Askari Polisi wakimdhibiti kijana  ambaye alifanya fujo kwa kupiga mawe vioo vya benki ya CRDB tawi la Azikiwe, Posta Mpya, Dar es Salaam jana na kusababisha wateja na wananchi kukimbia ovyo. (PICHA ZOTE NA KASSIM MBAROUK)
wewe unajifanya fara sio, basi mimi ni fara zaidi...

Kaa chini...arrraaaaah!
Na Kamanda Mwaikenda
TAFRANI kubwa ilitokea jana katika Benki ya CRDB, tawi la Azikiwe, baada ya kijana mmoja aliyehisiwa kuwa jambazi kurusha mawe kwenye vioo vya benki hiyo na kusababisha wateja kukimbia ovyo wakidhani wamevamiwa.


Tukio hilo lilitokea jana mchana, ambapo kijana huyo anayedhaniwa kuwa akili yake imeathirika kwa kubuia dawa la kulevya 'Teja' kurusha mawe kuelekeza kwenye jengo hilo na kuvunja vioo.


Baadhi ya wateja walianza kutimua mbio kutoka nje huku wengine wakilala chini kuhofia maisha yao.Baada ya kuona hivyo, Polisi waliokuwa kwenye lindo la benki hiyo, walifyatua risasi juu wakidhani majambazi wamevamia benki hiyo. Lakini baada ya muda walimuona kijana huyo aliyekuwa katikati a Barabara ya Azikiwe karibu na kituo cha Daladala cha Posta Mpya, akiendelea kurusha mawe.
Polisi walimuendea na kufanikiwa kumdhibiti na kuanza kumpatia mkong'oto wa nguvu, huku wanachi wenye hasira wakitaka nao waruhusiwe kumwadhibu.


Ndani ya benki hiyo hali ilikuwa shaghalabaghala, kwani mitungi ya maua na baadhi ya nyaraka zilitawanyika ovyo, huku wakioneakana baadhi ya wateja wakiwa wamezirai na wengine wakilia baada ya kupotelewa na nyaraka muhimu za benki vikiwemo kadi na fedha taslimu.


Wakati tukio hilo ilitokea, pia hali haikuwa nzuri kwa wafanyakazi wa benki hiyo, kwani baadhi walisikika kuwa walipatwa na hofu kubwa kiasi cha baadhi yao kukimbilia kujificha vyooni na kuacha kaunta zao. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Duuh! kweli sisi watanzania inabidi tuitunze amani kwa nguvu zetu zote, kama mawe tu yanawatawanya raia, sijui ingekuwaje ingekuwa ni risasi au bomu! mtu kazirai kusikia sauti ya jiwe lililotua kwenye kioo, mshindo wa bomu si ndio tunampoteza kabisa? TUITUNZE AMANI JAMANI, MIKIKIMIKIKI YA DARFUR HATUIWEZI.

    ReplyDelete
  2. Ubinadam unatakiwa jamani huyu mtu ni mgonjwa kwanini apigwe kiasi hichi hata huyo muuwaji alieuwa watu wengi huko Norway na hakupigwa hata kofi kwanini waafrica tuko zaidi ya wanyama hamna huruma hata kidogo?hata kutumia common sense inashindikana kazi kuoneana tuu tizama wanawake wamejaa wakiaangali wallah ingekuwa wazungu wangekuwa wakilia kumlilia huyo kijana..jaribu kufikilia angekuwa nduguyako ungejisikiaje?

    ReplyDelete
  3. sioni sababu ya mtu kama huyo umeshamkamata na anatii amri zote unazomwambia halafu ikawa bado huyo askari na buduki ikawa anampiga MATEKE, lazima tukumbuke kuwa kupiga ni udhaifu fulani

    na huyo kijana hata kama yuko na makosa si tayari mumeshamkamata sasa kwanini wanaanza kumuhukumu kumpiga mateke na kumuumiza
    kweli tanzania au bara la afrika kwa ujumla tuko nyuma sana katujui nini tunakifanya kwa raia wetu

    haya mimi yangu macho

    ReplyDelete
  4. ...Ni maoni yangu fikiria kama kijana huyo angekufa hapo hapo kwa kupigwa teke na huyo askari kungekuwa na utetezi gani hapo ?Anger management kwa askari inahitajika.

    kama angekufa isingukuwa excessive force halafu polisi wangeanza kulalamika wanonewa? lakini kumbe ni utendaji wao wa kazi mbovu.

    Hili tukio ambalo picha inaongea uhalisi wake.je kusingekuwa na picha ukweli huu unajificha.Polisi wetu badilikeni jamani.


    halafu uthibiti wa bunduki hapo ni hovyo,hovyo,hovyo hovyo kabisa.Askari wetu bwan.Oneni wenyewe.Huyo kijana inavyoonyesha alishakamtwa au kudhibitiwa miteke ya nini ?????

    ReplyDelete
  5. blackvirusAugust 04, 2011

    kaka nathani hiyo picha ya mwisho ni mbaya sana kwa jeshi letu kwani ni brutal use of force and assault on an unarmed victim (mualifu asie na silaa)-- inaonesha kabisa askari polisi wa kikosi cha FFU akimpiga mtu teke na yeye akiwa na silaa ambayo pia kwa muudo wake na alivo ishik ni hatari kwa civilians/pedestrians na viumbe hai vilivyopo karibu na tukio pia inaweza ikatumika thidi ya jeshi hilo na wilaya kama sijakosea kama tunafata haki za kibinadamu --- jeshi linatakiwa liwe na mbinu za kutuliza gasia na waaalifu bila kutumia nguvu wana kipigo kama hapo wako maaskari watatu wanamtuliza mtu mmoja kweli ????? hawa wako serious kweli ???!!

    ReplyDelete
  6. Kwa nini kumpiga!!? Si wangemkamata tuu na kuacha sheria ichukue mkondo wake? Sasa kama kweli huyo kijana ana matatizo ya akili, si askari watakua wamemuonea?

    ReplyDelete
  7. Yaani kama kichaa anapigwa namna hii !!! Kazi ipo!!

    ReplyDelete
  8. Afande anafanya kazi yake ipasavyo lakini ameshindwa kupewa elimu bora jinsi gani ya kuweza ku deal na watuhumiwa wenye kuvuja damu kama huyu ili kujikinga na maradhi thakili ya ukimwi

    ReplyDelete
  9. Naungana na wengi waliotangulia huu ni UKATILI NA UONEVU NA UMBUMBUMBU wa Askari wetu.

    Hata kama huyo mtu ametishia amani, ni wapi sheria na kanuni zimeeleza kuwa Askari aangushe kipigo namna hiyo ...! Hayo maaskari ni makatili na wengi wao wako hivyo kwasababu ya frastuation za maisha yao...!! Kumbukeni huyo ni Binadamu na ninyi ni Binadamu..hujafa hujaumbuka.Unajua kuwa na wewe kesho unaweza lipuka kichaa ??! mtu yeyote anafanya kitu kutokana na msukumo fulani..wangetafuta solution kwanza kabla ya kumuumiza hivyo..! hajaumiza mtu wala kuua why treated him like that?! ASKARI wa BONGO WOTE NIM.**&.CKERS***.SIIPENDI NCHI HII ILA BASI TU NDIYO NCHI YANGU..MIJITU HAINA UBINADAMU..ETI WANAFANYA KAZI ZAO..!LOL SHAME ON YOU.anayezungumza hivyo alilelewa kwenye mazingira ya ukatili na anaendeleza ukatili wake.MKUU WA MAJESHI NA WIZARA HUSIKA WAPENI MAFUNZO NA WAJIFUNZE KWA WINGINE...JE ANGEKUWA NA BASTOLA SI NDIYO WANGEMSHOOT KABISA.??! LOL..AKILI HAMTUMIA HATA BUSARA HAMNA..!!

    ReplyDelete
  10. afande wanatakiwa bado training ya uhakika sijui mwema akiiona hiyo anafurahi?Je fisadi akikamatwa anaweza pigwa hivyo?si kawaida kwa mtu kama huyo aliyekwisha kudhibitiwa kupigwa buti kiasi hicho ELIMU ELIMU ELIMU jamani watanzania.Nadhani jambo la kwanza lingekuwa kumpatia matibabu kwani anaweza poteza uhai kabla ya sheria kumpitia

    ReplyDelete
  11. Na kama ana akili zake timamu na nimesoma kua watu wamepotelewa na fedha na nyaraka za benki basi kuna uwezekano kwamba huyu jamaa hakua peke yake, wenzake waliendelea na wziai wakati watu wakikimbilia maisha yao.

    ReplyDelete
  12. KAZI YA POLISI NI KULINDA USALAMA WA RAIA.. AWE MWEMA AU MHARIFU.
    ASKARI WA AFRICA WANACHOJUA WAO NI KUTUMIA NGUVU KWA KUWA HAWANA AKILI.

    HAKUKUWANA SABABU YA KUMPIGA HUYU KIJANA KWANI HAKUWA NA TISHIO KUBWA ZAIDI YA HILO LA MAWE AMBALO TAYARI WALISHA MDHIBITI.

    ReplyDelete
  13. katika tukiao hilo Polsi ndio wanaonekana ni "wagonjwa wa akili". Kazi yao kubwa katika tukia hili ilikuwa kumpeleka hospitali na simkunyanga kwa kiatu ambacho kimenunuliwa na kodi za wananchi, pengine hata kodi ya huyo mgonjwa! Basi Polisi kitegengo cha Elimu watumie picha au tukio hili kuwafundisha Polisi namna ya kutoa Huduma za Usalama wa raia wote bila ubaguzi.

    ReplyDelete
  14. Wanaoiba mabilioni hawaguswi hata chembe tena wanabembelezwa kujiuzulu na kuwekewa TV gerezani. Ilisemwa rasilimali ya mnyonge ni umoja inabidi sasa watu waamke kwakweli uonevu huu lazima uishe

    ReplyDelete
  15. JAMANI M NAJUA KWENYE BLOG HII KUNA MAWAKILI KIBAO WAKUJITEGEMEA, PIA HATA BABA YANGU MTIKILA HUWA ANAHUDHULIA HUMU, NAOMBENI HUU JAMAA APATE HAKI YAKE KWAKWELI HAMNA SHERIA YA TANZANIA INAYOSEMA MTU ADHIBITIWE KWAKUPIGWA MATEKE NAMNA HII, NA HILI TEKE NDILO LINALOONYESHA LILIMTOA DAMU KWENYE USO NAMNA HIYO PLZ PLZ JAMANI.

    ReplyDelete
  16. Wadau mmesema yote lakini nami naona niseme ili kuongeza uzito. Jamani oneni Norway wamemkamata muuaji wa watu karibu 100 na alikuwa na silahaa je wamempiga hata kibao? Kazi ya polisi ni kupiga kuadhibu au kukamata na kupeleka watu kwenye mkondo wa sheria. Kwa nini lakini polisi wanachukua sheria mikononi? Afu mnakemea raia wanao waua wezi wakati serikali yenyewe ni role model wa uvunjaji wa haki za binadamu. Jamaa ameathirika na madawa ya kulevya ambayo yanawatajirisha vigogo leo hii amekuwa chizi mnamtembezea kichapo badala ya kumsaidia apelekwe hospital. Mwema you need to train your police hii ni kashfa baba.

    ReplyDelete
  17. Jukumu la polisi ni kumlinda huyu wanayemdhania mhalifu, na walichotakiwa kufanya na kumthibiti kwa kumfunga pinga na kumpeleka sehemu ya usalama, si hivyo vipigo wanavyomfanyia.

    Hapa ndipo tunaposhangaa kumshambulia Lema kwamba anachochea wakati hali halisi ndio hiyo hapo.

    ReplyDelete
  18. mimi kwa upande wangu sipindi polisi wanavyochukua sheria mkononi lakini bongo nayo haitabiriki kutokana na maisha magumu naungana na mchangiaji mmoja aliyesema yawezekana huu ulikuwa mpango wa majambazi wengine wameingia ndani wakijifanya wanataka huma za kibenki na mwingine awe nje apige mawe aakti wazimu yote yawezekana ila inatakiwa askari wa tz waelimishwe zaidi hawatumii akili ktk kazi yao wanatumia miguvu ya kijinga na masifa ya kipumbavu

    ReplyDelete
  19. safi sana polisi, fanyeni kazi kama kawaida kuondoa products za kama hizi kwani watu kama hawa ndio majambazi wa kesho. Ukikutana naye kwenye angle zake anakumaliza. Madawa ya kulevya na bangi ndio ndio chanzo cha uchizi wake na baadae ni kibaka au jambazi.

    ReplyDelete
  20. THIS IS POLICE BRUTALITY.........!!!!! These cops should be disciplined. Huyo jamaa hata kama mhalifu ana haki pia.

    ReplyDelete
  21. mnategemea nini huyo ni kijana rinajifanya rinaakiri hiri nitarichanachana wakina chacha tabia zao zinajulikana musoma hiyo. kazi zao upolisi, uanajeshi, na security, na kupenda ndogondogo.

    ReplyDelete
  22. Napenda niwapongeze jamaa wote waliotoa maoni kabla yangu, kwani ni ukweli askari wametumia nguvu visivyo,ni kweli askari wetu wanaitaji mafunzo ya kiubinadamu.

    ReplyDelete
  23. One day matapeli waliopo serikalini na mafisadi watapigwa namna hii.

    ReplyDelete
  24. Jamani tutasema tuu humu kwenye blog jee kuna lolote linatotendeka kuwaelimisha polisi kuhus brutality? kila human being ana right dunia pote wangetia ndani ya gari lao mpaka kituoni wakaacha sheria ichukue madaraka, CHANGE HAS TO HAPPEN SOON IN TZ, WANANCHI CHOKA NA VYOMBO VYA DOLA FAKE HIVI

    ReplyDelete
  25. Kama watu watanzania wameeamka basi wafanye maandamano kupinga POLICE BRUTALITY! Bado na hakuna atakayeandamana ttaishia kuandika kwenye BLOG! Mungu isaidie Tanzania.

    ReplyDelete
  26. Huu kweli ni brutality? Hao askari wanaolinda benki hawajui kama wanachofanya ni makosa..Nategemea kusikia na wenyewe wamechukuliwa hatua.

    ReplyDelete
  27. Hivi mkuu wa Polisi anasema nini akiona vijana wake wana abuse wananchi? I hope atamuwajibisha huyu askari. Inasikitisha jamani kuona unyama kama huu unaendelea karika karne ya 21. Tutafika?

    ReplyDelete
  28. Kwa ubabe huu tutafika? Au polisi alidhani atapata sifa? Kweli haya yanatokea karne ya 21?!!! Tunahitaji mabadiliko ya haraka na itakuwa ni vyema kama mkuu wa polisi kama atatoa mfano na atachukua hatua zinazofaa kuelimisha vijama wake.

    ReplyDelete
  29. Ukiukamata halifu basi mfikishe pahala husika sio kupiga jamaniiiiiiiii alaaaaaaaaaniwe alompiga hivi na watauua aliyevuja vioo na waaachingaaaaaa tu aliyeiba mabilioni analindwaaaaaaaaa mtalaaaaaaaaaniwaaaaaaaaaaaa nalaaaaaaaaaaniiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  30. Hakika ni ukatili mkubwa sana. Sawa ameshakamatwa, angetakiwa kuwa chini ya ulinzi wa polisi akiwa salama, sio akiwa amejeruhiwa namna hiyo. hali aliyo nayo hata akitakiwa kujitetea kwa lolote sina uhakika kama anaweza kuhema na kueleza chochote.

    ReplyDelete
  31. kama polisi wamemshika huyo kijana then wanampiga, hivi wananchi wanaoangalia hilo tukio wakishika mwizi mitaani kwao watawafanyaje.
    PILI: askari wote wanamshambulia kijana wakati wameacha bank bila askari, hivi wana akili hawa.

    ReplyDelete
  32. UKATILI WA POLISI UNAWATISHA RAIA NA KUIDHARAU SHERIA, KUNA HAKI GANI POLISI KUMPIGA MTUHUMIWA? HII NI SHERIA YA WAPI?
    VIONGOZI WANAOHUSIKA WANAFANYA NINI HAKI ZA KIBINADAMU ZINAPOKIUKWA NAMNA HII?
    WABUNGE NANYI MNALIANGALIAJE JAMBO HILI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...