Baharia Rashid Said Rashid wa meli ya MV Spice Islander, iliyozama na kuua takribani watu 240 huku wengine 619 wakinusurika visiwani Zanzibar juzi, amesema waligawa maboya ya kujiokoa kwa abiria na kuwavalisha watoto kisha kuwaondoa melini kupitia madirishani kabla ya kuzama.
Akizungumza na gazeti NIPASHE akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar, jana, alisema kabla ya meli hiyo iliyokuwa na mabaharia 12 kuzama majira ya saa 7:00 usiku wa Ijumaa iliyopita eneo la Nungwi, waliomba msaada kwa meli nyingine iliyokuwa inapita lakini hawakufanikiwa.
Said ambaye ni mkazi wa Shangani, alisema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya kabla ya meli kupinduka, abiria walimtaka nahodha atoe taarifa kwao kama meli inazama na alifanya hivyo, “Tulijaribu kufanya kila jitihada ili kuokoa hali hiyo, lakini tulishindwa na tukaamua tuiache meli na kuanza kutoka, hapo tena kila mmoja alikwenda kwa upande wake,” alisema.
Hata hivyo, alisema hafahamu kama mabaharia wenzake na nahodha wapo salama au wamekufa kwa sababu mara ya mwisho aliwaona kabla ya chombo kupinduka na kuzama, “Kwa kweli siwezi kusema kama ni uzembe au la umefanyika, lakini wakati inatokea hali hii tulipishana na meli ya MV Jitihada na kuwapa ishara ya kuzama, lakini hawakutusaidia,” alisema baharia huyo.
Alisimulia kuwa walichukua jitihada mbalimbali za kuwapa ishara, lakini hawakufanikiwa na hawezi kusema kama walidharau au hawakuwaelewa walichokuwa wakikitafuta kutoka kwao. [hiyo ni nukuu ya NIPASHE]

Katika mazungumzo yake na MTANZANIA katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, ZanzÃbar jana baharia huyo alisema abiria wengi walikufa kutokana na uzembe.
Baharia huyo aliyelazwa hospitalini hapo, alisema iwapo kama waokoaji wangewasili mapema eneo la tukio baada ya kupata taarifa, abiria wengi wangeokolewa kwa kuwa ulikuwa na sababu za kuwaokoa, ”Ajali ni ajali, lakini kwa hii ya kwetu nasema wengi wamepoteza maisha kwa sababu ya uzembe wa wahusika... “Lakini, hayo tuyaache kwa sababu yameshatokea, nakumbuka wakati tunatoka Dar es Salaam tumbo lilikuwa likiniuma, kwa hiyo, muda mwingi nilikuwa nimelala chumbani kwetu... Ilipotimia kama saa 7.00 usiku, Bubu mmoja ambaye ni mfanyakazi wenzetu alikuja chumbani kwetu na kutuonyesha kwa ishara, kwamba
tutoke nje hali imeharibika, tukamuuliza kuna nini akazidi kutwambia tokeni nje, tulipoona anazidi kutusisitizia tukatoka nje... Nilipofika nje tu, nikakuta maji yameanza kujaa melini, mimi na wenzangu tukaanza kuyatoa kwa ndoo na mashine za pampu.
“Baadaye umeme ukazimika na mashine zikashindwa kufanya kazi. Sasa tukaendelea kuyatoa kwa ndoo, lakini hatukuweza lolote kwa sababu yalikuwa yakiingia kwa kasi sana... Tulipoona hivyo tukaambizana kwamba hali ni mbaya, nikawaambia wenzagu tumwambie kapteni (nahodha) awatangazie abiria. Tulipomwambia kapteni akakubali akatangaza kwamba hali ni mbaya kwa hiyo, abiria wote wawe waangalifu wakati taratibu nyingine zikifuatwa,” alisema Rashid.
Kwa mujibu wa baharia Rashid, baada ya tangazo hilo, abiria walihamaki na kuanza kukimbia ovyo kuokoa maisha yao huku wakipiga kelele za kuomba msaada.
“Tangazo hilo liliwatisha abiria na wakati huo maji yalikuwa yakizidi kuingia ndani, nilipoona hivyo, nikachukua ‘my life jacket’ (makoti ya kuogelea) nikawa nawavisha abiria mmoja baada ya mwingine na kumtupa majini... Nilifanya kazi hiyo kwa muda kidogo, baadaye nilipoona maji yamezidi nikaamua kujitosa baharini baada ya kuvaa life jacket... Nilipojitosa majini, kuna abiria walikuwa wakijirusha majini na kuniangukia, kwa hiyo, nikaamua kulivua lile life jacket ili niwe huru kuongelea na kuwaokoa wengine... Nilipokuwa majini nilishtuka kuona watu wamezagaa majini na wengine wamekufa, kwa hiyo, nilichokuwa nikifanya nilikuwa nikizivua life jacket zilizokuwa katika maiti na kuwavalisha wengine ambao nilikuwa nikiwaweka katika turubai moja ambalo ni maalumu kwa ajili ya uokoaji.
“Wakati nikiwa katika turubai hilo, kuna abiria walikuwa jirani kabisa na mahali ilipokuwa meli, nikawaambia ondokeni hapo, meli itawapindukia, wakabisha na mwishowe kweli iliwafunika kwa sababu wakati nawaambia nilikuwa nikiiona imeshaanza kuegemea upande mmoja,” alisema Rashid na kulengwa na machozi na kuongeza, “Nilipoona wenzangu wamefunikwa, niliumia sana lakini nikasema hiyo ni mipango ya Mungu. Baada ya hatua hiyo nikamuona mzee mmoja akiwa na mtoto wake amembeba mgongoni, akaniomba, akasema mwanangu naomba umuokoe mwanangu, nikakubali, nikamwambia mzee tulia... Nikamchukua yule mtoto nikampeleka katika lile turubai nilikokuwa nimewaweka wengine.

“Nilipomuokoa huyo mtoto, mbele yangu nikaona watu watatu wanalalamika, pembeni kulikuwa na mwanamke mmoja akilia kwa huruma... Nikamfuata huyo mwanamke, nikamkuta na kitu kama mkeka hivi amekishika, nikamwambia achia huo mkeka, akakataa akasema nitakufa, nikamzaba kibao usoni kwa nguvu, akaachia ule mkeka, nikamkamata na kumpeleka kwenye lile turubai... Baadaye nguvu zilianza kuniishia, nikawa nashuhudia kabisa wenzagu waliokuwa pembeni na sisi wakiwa wanapoteza maisha mmoja baada ya mwingine, yaani niliumia sana na nadhani hili tukio litachukua miaka mingi sana kunitoka kichwani.
“Katika lile turubai nilikuwa na abiria kama 15 niliokuwa nimewaokoa, baadaye nikaona wanaanza kuchoka kwa njaa, nikaamua kujitosa tena majini nikaanza kukusanya juice za Azam zilizokuwa zimetapakaa majini... “Nilipopata za kutosha nikaanza kuwanywesha wale abiria wapate nguvu na kila aliyekuwa akinywa fumba moja namkataza namnywesha mwingine,” alisema.
Pamoja na hatari ya kifo aliyokuwa akiiona mbele yake, baharia huyo alisema alikuwa akiwapa moyo wenzake kwa kuwaambia kuwa mahali walipokuwa palikuwa salama na hakukuwa sababu ya kuhofia maisha yao.
“Nilikuwa nawapa matumaini nikawa nawaambia tutapona tu hata kama tutapeperushwa na upepo hadi Tanga au Mombasa, lazima tutaokolewa. Ilipotimia kama saa 12.00 alfajiri, niliona helkopta kwa mbali, nikamwambia mfanyakazi mwenzagu anaitwa Almada, achukue taa moja hivi, akaichukua akainyanyua kuwaonyeshea wale wenye helkopta waweze kutuona, lakini hawakutuona kwa sababu walikuwa mbali ingawa sisi tulikuwa tunaiona hiyo helkopta. Nilipoona hawatuoni, nikamwambia tunyooshe bendera, alipoinyoosha wakati huo helkopta ilikuwa imekaribia ndipo wakatuona na kutufuata huku meli za uokoaji kama Sea Bus na Sea Express zilizokuwa zikiongozana na hiyo helkopta zikatufuata na kutuokoa.
“Lakini, nakwambia kuna uzembe umefanyika… kama waokoaji wangefika mapema watu wasingekufa kwa kiasi hiki kwa sababu baada ya meli kuanza kupoteza mwelekeo, tulipiga simu polisi na bandarini kuomba msaada, lakini hawakufika hadi saa 12.00, sasa hapa tumlaumu nani, serikali au nani? Mungu anajua,’ alisema.
source: NIPASHE“Katika lile turubai nilikuwa na abiria kama 15 niliokuwa nimewaokoa, baadaye nikaona wanaanza kuchoka kwa njaa, nikaamua kujitosa tena majini nikaanza kukusanya juice za Azam zilizokuwa zimetapakaa majini... “Nilipopata za kutosha nikaanza kuwanywesha wale abiria wapate nguvu na kila aliyekuwa akinywa fumba moja namkataza namnywesha mwingine,” alisema.
Pamoja na hatari ya kifo aliyokuwa akiiona mbele yake, baharia huyo alisema alikuwa akiwapa moyo wenzake kwa kuwaambia kuwa mahali walipokuwa palikuwa salama na hakukuwa sababu ya kuhofia maisha yao.
“Nilikuwa nawapa matumaini nikawa nawaambia tutapona tu hata kama tutapeperushwa na upepo hadi Tanga au Mombasa, lazima tutaokolewa. Ilipotimia kama saa 12.00 alfajiri, niliona helkopta kwa mbali, nikamwambia mfanyakazi mwenzagu anaitwa Almada, achukue taa moja hivi, akaichukua akainyanyua kuwaonyeshea wale wenye helkopta waweze kutuona, lakini hawakutuona kwa sababu walikuwa mbali ingawa sisi tulikuwa tunaiona hiyo helkopta. Nilipoona hawatuoni, nikamwambia tunyooshe bendera, alipoinyoosha wakati huo helkopta ilikuwa imekaribia ndipo wakatuona na kutufuata huku meli za uokoaji kama Sea Bus na Sea Express zilizokuwa zikiongozana na hiyo helkopta zikatufuata na kutuokoa.
“Lakini, nakwambia kuna uzembe umefanyika… kama waokoaji wangefika mapema watu wasingekufa kwa kiasi hiki kwa sababu baada ya meli kuanza kupoteza mwelekeo, tulipiga simu polisi na bandarini kuomba msaada, lakini hawakufika hadi saa 12.00, sasa hapa tumlaumu nani, serikali au nani? Mungu anajua,’ alisema.
dah, inauma sana! Polen watanzania wenzangu. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, amen.
ReplyDeleteSitazungumzia Uzembe wa wazi.., ila huyu Baharia Rashid Said Rashid anastahili pongezi sana sana. Anastahili zawadi pia ingawa ni wajibu wake. Hongera sana Rashid Said Rashidi
ReplyDeletepole sana baharia rashid kwa juhudi zako kuokoa wengine. mwenyezi mungu atakulipa na atakulinda siku zote. kwenye ndege kila mtu ana life jacket under his seat sasa sijui kama kwenye hizo meli kama life jackets ziko karibu na abiria. jee abiria hupata briefings kabla ya meli kuondoka bandarini ili wajue cha kufanya kama kukitokea accident. je baharia hupata proper training juu ya kuweza kusaidia abiria in case of accident. hivi hiyo meli ilikua na life rafts za kutosha. hao baharia na watu walikua na simu za kutafuta msaada au vipi. kuna mambo mengi ya kufanya ili next time kusiwe na vifo vingi.
ReplyDeleteThis is very sad. Nafiriki si vema kutafuta wa kumlaumu, ni wakati wa kutafuta sababu za meli kuzama na kufanya maamuzi kutokana na majibu ya utafiti huo. Naomba sana watu wasio na nguvu kimadaraka wasinyanyaswe na kutolewa kafara, ni vema uchunguzi wa kina ufanyike kwanza na haki itendeke.
ReplyDeleteMeli imeanza kuzama saa 1.00 usiku waokoaji wamefika saa 12 asubuhi sehemu ambayo kutoka bandari ya Zanzibar mpka Nungwi ni saa mbili tu kwa Azam Marine!!
ReplyDeleteMimi ni muumini na namwamini Mungu, Nasikitika sana napoona watu wanatumia jina la Mungu katika maswala ya uzembe kama huu, kusema ajali hii ni majaliwa ya Mungu sikubaliani na hili huu ni uzembe wa vyombo vyetu tulivyovikabidhi dhamana ya kuangalia maswala ya usalama wetu, na watu wanaoangalia faida mbele badala ya uhai wa watu.
ReplyDeleteMungu hayupo katika hili Mungu ametupa free willing na ufahamu yaliyo mema na mabaya hivyo ni wajibu wetu sisi kuchambua mambo na kuangalia matokeo yake yatakuwa nini na siyo kufanya uzembe na kusema matokeo yake ni Mungu ndio amepanga.
SMZ inawawekea sheria kali wenye vimashua vya kusafirishia watalii kuwa lazima wawe na "life jacket" sasa hawa wenye meli "life jacket" zipo kumi!!
ReplyDeleteOOOh my it's like I'm reading the novel story but it's reality. May the Lord bless you brother for the kindness heart.
ReplyDeleteHuyu jamaa ni Hero. Sidhani kama kuzama kwa meli ni uzembe wake. Hii ni culuture ya uzembe kutoka serikalini mpaka kwa wamiliki wa meli. Kama meli imezama kwa ajili ya kuzidi uzito ni kwa sababu watu hawafuati sheria za usalama za baharini na serikali ambayo inweka hizi sheria hazifuatiliwi ili mradi tu kila mtu kula kwanza mambo mengine baadaye, na haya ndiyo matokeo yake. Mungu waweke mahala peponi wote waiotutangulia na ajali hii.
ReplyDeleteNimesoma hii habari,pia nilimsikiliza mtu mmoja kati ya watu waliokolewa kama sikosea anaitwa bw mbezi,du kwakweli niliumia sana,nahisi kama nasoma kitabu lakini nikifikiria kumbe ni kweli yametokea,mie naona uzembe upo mkubwa sana mana watu walipiga hadi simu ya bure ya police lakini haikuwa na majibu yoyote sasa kuna haja gani ya kutoa namba ya simu?bwana mbezi alisimulia waliokolewa saa mbili asubuhi toka saa saba kweli hii ni haki?na anasema elkopta mbili zilipita lakini hazikumuokoa!poleni sana watanzania wenzangu
ReplyDeletepole sana rashid, na mungu akubariki na akuondolee hiyo memory isikukae kichwani kwa muda mrefu, nasikitika jinsi hii serikali yetu walivyokuwa wazembe kila janga likitokea uwa awawajibiki ipasavyo kuokoa watu mapema si mara ya kwanza hata kwa MV BUKOBA ilikuwa hivyo! mi nashangaa sana ukipanda panton kwenda kigamboni kuna Tv lakini utakuta ni matangazo ya biashara tu, wakati ukienda mombasa kwenye panton Tv saa zote zinakuwa zina kipindi cha kufundisha abiria jinsi ya kujiokoa, kama vile njinsi ya kutumia maboya, kuvaa life jacket, na ni sehemu gani ukae salama na sikae sehemu gani sisizo salama, sasa bila kuwafundisha wananchi watajuaje jinsi ya kujiokoa? ni uzembe wa hali ya juu na hapa ni serikali ya kulaumiwa na si mtu wala shirika lolote maana vyote hivyo vipo chini ya serikali na kunasheria ya vyombo vya majini na nchi kavu, nani wajibu wa serikali kuhakikisha zinafuatwa la sivyo hatua zichukulie kwa yeyeyote anayezivunja kabla ya hatari! Na hii iwe ni mara ya mwisho hatutaki wananchi tumechoka tunapoteza ndugu zetu kwa uzembe wa serikali! na kubaki kumtupia lawama MUNGU! heti mipango ya MUNGU!,MUNGU ametuumba kwa mapenzi yake na apendi kutuona tukipata shida au mateso, Mateso ni kazi ya shetani ambaye aliwaingia hao wafanyakazi wa hiyo meli wakajaza watu na mizigo kwa tamaa zao, ambazo ni kinyume na mipango ya MWENYEZI MUNGU!!
ReplyDeleteHuyu baharia hakika anaijua kazi yake na ana moyo wa huruma maana sio kila mtu mwenye dhamana ya kuangalia usalama wa abiria kwenye chombo kama hicho anaweza kuwasaidia watu kiasi hicho.
ReplyDeleteZile sheria za usalama wa abiria ndani ya ndege ni muhimu zikasisitizwa nazo kwenye vyombo vingine vya usafiri.
Mungu azilaze roho za marehemu wote wa ajali ya hii mahala pema peponi, Amin.
Poleni sana ndugu zangu nawaombea kwa mungu awajalie amani na subira katika wakati huu mgumu,ombi kwa wahusika idara husika ingawa ajali haina kinga lakini ingelikuwa kuna life jackets za kutosha na ukaguzi wa upakiaji wa abiria na mizigo kuzingatiwa na fikiri maafa yasingalikuwa kiasi hiki jamani tunaomba mjitahidi kufanya na kutimiza wajibu wenu katika kunusuru maisha yetu na ya mali zetu.
ReplyDeletePole baharia Rashid,Mungu atakulipa kwa msaada wako mkubwa uliouonesha!
ReplyDeleteTumepata habari za kusikitisha kutoka kwa baadhi ya abiria kuhusu kitondo cha mabaharia kukiacha chombo kwa kutumia boti maalum za kuokolea maisha na kuwaacha abiria wakifa maji. Lakini kwa habari hii ka ni ya kweli kama Rashid alivyo eleza nampa big up sana. Mungu atakulipa ujira mnono kwa jitihada zako.
ReplyDeletehabari hizi zimeniliza kama mtoto mdogo nalia na nchi yangu mabayo hata mtu akivamiwa na majambazi au moto kuwaka kwenye nyumba yake basi hakuna hatua za haraka zinazoweza kuchukuliwa maana hata ukitoa taarifa polisi hawafiki kwa muda unaotakiwa nasikitika sana natamani ningekuwa na uwezo nichukue robo ya wananchi na kuwahamishia nchi zenye kujali haki za binadamu naoa kama serikali yetu haijali kabisa raia wake
ReplyDeletewapi tulipo na wapi tunapotoka na wapi tunapoelekea tanzania tanzania tanzania kwanini unatutesa kwanini hutujali kwanini walalahoi tunakufa kama kuku kutokana hatuna uwezo wa kumiliki vyombo binafsi na wala hatuna vyombo vya serikali vya kutusaidia kimaisha
ewe mola mwenyezi warudishie roho za upendo na imani viongozi wetu wajali raia wake wasijali maisha yao na familia zao pekeyao
ewe mola mwenyezi wajaalie viongozi wetu wawe na upeo wa kuona mbali wasiwe kama mazombi tu hayajui yanaongoza nini yapoyapo just kujaza matumbo yao
ewe mola mwenyezi jaalia viongozi mafisadi wanaojaza matumbo bila kujali vilio vyetu watoke panya kwenye matumbo yao wakifa wafe vifo vya kinyama
uchungu uchungu uchungu nalia mwenzenu mama yangu amenitoka na mama mdogo pia wote wamenitoka kwenye ajali hii mama yangu sitokusahau na sitochoka kukuombea
mpotelewa na mama zangu wawili mama mzazi na mama mdogo.
Poleni sana watanzania wenzangu Mungu awape moyo wa uvumilivu katika hili.Naomba serikali isimamie sheria ilizoweka kuepusha janga kama hili kujirudia.
ReplyDeleteMungu akubariki bwana Rashid Said Rashid, umejitahidiMungu akubariki bwana Rashid Said Rashid, umejitahidi
ReplyDeletejamani jamani,poleni sana watanzania wenzangu,kweli hii habari inasikitisha sana,yaani nimetiririka machozi sana,maana watu waliteseka muda mrefu bila msaada mpaka kufa.so sad!Mungu akulinde na akutunze rashidi kweli mgepatikana watano kama wewe kwenye hiyo meli naamini watu wasingekufa wengi hivi.nawalilia watanzania wenzangu waliokufa kwakukosa msaada mapema.serikali wanajisahau kama jukumu lao ni kulinda wananchi,sio kukaa tu maofisini.
ReplyDeleteMungu awalaze ndugu zetumahali pema peponi.
We talk of heroes for our country and talk of freedom fighters as our heroes.. Rashid Said Rashid is a national and international HERO to me and we should recognize him as so and not expect the Government to do the same...!!! Rashid Said Rashid, you are my HERO.
ReplyDeleteNIMESOMA HABARI HII MACHOZI INANITIRIRIKA HAKIKA HATA KAMA UNAROHO NGUMU NAMNA GANI LAZIMA KWA HABARI HII UTALIA TU HII HABARI IMENILIZA KAMA ILE ILIYOANDIKWA KTK GAZETI LA MWANANCHI KUNAKIJA ALIKUWA ANAELEZEA FAMILIA YA WATU 36 WAKIWEPO WANAHARUSI AMBAO NI FAMILIA MOJA WAMEFARIKI WOTE WAKBAKI 4 ALISEMA WAKATI MAJI YAMEANZAKUJAA KTK MELI YEYE ALIKUWA ANATEREMKA CHINI KUWANUNULIA CHAKULA WANAHARUSI ANASEMA WATUWALIKUWA WENGI WANAKANYAGANA ALIPOONA HALI INAZIDIKUWA MBAYA ALIWAATARIFU HIYO FAMILIA WAKAKUSANYIKA WAKANZA KUSALI PAMOJA WAKASALI WAKASEMA HALI NI MBAYA KILA MTU AJIOKOE KIVYAKE AKASEMA KAMA HATUJAONANA DUNIANI TUTAONANA MBINGUNI YAANI NIMESOMA HIYO HABARI NILILIA SANA TU POLE WAFIWA NA WATANZANIA WOOTE KWA UJUMLA
ReplyDeletePole sana baharia ulikuwa na wakati mgumu, roho inauma.Ila mungu atakulipa
ReplyDeleteasante ankali kwa kujali maumivu yangu na kuniwekea kilio changu hapa maana naumia sana ankali mama na mama mdogo jamani wameenda
ReplyDeletePole sana bwana Rashid Saia Rashid.Mungu baba akupe baraka katika maisha yako.Sasa ni kweli serikali yatu imeonyesha uzembe mkubwa katika kuwaokoa ndugu zetu waliopata ajali hii, maana walipata taarifa mapema sana kabla meli haijazama na baada ya meli kuzama lakini kama kawaida ya kutojali hawakuchukua jitihada za haraka kama nchi nyingine zinavyofanya.Mimi nadhani serikali ingetumia jeshi la majini (NEVI),Boti za watu binafsi,mashua na mitumbwi na hata kuomba msaada w nchi za jirani waje haraka kusaidia huo usiku kuliko kukaa kimya hadi asubuhi kama ilivyotokea. Kweli inauma sana kupoteza watu wengi kwa uzembe harafu tunasingizia eti ni mipango ya Mungu.Kungekuwa na mtoto wa mkubwa juhudi za haraka zingefanyika. Tupendane jamani.
ReplyDeleteDuh!! inasisimua hii habari kama picha fulani hivi, lkn juu ya yote hongera baharia Rashid mola akuzidishie kwa hao uliowaokoa.
ReplyDeleteAnonymous uliyepotelewa na mama zako pole sana, Mungu akupe nguvu wewe na familia yako
ReplyDeleteni sawa baharia lakini wakati wa kupanda meli kuna watu waliomba kutoka kwa nini mliiondosha ngazi mbio mbio mkasema wanataka kuhatarisha maisha.
ReplyDeleteKwanza Mwenyezi Mungu Inshallah awaweke mahala pema peponi marehemu ameen, Pili awape moyo wasubra wafiwa wote katika kipindi hichi kigumu. tatu hongera ndugu Rashid kwa jitihada zako mwenyezi mungu ndie atakayekulipa. nachangia maoni hayo na kumuunga mkono ndugu Rashid kwamba ajali ingawa ni mipango ya Mwenyezi mungu lakini hii inaonyesha moja kwa moja ni uzembe wa Nahodha na maofisa wake .naeleza hivi ni kama historia inajirudia kwani mimi yameshanikuta (kuzama na meli) tulizama na meli(cargo ship) 1/07/90 na kuokolewa 07/07/90 wakati tukitoka Iran tukielekea Singapore tukiwa mabaharia 21 kati yao watanzania 4 na wengine mataifa mengine .kwa uwezo wake mungu watanzania wote tulisalimika baada ya kukaa majini kwa muda wa siku sita na kati ya watu 22 wenzetu 8 walifariki. tukiachia story hiyo turudi kwenye uzembe . kisheria kabla ya ajali captain alibidi aite mabaharia wote kuwaeleza hali halisi na nini cha kufanya huku akiomba msaada wa simu S.O.S .2 ilibidi mabaharia washushe life raft(kama anavyoita ndugu Rashid turubai)majini na kuwagaia abiria wote majacket(life jackets) kabla ya kutoa order ya kujitosa na wao maofisa na mabaharia kuwa watu wa mwisho inaonyesha hilo halijafanyika walianza kujitosa mabaharia kabla ya abiria.3 kisheria kwenye meli lazima ziwepo flash flash(miale) inaonyesha zilikuwa hazijawashwa na kurushwa hiyo inasaidia kuonyesha eneo la meli ilipo ndio maana walishindwa kuonekana nadhani hilo pia halijafanyika pengine kulikuwa na meli au wavuvi karibu ambao wangesaidia kuokoa baadhi ya abiria 4 kisheria kila jacket lazima liwe na tochi(water proof) na firimbi inaonyesha kwenye jacket hakukuwa na vitu hivyo na pia idadi ilikuwa ni ndogo kuliko idadi ya abiria.5 kila meli ina alama ya mistari chini hiyo inaonyesha kama imeover load au la. na kabla ya meli kuondoka bandarini ofisa muhusika wa bandari anatakiwa kuchunguza uwezo wa ubebaji wa meli (uzito wake na ubebaji wake ) kama uzito umezidi meli hairuhusiwi kuondoka bandari nalo hilo pia halijafanyika 6. kwa mtazamo wangu wa picha ya meli inaonyesha moja kwa moja kuwa meli iliundwa kama kivuko na sio kama meli ya abiria inabidi chombo husika cha leseni kinabidi kiwajibike kwa kutoa leseni na kuruhusu meli ya mizigo kubeba abiria. mwisho baada ya kupoteza roho za marehemu wasio na hatia inabidi Maofisa wanao husika na kutoa leseni, maofisa wa kampuni ya meli,maofisa wa bandari ,maofisa wa meli kama walio salimika wote wachukuliwe hatua hiyo itakuwa ni fundisho kwa wote wanaohusika na wenye vyombo vya usafirishaji ama sivyo kila mwaka tutapoteza wapendwa wetu kwa uzembe wa wachache.
ReplyDelete