Ankal,
Nimesoma barua ya Albino flani na majibu toka kwa Mtanzania juu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru.Napenda mijadala kwa kuwa naamini inajenga ila kwa huu naomba kutoa maangalizo kadhaa.
1-Kwa Albino Fulani na Mtanzania sijui walengwa wa Ujumbe wao ni kina nani kwa sababu kama ni Watanzania basi ingependeza kuonyesha ukomavu na Uzalendo wao kwa Kutumia Lugha ya Taifa yaani Kiswahili.Au labda wamekaa sana huko na kusahau Kiswahili??Lakini sidhani kama hili ni kweli kwa sababu hata hicho kingereza hakijanyooka.Si lengo langu kuanza kuainisha matatizo ya ‘tense’ na ‘grammar’ hapa.
2-Kwa Albino Flani na Mtanzania naomba wakumbuke kuwa Tanzania haijawahi kupata Uhuru na wala haisherehekei Miaka 50 ya Uhuru.Tunachoadhimisha ni Uhuru wa TANGANYIKA na sio TANZANIA.Suala hili nimeliona kwenye barua zao wote wawili hali inayoonyesha kuwa kidogo wameteleza kihistoria.
3-Kwa Albino Flani,mara zote ni Rahisi kukosoa kitu ambacho tayari kipo lakini kukianzisha ni kazi. Nadhani hili lingetoka kama pendekezo na wala sio kama malalamiko na maagizo ya kuwataka viongozi wajihabarishe zaidi na taarifa za Nyumbani.Naamini viongozi walichaguliwa na kupewa dhamana ya kuongoza kwa niaba ya wengi kwa kuwa hamuwezi wote kuwa viongozi kwa wakati mmoja.
Naomba Kuwasilisha
Mdau wa Mayfair


Nafikiri kama ulienda shule hukuelimika. Kwanza soma hiyo barua yako halafu utuambie kuwa ni ujumbe gani ulikusudia kuutoa na kama unadhani huo ujumbe umewafikia walengwa. Barua yako haina muelekeo wala dhumuni na kusababisha confusion tu kwa watu. Kweli "common sense is not common to all"....!! Mdau-NYC, USA
ReplyDeletemdau umenikuna kweli juu ya mada ya hii sherehe ya miaka 50. Nilitaka kutuma maoni yangu lakini nikahsi huenda ankal akaweka kapuni.
ReplyDeleteWatu wengi huwa wanasema sherehe za uhuru wa Tanzania jambo ambalo sio sawa. Kuna sherehe za uhuru wa Tanganyika na kuna sherehe za mapinduzi ya zanzibar. Pia kuna sherehe za muungano. Tanzania haina sherehe za uhuru.
Kwa kweli sikugundua hilo swala la wao kutokutumia Kiswahili
ReplyDeletePili kama babu alitaka achaguliwe yeye kuimba tunaomba atuwie radhi wengine hapa maana kipaji chake sio kivile jamani
Pia hivi vitu vinapangwa muda mrefu, ni kweli wangeweza kukatisha lakini jinsi Albino Fulani alivyoandika ni kama watu wanakurupuka tuuu
Mtanzania sijasoma barua yake nimeona nae ananiyeyusha tuuu
Nimependa barua yako
acheni uswahili , hata ulaya bado mnaleteana swahili na roho za korosho.watanzania kwa nini amuwezi kuishi pamoja ?
ReplyDeleteau mnazani kila mtu sasa kawa mweupe. mtabaki hivyo hivyo na kwenye cycle ya uzungu amuwezi kukaribishwa, bora mjikubali na kushikamana.
peace mdau china
Mdau wa Mayfair, naomba ujifunze ku-ainosha tungo zako.
ReplyDeleteKwa Mdau wa Mayfair:
ReplyDeleteKwanza kabisa kabla sijachangia hoja zako ukizotoa hapo juu, ningependa kwanza nikuelimishe kuhusu hoja yako ya kwanza kabisa ulioitoa kuhusu ujumbe wa Albino Fulani ulikuwa unawalenga wakina nani. Jibu moja fupi tu--ni Watanzania wote ukiwemo wewe. Inasikitisha sana kuwa watu kama wewe kulinganisha kutumia lugha ya Kiingereza na uzalendo. Tanzania kwa taarifa yako inatambua lugha mbili Kiswahili kama na Kiingereza kama foreign language. Kama kweli hukupendezwa na Albino Fulani kutumia wa lugha ya kiingereza kuelezea hisia zake kuhusu DICOTA, basi ni vizuri ukawa mkweli na kuanza kuishambulia serikali yetu kwa kuruhusu lugha ya kiingereza itumike kufundishia masomo kuanzia elimu ya secondary mpaka vyuo vikuu. Wenzetu Warusi, Wachina, Wacuba, nchi zote za Scandnavia zinawafundisha wananchi wao katika lugha zao na si English. Kwa hiyo hapa naona mashambulizi yako kwa Albino Fulani kuhusu utmiaji wa lugha ya kiingereza hayana uzito wowote isipokuwa ni wivu wako tu. Na sioni ulikuwa na haja au sababu gani ya kubeza english yake wakati wewe mwenyewe umetumia lugh ya kiswahili na hukuandika sentensi zilizo nyooka. Kwa sababu naweza kukusahisha sentensi kama nne hivi katika hizo hoja zako hapo juu.
Sasa kwenye mambo ya msingi yaliopelekea wewe kujibu. Kwanza ikumbukwe kwamba Albino Fulani ni mwanamuziki wa kizazi kipya ambaye shughuli zake za muziki anafanyia diaspora na huko nyumbani. Kwa position yake kama mwanamuziki, ana haki hiyo ya kuhoji na kutegemea kupata ufafanuzi ni vipi wanamuziki wa kitanzania katika diaspora hawakuhusishwa. Hilo ni swali zuri kabisa na kwa nafasi yake kama asingeuliza mimi pia nisingemuelewa.
Pili, hapa nimesoma barua yake nzima na sikuona kitu chochote kikubwa ambacho ametoka nje ya mstari huku aki jaribu kuwa vocal kuhusu mambo yanayomgusa yeye moja kwa moja kama mwanamuziki. Katika barua yake unachoweza kuona kama kweli umesoma na kutumia critical thinking analysis, ni kutoridhishwa na zoezi zima lilivyotumika kupata hao watumbuizaji kutoka bongo. Ni kweli kwamba ametumia lugha kali kidogo katika kuelezea kero zake kuhusu DICOTA lakini hakutoka nje ya msitari. Lugha kama hiyo haiepukiki kwa binadamu yeyote aliye/anae kerwa na kitu fulani.
Tatu, nimesoma kwenye majibu yako ukijaribu kutofautisha kuadhimishwa kwa uhuru wa TANGANYIAK v/s TANZANIA. Hii haina point yoyote in the overall issue and frankly you should have not even raised an issue on it. Hii inaonyesha kwamba hukusoma maoni na kero za Albino Fulani kwa kutaka kumuelimisha bali ulikuwa ukidodoza hapa na pale ukijaribu kutafuta makosa--hii ni aibu sana kwako na kwa jinsi ulivyoandika unaelekea kuwa mtu wa makamo na labda kuheshimika kidogo katika society unayoishi. Lakini ulivyokosoa hili kwa kweli heshima yangu kwako iliporomoka ingawa sikufahamu na sijawahi kukutana na wewe.
Mwisho, Ningependa nikuombe Mdau wa Mayfair kwamba siku nyingine jaribu kusoma na ujaribu kumuelewa mwandishi anajaribu kukueleza nini na siyo tu kukaa na kutafuta vimakosa vidogo vidogo hapa na pale wakati haujibu hoja ya msingi inayojadiliwa. Haya si mashambulizi kwako ila nimeona ni kitu ambacho umepungukiwa aidha kwa kujitakia au kwa kuteleza. Nonetheless, nimeona nikuelimishe kidogo.
Hivi unavyofanya wewe ni kujaribu kuziba watu midomo jambo ambalo tulipumbazwa sana enzi za Nyerere. Kwa hiyo nakuomba uangalie picha nzima mtu anapokuja na malalamiko yake na siyo tu kujaribu kumchambua mtu. Unahitaji kuwa na uwezo wa kusikiliza, kusoma, na kufanya tathmini ya jambo kuu linalozungumzwa.
Asante, na kila la kheri.
BS
BS a.k.a albino fulani,
ReplyDeletekila aina ya muziki na mahali pake...bongo fleva za kwako kwa dicota sio mahali pake...sorry. next time tutakufikiria anyway usilielie hapa.
Wandugu, are we serious... Kila mtu anajua post gani ameituma. Kabla huja kosoa post ya mwanzako, kwanza soma post uliyoituma ujicheche mwenyewe. Hii ni aibu.
ReplyDelete