
Wadudu wanaosababisha kuoza kwa meno ni sehemu ya wadudu wakazi kinywani (oral flora). Wadudu hawa hujishikiza kwenye meno na kufanya utando, wana uwezo wa kuchachua vyakula hasa vyenye asili ya sukari na kutoa tindikali. Ni tindikali hii ambayo huvuta madini kwenye meno na kuweka matobo. Utando huu wa wadudu kwenye jino moja unaweza kuwa na wadudu nusu bilioni, miongoni mwao wakiwemo jamii ya mutans streptococci ambao kimsingi ndiyo wasababishaji wakuu wa kuoza kwa meno. Wadudu wengine ni kama Lactobacillus na Actinomy
Jinsi wanavyoambukiza
Ndani ya jamii ya wadudu hawa ziko jamii zingine ndogondogo ambazo zinatofautiana kwa uwezo wa kuchachua vyakula na kutoa tindikali na hata uwezo wa kujishikiza kwenye meno. Kwa mtu mwenye wadudu wasio wakali anaweza kuambukizwa na mwenzake mwenye wadudu wakali na hivyo kuingia kwenye hatari zaidi ya kuoza meno. Tafiti zimeonesha wapenzi/wanandoa wanaweza kuambukizana kwa njia ya kubusiana. Watoto wanaochangia ice cream/ice water mashuleni pia wanaambukizana kwa njia hii. Tafiti pia zimeonesha wazazi wanaotafunia vyakula watoto wao kama sehemu ya kuvilainisha wanaweza kuwambukiza pia watoto wao.
Njia nyingine ni jino lililooza kuambukiza mengine yanayogusana nayo, tindikali inayozalishwa na wadudu katika jino lililooza inaweza kuathiri jino lililo jirani. Ndiyo maana inashauriwa ukiona jino limeanza kuoza muone mtaalamu akalitibu au akaling’oe kama halitibiki ili lisiambukize mengine.
Namna ya kujikinga
Njia nyingine ni jino lililooza kuambukiza mengine yanayogusana nayo, tindikali inayozalishwa na wadudu katika jino lililooza inaweza kuathiri jino lililo jirani. Ndiyo maana inashauriwa ukiona jino limeanza kuoza muone mtaalamu akalitibu au akaling’oe kama halitibiki ili lisiambukize mengine.
Namna ya kujikinga
BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...