CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA MOSCOW-URUSI wanatoa pongezi kwa timu ya mpira wa miguu ya watanzania waishio nchini URUSI-MOSCOW iliyoingia fainali ya kombe la dunia kwa kufungwa goli 1-0 na timu ya IVORY COAST mechi iliyochezwa katika uwanja wa CHUO KIKUU CHA URAFIKI-LUMUMBA siku ya jumapili tarehe 04/09/11.
Timu hiyo ilijitahidi sana kucheza vizuri na kuweza kuingia katika fainali hiyo na hivyo basi kuitangaza TANZANIA katika nyanja ya kimataifa katika masuala ya mpira na kiutamaduni pia.Hivyo basi CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA MOSCOW linaipongeza timu hii ya taifa ya watanzania MOSCOW-URUSI kwa kufanya vizuri katika mchuano huo uliokuwa mkali na wenye mvuto kwa jinsi walivyocheza vizuri katika mechi hiyo.
Pia pongezi ziwaendee mashabiki wote walioshiriki kwa pamoja katika kushangilia katika mechi hiyo kwakuwa ni changamoto kubwa na uhamasishaji wa kutosha na kuweza kuwasaidia wachezaji kucheza kwa ari, moyo, nguvu zote na maarifa ya hali ya juu.
ASANTENI
KATIBU ITIKADI NA UENEZAJI TAWI MOSCOW-URUSI
KOLOWA.K.M
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA
“KWA KISHINDO TUTASHINDA”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...