,000/- au 28,000/- ina maana hutaki usumbufu lakini huwezi amini mimi nilikuwa natoka Arusha tarehe 27/5/2011, dereva alikuwa anaendesha gari vibaya mno hadi mama 1 akashuka baada ya yule mama kushuka yule dereva akasema abiria wa Dar ni sawa na kima hivi kweli unaweza kumwita binadamu mwenzio kima wakati analipa nauli, tena kwa jeuri hawa kima tu hakuna wa kunibabaisha, hiyo kauli ikawa suppot na wahudumu, tatizo nililoliona ni kupeana kazi kwa kujuana hata kama hujui kusoma huna customer care ilihali wote kabila moja mtoto wa mjomba mtoto wa shangazi nakushukuru mdau kwa kuliona hili tabia za hawa wahudumu zina kera sana

    ReplyDelete
  8. Pole sana Ndugu. Hayo yalishawahi kunipata miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa hilo basi sithubutu kupanda wala kumpandisha ndugu yangu. Huwa nalitazama nasema "Ondoka Mwalimu".....!!

    Kuna kondakta wake alishawahi kunikashfu ( majibu mabaya mbele ya abiria wenzangu na wanangu wawili) Oh! God forbid. Nilijisikia vibaya sana na niliona safari yote chungu mpaka nafiki Arusha. Nilitamani hata niwe na namba ya mjukuu wa mwenye gari lakini haikuwa hivyo. SUMATRA TUNAOMBA MUANGALIE SWALA ZIMA LA UONGOZI WA HIYO KAMPUNI. mmasai wa loliondo.

    ReplyDelete
  9. WE MDAU WA SUMATRA ACHA USANII!

    Tunahitaji taarifa rasmi,kutoka SUMATRA sio kutuzingua! Tutajuaje kama we ni huyo konda umejita mdau wa SUMATRA?

    TZ usanii kila mahali, mashirika mengine ni kula kulala tu, nadhani EAC itatuamsha uzembe mwingi!

    Abiria na wananchi inabidi tuwe na sauti kama mwenzetu, sio ndio mzee kila kitu.

    ReplyDelete
  10. Kwa Msaada zaidi Number za Mwenye magari ni hizii Mr Judica Mremi 0718 403181 or 0784 276060, Ninaco kijua mimi kwa sasa Tokea Kifocha mukewake Mambo yana Yumba kwakiasi na aameamua Kuachia Madaraka Kwa Company nyingine.

    ReplyDelete
  11. Jamani mdau uliyeleta hii post kweli nimefurahi sana, jamani kondakta wote wa haya magari wanakauli chafu sana hawana Customer care yoyote, unauliza kitu kwa wema lakini wanakujibu vibaya sana hii mm ilinitokea mwezi wa saba mwishoni unamuuliza jambo anajibu vibaya sana.
    Ushauri
    Ni vyema hao makondakta wote wapewe namba au majina yao yaandikwe kwenye masharti wanayovaa ili kuweza kuwatambua majina yao na pia kuwe na namba ambayo itaweza kuwasiliana na mkuu wao moja kwa moja.

    ReplyDelete
  12. mdau kutoka SUMATRA weka jina lako unaogopa nini katika kutimiza wajibu wako? nao si sehemu ya wajibu wako kuelezea wasifu wa mmiliki

    ReplyDelete
  13. Afadhali kasema mdau wa Mtwara. Hali ni mbaya zaidi ingawa kuna nafuu ukilingalisha na miaka mitatu nilipokuwa nafika kwa mara yakwanza. Yaani ilikuwa mzigo ukiingia kwenye buti tu unatakiwa uulipie hata kama ni begi dogo ambalo umelazimika kuliweka kwenye buti kwa kuwa sehemu ya ndani ya kuwekea mizigo imejaa. SUMATRA WEKENI UTARATIBU WA KIKOMO CHA UZITO WA MIZIGO ANAOTAKIWA ABIRIA WA BASI KUSAFIRI NAO BURE.

    ReplyDelete
  14. DAR EXPRESS zamani bwana , siku hizi sijui wameajiri wavuta bange? tena hasa huyo konda aliyetajwa humu ndani ndio zake ana kauli chafu sana kazi kuharibu mood za watu. wakati alipoenda kuomba kazi alienda kainamisha kichwa chini sasa anajifanya mbabe na kutoa kauli mbofumbofu. nunua mbasi yako na sio kuaribu biashara za watu!

    ReplyDelete
  15. Poleni wadau, lakini kubase kwenye uzito wa mzigo tu haitoshi. Ujazo pia lazima uzingatiwe. Vinginevyo tutakuwa na watu wanaosafirisha marobota ya pamba kwenye basi.

    ReplyDelete
  16. Mbona hili suala mnafanya siri? Pamoja na kusafiri kwangu kwa basi muda mrefu kwenye route hiyo leo ndio najua kwamba limit ya mzigo ni 20kg. Kwa ninyi SUMATRA kufanya hili suala ni siri na kutoweka sheria kwa wamiliki kupima mizigo kunafanya ninyi mbebe lawama kwa kiasi kikubwa kuliko hata wao wamiliki wa mabasi.

    ReplyDelete
  17. Asante sana Mdau wa Sumatra, nimeipenda taarifa yako. Msaidie huyo Bwana mana investment yake ni kubwa sana. Mimi pia niliwahi kupanda Dar Express one day. Wakawa wanatukataza kufungua vioo lakini AC yenyewe wanawasha na kuzima, basi ilikuwa joto mtindo mmoja. Abiria walilalamika sana siku ile lakini wahudumu wa basi waliweka masikio pamba mpaka tukafika Dar kutoka Arusha tukiwa tumechoka sana mana hakukuwa na hewa ya kutosha kwenye basi. Ni basi zuri sana, lakini usimamizi wa huduma bado ni duni. Mshauri aajiri professionals asiogope kuwalipa fedha kubwa mana in the long term itanusuru biashara yake.

    ReplyDelete
  18. Kwakweli Kero za usafiri Tanzania zimepita mpaka kwani si haki kwa mtanzania wa kawaida. Nakummbuka Januari mwaka huu mimi na ndugu yangu tulienda Mbeya kwenye graduation kwa kutumia Upendo Express safari ya kwenda na kurudi na tulikumbwa na similar matatizo kama wadau hapo juu.

    Wakati wa kwenda hakukuwa na matatizo yoyote as hatukuwa na mizigo isipokuwa rough za hapa na pale tukiwa barabarani. Matatizo yalikuwa wakati wa kurudi. As tulikuwa 2 so tulitegemea kuwa na mzigo ya kilo 40 ingemaanisha hatutoilipia, lakini tuliambiwa mizigo lazima ilipiwe na receipt wakatupatia ila wakati tuko njiani tumeshaondoka wakasema kuwa mizigo mingine wameipakia gari yao ingine ambayo ingefika Dar same time as tulikuwa tunaongozana wakati wa kuondoka. Sababu ya kupakia hiyo mizigo gari ingine ni kuwa hiyo ambayo tumepanda ilizidi kilo, ila njiani waliendelea kupakia mizigo na abiria wapya (uongo namba 1). Tumefika ubungo ile gari ilishafika terminal na kuondoka, so kwenda ofisini wakasema hawana msaada twende yard, ambayo sikuwa naijua. Baadaye wakasema tupige simu kufatilia mizigo, as tulikuwa tumechoka tukakubaliana na huo upuuzi. Kesho yake tunapiga simu kumbe walitupatia namba ya mlinzi wa hiyo yard.

    Cutting story short, ingawa tulilipia kuepuka usumbufu mizigo ikapotea na hakukuwa na msaada as hawana ofisi ubungo ila kuna kachumba ambako ni shared for different buses. Na wanaokaa kwenye ofisi ni matapeli tu kwani hawana msaada kwa abiria

    ReplyDelete
  19. TZ bado biashara tunafanya kama wakati wa Mwalimu. Sera ya wafanyabiashara wakati wa Mwalimu ilikuwa "Mkopo kesho" na "Kiuzwacho Hakirejeshwi"!!!

    ReplyDelete
  20. "MZALENDO" uliyeandika/julisha habari hii tunakushukuru na tunaomba wadau wengi "WAZALENDO" watujulishe mambo kama haya "MENGI KATIKA JAMII" ambayo ni kero kwa wananchi tuyafuatilie.(VIONGOZI WETU HAWAJIBIKI IPASAVYO)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...