Na Woinde Shizza,,Arumeru
FAMILIA zaidi ya 200 wilayani Arumeru mkoani Arusha, zipo hatiani kukosa makazi ya kuishi na sehemu ya biashara,baada ya halmashauri ya Arusha kuziwekea alama ya X ikidai kwamba zimo ndani ya hifadhi ya barabara inayotarajiwa kupanuliwa hivi karibuni yenye urefu wa kilometa tatu.
Wakizungumza na vyombo vya habari wananchi hao,wamesema kuwa halmashauri hiyo haikuwatendea haki kwakuwa tangu mchakato mzima wa kupanua barabara hiyo, itokayo Mianzini hadi Timbolo haikuwahi kuwashirikisha zaidi ya kuwawekea alama ya X ikiwataka wabomoe wenyewe nyumba hizo zinazoonekana kuwa ndani ya hifadhi ya barabara hiyo.
Wakitoa malalamiko yao,mmoja ya wananchi hao ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya waathirika,Fanueli Lamai alisema kuwa , wao hawazuii kupanuliwa kwa barabara hiyo ila kinachomshangaza ni kutaka kujua anayewalipa fidia zao kwa nyumba zao zitakazovunjwa.
Alisema kuwa, pia wamekuwa hawashirikishwi katika mchakato huo wa upanuzi wa barabara na wala hawajui atakayewalipa fidia iwapo watapisha kwa hiari yao upanuzi wa barabara hiyo.
Aidha alisema kuwa, wanahitaji kuundwa kwa tume itakayoratibu utaratibu na kufuatailia mwenendo wa upanuzi wa barabara .
‘Unajua sisi tunapenda maendeleo sana kwa ajili yetu pia kwani barabara itakapopanuliwa ni mafanikio yetu pia ila kinachotupa wasiwasi ni nani atakayetulipa fidia zetu jamani na swala hili mbona hatushirikishwi tukiwa kama wananchi ambao ndio walengwa’alihoji .
Alifafanua zaidi kuwa, mwaka 2006 halmashauri hiyo iliwawekea alama ya X ambapo hawakupingana na kitendo hicho badala yake walitoa ushirikiano kwa kuvunja nyumba zao sehemu iliyozidi ,na kwamba alama hiyo tena imewekwa mapema mwezi huu ikisisitiza wavunje ambapo kwa mwaka huu alama hiyo imeingia ndani zaidi kuliko walivyotegemea.
Aliongeza kuwa, hatua hiyo imepelekea kwa miongoni mwa wananchi kuingiwa na wasiwasi mkubwa kwani iwapo watavunja baadhi yao watakosa makazi kutokana na nyumba zao kumezwa na sehemu kubwa ya upanuzi wa barabara hiyo.
Alisema kuwa , athari hiyo ya bomoa bomoa itazikumba kata za Kiranyi, Olturoto , Moivo na Ilkiding’a ambapo wananchi hao walidai kuwa kuvunjwa kwa nyumba hizo kutawaathiri wananchi walio wengi na kukosa makazi ya biashara kutokana na nyumba nyingi kujengwa karibu na hifadhi ya barabara hivyo kusababisha baadhi ya walio wengi kukosa makazi ya kuishi endapo hawatalipwa fidia.
Kwa upande wa mkurugenzi wa halmashuri ya Arusha, Khalifa Ida aliwataka wananchi hao kufuata utaratibu na sheria za kubomoa nyumba zote zilizozidi kwenye hifadhi ya barabara kwa kuwa mpango huo ni wa muda mrefu na kila mwananchi wa eneo hilo alifahamishwa.
‘Ninyi waandishi wa habari saidieni kuwaelimisha wananchi ambao wamewekewa alama ya X kutii sheria kwa kuwa nyumba zao zimejengwa ndani ya hifanyi ya barabara ili waweze kuzibomoa bila kushurutishwa .’alisema Ida.
Aidha alisema kuwa, mchakato wa upanuzi wa barabara hiyo utakapoanza watashirikishwa kupitia uongozi wao wa kijiji na kata .


CCM Oyeeee?? Oyeeeee !
ReplyDeleteKikwete Oyeee?? Oyeeee !!!
Michuzi Blog Oyeee??? Oyeeee
Watanzania Wote Oyeeee??? Oyeeee!!
Hahaha haaaa
Chimba chimba Oyeee!!!
Mdau wa Kilosa
But jamani hivi huu ni utaratibu mzuri kweli? Mbona serikali yetu haitumii Geography? Wanasubiri hadi wananchi wanamaliza kujenga ndo wanakuja na utaratibu wao. As if hawakuwepo hizo nyumba zikijengwa, upuuzi mtupu tena haina cha usomi wala cha hekima hapo. Kujenga nyumba is a lot of money na maisha ya Watz yalivyokuwa magumu!!!!!!!. Msiondoke hadi kieleweke nanyi Watz mmezidi kuwa wapole, wapigeni mawe kama walivyofanya wameru(it was good example) Michuzi usinibanie please hata kama nimechafua hali ya hewa
ReplyDeletesio sawa kabisa kubomoa nyumba za zamani kwanini wasipanuke kwenda nje ya mji kukawa na old town na mji mpya uliopangwa vizuri kuliko kuvunja nyumba za watu au za zamani watu watoe wapi tena pesa ya kununua viwanja na kujenga upya na maisha yenyewe ndio haya haya heleweki jamani embu nyie viongozi jiwekeni kwenye hayo mazingira muone jinsi gani watanzania wa kawaida wanavyoishi kwa tabu embu acheni kujifikiria wenyewe nyie viongozi wa Tanzania kuweni na ubinadamu na kuweni wagundizi sio kung'ang'ania sehemu moja jaribuni kupanga miji sehemu zingine na sio kubomoa majengo ya zamani.
ReplyDelete