Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Well done Gado! Hawa vibaraka wa NTC ya Libya ni wauaji wakubwa na wabaguzi wakubwa wanaoendelea kuwatesa na kuwaua watu weusi Libya wasio na hatia. Hiyo ndiyo tathmini ya Amnesty International na Human Rights Watch. Hao NTC wajue kuwa enzi za apartheid na utumwa zimekwisha. Lakini wajue kuwa atatokea Gaddafi mwingine ambaye atakomesha ubaguzi wao dhidi ya ndugu zetu weusi kama vile Muammar Gaddafi alivyopiga marufuku utumwa Libya 1969. This is what I call FALSE START IN LIBYA. J. Ngowi, Arusha.

    ReplyDelete
  2. Jana nilikuwa nasoma habari kwenye bbc.co.uk na aljazeera.net nikastushwa kusoma kuwa walibya weusi na Waafrika kutoka nci za kusini ya sahara walioko libya wanaendelea kuuwawa. mbona hatusikii nato wakiwashutumu serikali mpya ya libya kwa kuua watu weusi? je nato wanatumia vigezo gani kukuza haki za binadamu? au rangi ya ngozi ya mtu ndiyo kigezo chao?

    ReplyDelete
  3. Duh! hii kali Gado. Kwa kweli umeipatia kisawasawa.

    Nawapa pole wale waLibya masikini ambao tayari wameanza kubaguliwa kwa rangi zao.

    ReplyDelete
  4. Kwa mujibu wa mwanafunzi mmoja wa Libya hapa ukerewe anasema kuwa Gaddafi alikuwa anawatumia sana watu weusi kuwatesa Walibya na pia aliwaajiri kama majeshi ya kukodiwa wakati huu. Aidha, anasema ya kuwa Gaddafi alikuwa akitumia pesa nyingi kuzipa nchi za kiafrika badala ya kuzitumia hizo pesa kwa Walibya. Ndio maana sasa na wao wanalipiza KISASI.

    ReplyDelete
  5. Waafrika hatueleweki Gadafi si mulikuwa mukimuona kichaa ? Nakumbuka huyu huyu GADO alichora kikatuni kuhusu Gadafi alipotoa maoni kuwa Nigeria igawike ili kumaliza mapigano ya kidini, katunin nyengine kadhaa za kumu potrait Gadafi kama ni kichaa tu na hafai kuwa mkuu wa AU.Sasa kioneni.

    ReplyDelete
  6. Ubalozi wa Libya nchini unawaunga mkono NTC na ndio maana walishusha bendera ya Libya kabla hata NTC hawajatwaa nchi. Does that mean they support everything NTC does? Like killing black Africans????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...