Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evance Balama akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa askari Polisi PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi akitoa heshma za mwisho kwa mwili wa askari Polisi PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi
skari Polisi wakitoa wakitoa heshma za mwisho kwa mwili wa askari mwenzao, PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.Picha Zote na Venance Matinya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ninatoa pole sana kwa Familia ya Marehemu PC Meshack Urasa. Jamani wana jamii wenzangu kutoka mikoa mingine ya Tanzania, kwa imani zenu zozote uombeeni mkoa wa Mbeya. Kama haujawahi kukaa Mbeya unaweza usiilewe nini kinaendelea ndani ya Mkoa huu. Huu mchezo wa kupiga watu nondo ni ushirikina mtupu unao sumbua watu wakiamini eti nondo aliyopigiwa mtu ikitumika kutundikia nyama buchani,basi watu watakuja kununua nyama hiyo kwa wingi.Huu ni Upumbavu wa hali ya juu. Pia natoa wito kwa IGP Said Mwema, mkuu enzi za mzee Augustine Lyatonga Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani uhalifu kama huo haukuwepo kabisa. Hebu waambie vijana wako wafanye kazi bana. Ona sasa Jamaa wamepiga nondo hadi Polisi. Hii si ni kashfa kwenye Jeshi lako? Mimi nadhani ifike mahali huruma huruma hizi tuachane nazo. Mijitu inayo uwa wenzao kwa uhalifu kama huo ikikamatwa, nayenyewe tuyapige nondo hadharani yafe yanajiona.Mbeya kuchuna ngozi,kukata sehemu za siri, mauji ya albino, ajali za ndege, masoko kuungua kiajabu ajabu, ujambazi.Aaah Mbeya imezidi. Halafu nimkoa huohuo ambao nadhani kwa tanzania hii ndiyo kuna makanisa mengi kuliko mikoa mingine.
    JK,Shamsi V.Nahodha, IGP S.Mwema, Viongozi wa dini zote, wanaharakati wote,hebu ingilieni kati matukio haya ya ajabu mkoani Mbeya. Michuzi hii ndiyo Mbeya bana kama utaenda uwemakini.

    ReplyDelete
  2. polisi ni watu wanapaswa kuwa karibu sana na raia kuwa na uhusiano mzuri na raia sio uhasama na raia

    polisi wa bongo hawana uhusiano mzuri na raia yani polisi na raia ni kama paka na chui ndio sababu matukio kama haya hayawezi kuisha kutokana na polisi kutowatendea haki raia...kuwanyanyasa, kuwapa adhabu pasipo na sheria, kuwaomba raia rushwa bila kuzingatia uwezo wa huyo raia,nk

    polisi wanatakiwa kulinda raia na kujali haki za raia bila upendeleo na kuwa karibu na raia kiurafiki ili raia waweze kushirikiana na polisi kikamilifu katika kupambana na mabaya ya uharifu n.k

    leo hii nchi yetu ni wachache sana wanaoweza kushirikiana na polisi katika kupambana na maovu yanayojitokeza hata ikiwa polisi wapo kwenye uchunguzi wa jambo fulani ni vigumu kupata ukweli kutokana na kukosa ushirikiano wa raia wema.

    ni vizuri jeshi la polisi kutoa mafunzo yatakayowezesha polisi kuwa wema kwa raia na kujenga ukaribu na upendo kwa raia kutasaidia sana kupunguza maovu na kupambana na uhalifu kwa umoja wa kushirikiana na raia wema.

    poleni sana familia ya wafiwa na mungu ailaze pema roho ya marehemu
    ameen.

    mdau mahakama kuu ya dunia
    The hague

    ReplyDelete
  3. hao ni CHADEMA tu ndio waleta fujo

    ReplyDelete
  4. Poleni wafiwa, ila tuangalie yanayotendeka? kati ya askari na raia tukipata jibu tutajua chazo cha nauaji ya askari yanasababishwa na nn?

    Mungu ailaze mahali pema pepoa roho ya Bwana Meshak Urasa.

    Bwana alitwaa na Bwana kachukua jina la bwana lihimidiwe Amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...